Askari anapotumia silaha ovyo mtaani, anawakomaza na kuwapa ujasiri wananchi

Bururu

JF-Expert Member
May 21, 2016
877
584
Tusipokuwa makini Watu watazoea miito ya Bunduki na kuona ni jambo la kawaida.Ikifikia hapo Kwishenea Aman.
 
Hatujaanza leo kuona au kusikia milio ya bunduki au mabomu,toka enzi za Avaloni,New Chox Starlight mpaka leo mubashara kwa Adam Malima
 
Mwigulu wizara imemshinda au ameishindwa. Baki na mbwembwe na kuvaa Bendera tuu
 
Mwigulu wizara imemshinda au ameishindwa. Baki na mbwembwe na kuvaa Bendera tuu
Lini aliiweza?
Miaka miwili nyuma huyu kalalamikiwa sana kwa vitendo vyake alivyokua katibu msaidizi ccm,hebu kumbukeni kdg,alikua anampandisha jukwaani yule mmlemavu wa USO,na mengine mengi ( hebu kumbukeni)
 
Tusipokuwa makini Watu watazoea miito ya Bunduki na kuona ni jambo la kawaida.Ikifikia hapo Kwishenea Aman.
Tumeisha zoea mkuu maana siku hizi bastola imekuwa kama fasheni fulani hivi ya kumtishia mwenzako hata kama unamzidi nguvu na hii nadhani maadili ya utumiaji wa silaha umezidi kuporomoka siku hadi siku. Mamlaka husika ya udhibiti wa silaha mnaliona hilo au nanyi mpompo kama ilivyokuwepo cda.
 
Ndg zangu,

Hii tabia ya wananchi kutishiwa silaha ovyoovyo,haikubaliki kabisa. Siku hizi askari wanatoa silaha ovyo na kutishia watu mtaani bila uwepo wa hali ya hatari.Jeuri hiyo nani anawapa? Wananchi wakishazizoea bunduki nn kitakachofuata?

Mh Nape alitishiwa bastola bila sababu ya msingi.Jana Adam Malima nae hivyohivyo Askari amemfyatulia risasi mbili za SMG.Hii siyo sawa kabisa.

Sasaiv mara Panya road,mara Kibiti, mara Mkuranga.
Jana nimeshuhudia ukomavu wa watu kuhusu silaha. SMG ilipigwa,watu wakasogea kidogo na kurudi tena,na Adam Malima hakustuka kabisa.Nn maana yake?
1.jpg
nape%2Bbastola.jpg
malima2.jpg
 
Huyo pot hataki kudharaurika ila hizi kazi hizi za majeshi wee acha tuu
 
kama kipimo ni "THE LESSER EVIL" basi malima ndiye LESSER.. kwa kweli polisi kachemka sana kupiga risasi hovyo.
 
Huyu Malima mjinga Sana risasi zinapigwa ndio anazidi kusogea anafikri kuwa risasi inamjua kuwa alishawahi kuwa waziri,kwanza ashukuru askari aliyeshika silaha ni askari mwenye busara,askari anapo piga risasi hewani maana yake anakutishia ukimbiye au usalimu amri ukamatwe kwa Amani.

Lakini Kama utajifanya nunda wa kuto kuogopa risasi,askari anapiga risasi hewani wewe unazidi kumsogelea hiyo ni sababu tosha yakumfanya askari akugonge za kichwa kwa kuwa hiyo ni sababu ya msingi ya kuonekana kuwa ulikuwa unatishia maisha ya askari.

Sababu za kuanza kujadili uhalali wa askari kukupa za kichwa zitakuja baadae wakati ukiwa umefunikwa sanda.
 
T

Tunataka watu majasili kama malima acha uoga bro
 
Back
Top Bottom