Asilimia kubwa ya wanawake hawana ujasiri wa kununua Condom(salama) dukani(Pharmacy)

Good Father

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
10,321
18,543
Habari zenu wadau,

Niende kwenye mada moja kwa moja, nimefanya utafiti mdogo usio kua rasmi kuhusiana na matumizi ya condom(salama), nimebaini yafuatayo:

Asilimia kubwa ya wanawake hawana ujasiri wa kwenda dukani au pharmacy kununua condom, wengi wao niliowahoji wanadai wanaona aibu sana kuagiza condom dukani.

Katika suala la matumizi ya condom wengi wanadai wanaweza kutumia condom kwa malengo mbalimbali kama vile kuzuia ujauzito au mimba zisizotarajiwa, kujikinga dhidi ya magonjwa yaenezwayo kupitia kujamiana kama VVU, kisonono etc

Kwa upande mwingine, jamaa zangu wa kiume wanadai hawapendi kutumia condom ila kuna wakati wanalazimika kutokana na kuogopa mimba (asilimia kubwa wanasema hii ndio sababu ya wao kutumia condom).

Pia wanadai suala la kununua condom dukani kwao sio tatizo, tatizo ni wakati wa kutumia hizo condom walizonunua, wanadai condom zinawafanya wasi-feel vitu flani kwa usahihi, wengine wanasema wakivaa condom hamu ya tendo inaisha, wachache wamedai wakivaa condom wanajikuta hawamalizi tendo kwa wakati.


Kama nilivyotangulia kusema, huu ni utafiti mdogo na usiokua rasmi, maana yake nilikua nawahoji watu wangu tu bila wao kujua kama kuna utafiti naufanya.

Naleta kwenu wanaJF najua watu mlioko hapa ndio watu walioko mtaani, katika uzi huu mtaongeza dondoo za tafiti zenu na maoni yenu.

Mimi maoni yangu ni haya:
Mwanamke kuona aibu kununua condom dukani ni mtazamo wa zamani, dunia imebadilika sana, ni gharama ndogo kununua condom ila ni gharama kubwa itakayokugharimu maisha endapo utapata maambukizi kama VVU, badilika leo, acha aibu zenye kuleta hasara maishani, ukiona boyfriend wako anakwepa kutumia condom ilihali una mashaka na nyendo zake, au huhitaji kubeba ujauzito jitoe kanunue condom dukani na hakikisha mnatumia condom.

Upande wa wanaume wenzangu, acheni utoto hakikisha unatumia condom endapo unayetoka naye sio mkeo, endapo unakutana na mkeo katika siku hatari hakikisha unatumia condom kuepuka mimba usiokua na mpango nayo, ondoa tabia ya kuamini kwamba matumizi ya condom yanafanya usifeel vitu flani. Kumbuka ni faida zaidi ukiwa salama kwa miaka mingi, kuliko kufurahia maisha kwa miaka michache.

Nawasilisha.
 
Acha kuhamasisha zinaa, watu wasubir mpaka watakapooana dipo wafanye mapenzi,
Acha kujidanganya watu wanafikia mabadiliko ya kimwili kabla ya kuoa au kuolewa, sasa wasipoambiwa ukweli faida iko wapi ilihali watafanya tu hata kama sitaandika huu uzi Jf
 
Mi sijawahi na siwezi, yani mtu anajua kabisa kwamba ndo naenda kukwichi mmmh....
Rafiki angu mmoja ye alikua anaenda pharmacy ananunua box kabisa anakaa nalo ndani
Hata wanaume wengi wakishanunua ni asilimia 25% huzitumia hizo ndomu.

Halafu nakupendaga
 
Ni kazi rahisi kwa mwanaume kumthibitishia muuza kondom kuwa anaenda kula mzhgo lakini ni ngumu sana kwa mwanamke kufanya hivyo kwa kununua kondom kwa ujasiri tena mchana kweupe. acha tu wawe waoga
 
Siendi cha pharmacy wala kwa Mangi wala pm...
Nije kununua pm usiponiona jukwaani utajua tu huyo anakulwa....

No, thank you!!!!
Sasa nikijua kuna tatizo Gani???? Hebu njoo pm upate mzigo
 
Mmmmmmh hiyo ni mitazamo hasi kuogopa kununua k**dom mkuu, mm hata asubuhi naenda wala cna hofu kwani nikwaafya yngu. Ila wanaume walio wngi hawapendi kutumia jambo ambalo ni hatareeeeeee
 
Aisee siogopagi kuuliza yaani, nikifika tu nauliza muuzaji " una aina gani ?"

dah kitambo sijanunua hii kitu.

Note: kwa usalama wa afya yako mwanamke ndo mwenye wajibu wa kununua na kusisitiza kutumia.
 
Back
Top Bottom