Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,806
- 15,366
Jambo moja ambalo wengi hamlijui ni kwamba, takriban asilimia tisini ya Watanzania wamejikuta tu wakiwa ni wafuasi wa dini hizi za mapokeo yaani Uislamu au Ukristo sio kwa utashi wao, bali kwa utashi wa wazazi, au walezi wao, yaani kwa kuwa wazazi au walezi ni wafuasi wa dini fulani, watoto hawawezi kwenda kinyume na imani za wazazi au walezi wao. Asilimia kumi waliobaki wapo kwenye dini hizo kwa kimaslahi zaidi, kama sio kwa sababu za kielimu basi yaweza kuwa kwa ajili ya mke, mume au hata ajira……………..
Kama mnavyofahamu, kuna baadhi ya watu walijikuta wakibadili dini ili kuweza kupata elimu kutokana na mfumo wa kielimu uliokuwepo kipindi cha ukoloni. Na pia wapo waliobadili dini sio kwa sababu ya utashi wao, bali ni kwa sababu ya kupata ridhaa ya kuoa au kuolewa. Na wapo waliolazimika kubadili dini ili kupata ajira mahali fulani kulingana na sera za taaisisi husika. Na ndio maana nikasema ni kwa sababu za kimaslahi zaidi…………………………..
Nimewaza tu kwa sauti……………………