Asilimia 20 ya watanzania hawajui kusoma na kuandika, aibu kwa taifa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Asilimia 20 ya watanzania mbumbumbu, aibu kwa taifa

pic+mbumbu.jpg

Kwa ufupi
Serikali ilikiri hivi karibuni bungeni kuwa Watanzania wasiojua kusoma na kuandika, wamefikia asilimia 20.
By Tumaini Msowoya, Mwananchi tmsowoya@mwananchi.co.tz
Sifa ya Watanzania kujua kusoma na kuandika duniani imepotea. Ni sifa hii iliyoipandisha chati Tanzania miaka ya 1980 kiasi cha kufikia kupewa tuzo maalumu na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco).
Miaka hiyo kiwango cha Watanzania kujua kusoma na kuandika kilikuwa zaidi ya asilimia 80. Shukrani kwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) na uongozi thabiti wa awamu ya kwanza, kwa kuwa chachu ya Watanzania kufuta ujinga.
Miongo takriban minne baadaye, Watanzania wanaonekana kupoteza sifa hii. Kila siku watu mbumbumbu wanaongezeka.

Asilimia 20 ya Watanzania ni mbumbumbu
Akizungumza bungeni hivi karibuni, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Stella Manyanya alisema asilimia 20 ya Watanzania hawajui kusoma na kuandika.
Alitoa takwimu hiyo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalum Tasca-Restuta Mbogo (CCM) kwa niaba ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Katika swali lake, Mbogo alihoji kama kuna mpango wa Serikali kurudisha elimu ya watu wazima iliyokuwepo miaka ya nyuma.
Ripoti ya Unesco) inasema watu wasiojua kusoma na kuandika duniani wanafikia 774 milioni. Ripoti hiyo inaeleza wazi kuwa watu hao wengi wanaishi katika mabara ya Afrika na Asia. Haya ndiyo mabara yenye changamoto nyingi za kielimu, ikiwamo uwekezaji mdogo unaofanywa katika sekta ya elimu.
‘’Fedha zinazotengwa kwa ajili ya elimu ni ndogo. Serikali nyingi zimeongeza matumizi, lakini ni chache tu ndizo zimeipa elimu kipaumbele kwenye bajeti zao za taifa, na zilizo nyingi zinashindwa hata kutenga asilimia 20 iliyopendekezwa ili kufidia upungufu wa fedha,’’ inasema ripoti ya Unesco kuhusu ufuatiliaji wa Elimu kwa Wote: Mafanikio na Changamoto (2005-2015)

Doa kwa Taifa
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa, Dk Jimson Sanga anasema ni aibu kwa Taifa kuwa na idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma wala kuandika.
“Nchi kuwa na watu wasiojua kusoma wala kuandika ni kujipalilia umaskini. Tukiwa na watu wengi wasio na maarifa, hawatoweza kuzalisha; watakuwa watumwa,” anasema.
Kwa mtazamo wake, hali hii ni dalili za kushindwa kwa vita ya kupambana na ujinga.
“Kutojua kusoma wala kuandika ni janga, tena bora kwa watu wazima kuliko kuwa na watoto wanaomaliza darasa la saba lakini hawajui kusoma wala kuandika,” anasema.
Meneja Miradi wa Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten\Met) Nikodemus Eatlawe, ana wasiwasi kuwa huenda tatizo ni kubwa zaidi kuliko takwimu zilizotolewa.
“Nenda kule Umasaini, katafute idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika; utashangaa, bado wapo wasiojua kusoma na kuandika,” anasema
Anasema kujua kusoma na kuandika ni hatua moja. Hatua ya pili ni hao wanaojua kusoma na kuandika kupata mwanga wa kuendesha maisha yao kwa kuweza kupambana na umaskini.
“Elimu inasaidia kuondokana na ugumu wa maisha, ikishindwa kufanya hivyo haitakuwa na maana.
Mbumbumbu shuleni
Wakati hisia za walio wengi ni kuwa pengine asilimia 20 iliyotajwa inawahusu zaidi watu wazima waliokosa fursa za elimu zamani, ukweli ni kuwa hata wanafunzi walio shuleni baadhi hawana ujuzi wa kutosha wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
Tafiti nyingi zikiwamo zile za Uwezo zinazoratibiwa na shirika la Twaweza, kwa miaka kadhaa zimekuwa zikionyesha ukubwa wa tatizo kwa wanafunzi wa shule za msingi.
Kwa mfano, katika ripoti ya tathmini ya Uwezo yam waka 2017, idadi kubwa ya watoto wenye miaka kati ya tisa na 13 walishindwa kufanya majaribio ya darasa la pili, huku utofauti ukiwa mkubwa kati ya wilaya na wilaya.
“Mwanafunzi mmoja kati ya 10 wa darasa la tatu alikuwa ana uwezo wa kusoma hadithi ya darasa la tatu, huku watano kwa kila wanafunzi 10 wa darasa la saba waliweza kufanya hivyo,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo iliyotolewa Aprili 2018.

