matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,587
- 15,373
Mama mmoja muuza mchicha Rafiki yangu aliwahi kuniambia. Jiji la Dar es Salaam halitaki mtu mvivu au mgonjwa. Ukishinda hapo huwezi kulala njaa.
Kuna huyu Muha na yeye akaniambia alipofika DSM alianza kuishi kwenye karavati maeneo ya external hadi alipotoboa. Leo ananyumba Kubwa tu.
DSM ndio unapatia michongo ya nchi nzima.
Huyu yeye alikuwa houseboy wa Mchungaji fulani. Leo ni graphics designer ambaye hajui hata adobe Photoshop inafananaje. Yeye anachojua nani anataka nini na yeye anahakikisha anapata solution ya anaychotaka hata kwa Kukodi designers. Haishiwi huyu mchicha.
Huyu ananiambia siku anafika DSM alitaka kulia. Kila anakopita anaona ni mahela tu yako nje nje.
Huyu alikuwa form four failure, alipokutana na wachina Leo bila digrii ni construction engineer anayesimamia matechnician na miradi mikubwa ya hao wachina bila kuharibu.
Core values za mdareslam aliyetoka kwa mujibu wa mama muuza figiri, mchicha, mnamfu, gwasi na tembere ni
1: Usiwe mvivu, amka MAPEMA.
2: Hakikisha huuguiugui. Linda afya.
3: Usiwe teketeke force mambo hadi yawe.
4: usiwe na kinyaa au aibu wala usiogope mtu.
5: uwe na utayari kufanya chochote kwa schedule yoyote.
6: usiongeeongee sana, piga kazi kimya kimya.
7: Unyumbuke, usiwe yabisi. Ukisikia kuna mchongo Mkoani kapige fasta kisha rudi kwenye bezi yako.
8: Ukitaka kutoka haraka usipitwe na habari sahihi. Achana na masiasa, ugomvi wa wanawake. Wewe hakikisha tu unafuatilia habari zinazoweza kukuvusha. Mali Mpya, chimbo jipya, semina za maana, mikutano inayokutanisha watu wengi. Pia achana na mambo ya ndugundugu sijui flani nilisoma naye huko wapi. Kuwa na tabia za kiUS yani tafuta link za kimaslahi tu.
Haipiti muda utaitwa freemanso. Maana lazima utoboe.
Vijana mnafeli nini hapo jijini...