Asilimia 75 ya wanawake/wasichana wanakiri simu zinavunja mahusiano yao

baptist

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
426
255
34922_439584870971_742520971_5779673_6776129_n.jpg

Kama simu yako ya mkononi haikatiki kiganjani mwako muda wowote, inaweza ikawa inaharibu uhusiano wako na umpendaye. Wanasaikolojia wamesema kuwa watu wengi kwa sasa wanalazimika kushindana na smartphone za wapenzi wao kupata attention.

Utafiti uliofanywa, umebaini kuwa robo tatu ya wanawake wanaona kuwa smartphones zinaingilia maisha yao ya mapenzi na kupunguza muda ambao wangetumia kuzungumza au kuwa karibu na wapenzi wao. Wanasayansi wamedai kile walichokiita ‘technoference' kina madhara makubwa kama migogoro mingi, kupunguza quality ya uhusiano, kupunguza mridhisho wa maisha na hatari kubwa ya msongo wa mawazo.

Utafiti huo ulifanywa na mwanafunzi wa chuo kikuu cha jimbo la Pennsylvania, Marekani na mwingine wa chuo kikuu Brigman Young University cha Utah na kuhusisha wanawake 143.

Asilimia 62 walisema teknolojia imeingilia muda waliotumia pamoja na wapenzi wao na theluthi moja wakisema boyfriend zao waliangalia smartphone wakati wakizungumza.

Wanasayansi hao wameshauri kuweka simu silent na kutokuwa nazo muda wote ili kuwa na muda wa kufocus kwa mpenzi wako. "Kama unataka kuangalia kitu muhimu, toa maelezo kwanza na kisha angalia simu yako.

Na pia usijitetee pale mpenzi wako akionesha kukerwa na tabia yako ya kuangalia sms au kucheza games mara kwa mara – ni njia ya yeye kusema kuwa angetaka kuconnect na wewe moja kwa moja," wamesema.



Source: Bongo 5
 
vere true, hadi nammiss my dia nokia tochi, hii smartphone hapa ndani ishakuwa kama mke mwenzangu vile

Shost bora wewe imekuwa mke mwenzio, mie imekuwa mume. Yaan bora nimkose mume lakini smartphone yangu iwe karibu.

Nikizinguliwa kidogo tu naitafuta ilipo naingia net full kucheka utadhani kuna mwanaume mwingine huku!
 
Shost bora wewe imekuwa mke mwenzio, mie imekuwa mume. Yaan bora nimkose mume lakini smartphone yangu iwe karibu.

Nikizinguliwa kidogo tu naitafuta ilipo naingia net full kucheka utadhani kuna mwanaume mwingine huku!

si bora hata wewe aisee, unajua simu ikifanywa mke mwee lakini?
muda wote imepakatwa mi sijui hata mara ya mwisho nimepakatwa lini, inaangaliwa kwa tabasamu,inaekwa kifuani aroooo inapewa maupendo mi si ya kitoto
 
Yaani aliyegundua hizi smartphone nampenda sana ukiwa a stress tu ingia net unacheka had basi.
 
Simu ni mbaya, especially smart phones. Watu tumekuwa tuna uhusiano mzuri na simu zetu pengine zaidi ya marafiki ama wapenzi wetu wanaokuwa pamoja nasi kwa muda huo.

Kitu muhimu kufanya ni kuzima simu pale tunapokuwa katika mazungumzo na wenzetu,hususan baada ya kazi.

Tatizo ni je, unapozima simu, huleti hisia mbaya kwa mwezanko, especially akiwa mpenzi wako? Si aweza kukwambia kuna kitu wataka kumficha?
 
Duh! Sipati picha huyu jamaa kwenye picha hapo juu alichokuwa anaongea, ila jinsi demu hapo nyuma alivyo, hiyo simu ikikatwa tu, kuna kimbembe!
 
Ukitazama vizuri simu zinaathiri pande zote. Rejea wimbo wa Rose Mhando, 'facebook'
^^
 
Huu utafiti haujanlenga mimi.hao wanaona smartphone ndio kila kitu yaani Me au KE ni washamba tuuh.
 
Ni ukweli usiopingika hizi smat foni zimepunguza mahusiano katika familia, mke na mume, mama na watoto wake au baba na familia yake watu hata kwenye madaladala watu hawazungumzi kabisa yaani hata kumsalimia mtu ni kazi wote wako bize wanachat nadhani ni lengo la wazungu tusiwe na mahusiano ya kudumu tuwe na ndoa za mikataba kama kwao
 
Back
Top Bottom