TEWW yatwishwa mzigo
Dk Sanga anasema huu ni wakati mzuri kwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kuandaa mkakati wa kusaidia kupunguza idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika.
Anasema ujinga ni adui mkubwa wa maendeleo na kama watu wengi watakuwa hawajui kusoma wala kuandika, sio rahisi kufikia Tanzania ya viwanda inayotarajiwa.
“Kama mtu hajui kusoma na kuandika anawezaje kupambana na umaskini? Mwalimu Nyerere alipigana na maadui watatu kwa sababu hao wanaenda pamoja,’’ anaeleza na kuongeza:
“Hakuna namna zaidi ya kurudi darasani, lazima kuwe na madarasa ya watu wazima kwa sababu kutojua kusoma na kuandika kwa zama hizi ni hatari zaidi.’’
Akifungua mkutano wa nane wa Baraza la Wafanyakazi wa TEWW mwaka 2017, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo aliitaka taasisi hiyo kuandaa utaratibu mzuri wa kuwafikia wananchi wengi ambao hawajui kusoma wala kuandika.
Alisema ongezeko la wasiojua kusoma wala kuandika linaelekea kuwa tatizo kubwa na kuitaka taasisi hiyo kubadili namna ya kuendeleza kampeni za kimasomo na kutoa mafunzo kwa wawezeshaji wa programu za kisomo ili kukabiliana na tatizo.

Mkakati wa TEWW
Kaimu Mkurugenzi wa TEWW, Dk Kassim Nihuka anakiri kwamba lipo tatizo la watu kutojua kusoma wala kuandika nchini.
“Sensa ya mwaka 2012 ilionyesha kwamba asilimia 22 ya Watanzania hawajui kusoma wala kuandika na takwimu hizo kwa sasa zinaongezeka,” anasema.
Anasema tayari taasisi hiyo imeandaa mkakati wa kitaifa wa kukuza kisomo na elimu kwa umma, unaolenga kukuza stadi za kimasomo kwa vijana na watu wazima wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu nchini.
“Huu mkakati utaanza mwaka 2019 na nia ni kuhakikisha Watanzania wote wanajua kusoma na kuandika,” anasema.
Mkakati huo anasema utatekelezwa kupitia programu mbalimbali na kwamba maandalizi yake yamekamilika…. “Tayari tumeshaandaa mitalaa, mihutasari na vitabu kwa ajili ya kuanza kazi hii,” anaeleza
 
Kijana tunaomba passport yako
 
ndio kura za chama chetu hizo jmn

Harro mura,
Hii rimenifungua macho mura....kumbe zire kura mirioni 8 arizopata Magufuri ni za hawa Watz mambumbumbu...!!!
Hakika huo ni mtaji mkubwa sana kwa CCM na ndo maana kwa sasa kuna juhudi kubwa sana za kutaka kuwanyamazisha watu wenye akiri wasiseme au kupiga kerere maana wanaweza kuwafanya hata hao ma-mbumbumbu wa CCM wanaweza kuerevuka na kurikataa rijitu hiri au haya majitu yote ya CCM mura..!!!
 
Acha kupotosha kwa kutumia takwimu! Kwenye hizo asilimia 20 wapo walozaliwa leo ambao hata popote pale hawawezi jua hata kutamka neno! Wanchojua ni kulia tu. Inatakiwa useme ni asilimia 20 ya umri upi. Mnaboa kila wakati mnarukia vitu hamvijui mnapotosha Umma ndo maana Sheria ya Takwimu imewekwa viraka
 
Harro mura,
Hii rimenifungua macho mura....kumbe zire kura mirioni 8 arizopata Magufuri ni za hawa Watz mambumbumbu...!!!
Hakika huo ni mtaji mkubwa sana kwa CCM na ndo maana kwa sasa kuna juhudi kubwa sana za kutaka kuwanyamazisha watu wenye akiri wasiseme au kupiga kerere maana wanaweza kuwafanya hata hao ma-mbumbumbu wa CCM wanaweza kuerevuka na kurikataa rijitu hiri au haya majitu yote ya CCM mura..!!!
Ndio hivyo mkuu
 
Haziendani na uhalisia...mnyonge mnyongeni, watanzania 20% kutokujua kusoma sidhani labda kama inajumuisha na watoto ambao hawajaanza shule

Halafu watanzania wa miaka ya 80 ambayo ni miaka ya giza sana kuwazidi watanzania wa mwaka 2018 ni hadithi nyingine, nadhani waliokuewepo mika hiyo wataweza kushuhudia
 
Back
Top Bottom