Asilimia 62 ya wanaume wamekiri kutonawa mikono pindi wanapotoka chooni

BigBaba

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
1,908
9,040
5272121717d4de2549a0e8be9c4642bf.jpg



Asilimia 62 ya wanaume na asillimia 40% ya wanawake duniani wamekiri kutonawa mikono pindi wanapotoka chooni. Hali hiyo inapelekea 80% ya maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya tumbo. Watanzania tujenge mazoea ya kunawa mikono baada ya kutoka chooni.
 
Bila shaka huo utafiti umefanyika Marekani, Maana wao wakitoa utafiti ndio utasikia neno 'Duniani'.

Na Waafrika huwa tunazibeba kama zilivyo....

Hii inanikumbusha Waliosema Beyonce ndio mzuri kuliko wote duniani. Na Watu wakakubali kuwa ni kweli.

Waafrika tuacheni ujuha sio kila utafiti utakaofanyika Ulaya na Marekani basi Ujumuishe Ulimwengu mzima.
 
huu utafiti ni wa ukweli tusiwe wabishi mara masela huenda kukojoa wala huwa hawanawi mikono wakitoka huko chooni
 
Hata hao 38% wamedanganya tu. Kundi kubwa la wanaume tukimaliza kususu hatunawi mikono licha ya kushika kambale!
 
Ila msemakweli mpenzi wa MUNGU.....huu utamaduni ni tatizo kubwa kwetu wanaume. Na kila mmoja anajua hilo. Hapa tutabisha tu kujitutumua
 
Back
Top Bottom