tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
skari 15 waliopo mafunzoni katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi, maarufu zamani kama CCP mkoani Kilimanjaro, wamenusurika kifo baada ya gari walilopanda kuhusika kwenye ajali ya uso kwa uso na lori aina ya Fuso.
Tukio hilo lilitokea jana, Jumanne Agosti 12, 2025 katika eneo la Kwa Sadala, Wilaya ya Hai, likihusisha gari la polisi lililokuwa likitoka kambi ya jeshi la polisi wilayani Siha na lori hilo lililotokea upande wa Moshi.
Soma pia: Askari afa kwenye ajali ya gari njia ya Chanika. Alikuwa kwenye gari dogo lagongwa na daladala
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa majeruhi wote wamepelekwa Hospitali ya Wilaya ya Hai kwa matibabu.
Alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa tano asubuhi, baada ya gari aina ya Landcruiser la jeshi la polisi kugongana uso kwa uso na lori la Fuso, na kusababisha majeruhi kadhaa.
RC Babu aliongeza kuwa magari hayo yalikuwa yakitokea pande tofauti; gari la polisi likitoka Bomang’ombe kuelekea mjini Moshi, likiwa limewabeba wanafunzi wa jeshi la polisi kutoka kambini, huku lori la Fuso likiwa kwenye shughuli zake za kawaida likitokea Moshi.
Alisema chanzo kamili cha ajali hiyo bado kinachunguzwa na vyombo husika.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Dk. Emmanuel Minja, amesema walipokea majeruhi 15, ambapo mmoja kati yao amepewa rufaa kwenda Hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi.
Alibainisha kuwa hali za majeruhi wote zinaendelea vizuri, huku baadhi yao wakishonwa majeraha na kupatiwa huduma ya kwanza haraka baada ya kufikishwa hospitalini.
Chanzo: Global online tv