Asili ya nchi ya Afrika ya Kusini

Asili ya nchi ya Afrika ya Kusini

Kitang'wa1

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2014
Posts
460
Reaction score
285
Habari za muda huu jamani.

Nina jambo huwa linanitatiza kutaka kulijua, yaweza kuwa lilishajadiliwa humu, ila binafsi sikuliona likijadiliwa humu, kama tayari basi si vibaya mkanijuza nami, hasa kwa wale wajuzi wa mambo mbali mbali.

NAPENDA KUJUA, NI KWA NINI NCHI YA AFRIKA KUSINI, HAINA JINA LAKE HALISI, JAPO TUNAJUA YA KUWA IPO KUSINI MWA AFRIKA, LAKINI NCHI ZILIZOIZUNGUKA NCHI HIYO KUSINI HUKO HUKO ZINA MAJINA YA NCHI, MFANO ZIMBABWE NA LESOTHO, ILA KWA AFRIKA KUSINI IMEBAKI HIVYO HIVYO, JAPO KUNA MAJINA KAMA YA A.K.A VILE, (kwa Madiba, Bondeni, n.k), ILA NAAMINI SIYO RASMI.

NI KWELI NCHI HIYO HAINA JINA LAKE LA ASILI?!

NAOMBA KUJULISHWA TAFADHALI.

Ahsante!
 
Jina mbona lipo inaitwa Dizonga...tatizo ni nani anayetoa jina la nchi kwahiyohiyo mfano uliyotoa
 
Dizonga - daah ahsante sana mkuu, ngoja labda watakuja wengine kutuambia, kwa nini hili jina siyo maarufu.

Duh!!!! Dizonga!!!! Hilo ni jina wabongo wa Sauzi wanapenda kuiita ile nchi. Mie nimeishi huko kwa muda mrefu na nimeoa huko, japo kwa sasa ninaishi bongo na huyo waifu na watoto niko nao hapa Bongo. Nakubaliana na wewe majina yapo, ila hawakubaliani nayo kwa sababu ya nani anayatoa. Wazulu, WaXhosa, Waswati, Wandebele wanaiita Mzantsi Africa, Watswana, Wasotho na Wapedi wanaiita Africa Borwaa, Watsonga wanaiita nDizimu Africa, WaAfrikaneer wanaiita Zeid Afrikanche, na Waingereza wanaiita South Africa. Maana ya majina yote hayo,ni moja yaani Africa ya Kusini. Ila, kuna jina ambalo wote wanalikubali ambalo inasemekana lilikuwa linatumika sana enzi za kugombania uhuru wao,nalo ni Azania. Tatizo hilo jina lilitumiwa sana na wapigania uhuru wa vyama vya Azapo ( Azanian Peoples Organization) na PAC ( Pan Africanist Congress of Azania) wakati ANC ( African National Congress) walitumia South Africa. Sasa ANC haitaki kutumia jina la Azania kwa sababu itavipa hivyo vyama credit zaidi. Kwa kweli kuna mgongano na mgogoro mkubwa sana huko juu ya jina la Africa ya Kusini. Weusi wanataka nchi yao itambulike kwa jina la asili yaani Azania badala ya eneo la kijiografia yaani Afrika ya Kusini. Inasemekana pwani ya kuanzia Durban kwenda Xhluxhluwe, Port Alfred, Port Shepstone, mpaka Port Elizabeth, hadi Cape Town zamani sana ilijulikana kama Pwani ya Azania.
 
inaitwa South Africa, ndio jina lake, wala sio Afrika kusini, wenyewe hawajui kama kuna kitu kinaitwa Afrika kusini.pia kuna nchi nyingine inaitwa central Africa
 
Duh!!!! Dizonga!!!! Hilo ni jina wabongo wa Sauzi wanapenda kuiita ile nchi. Mie nimeishi huko kwa muda mrefu na nimeoa huko, japo kwa sasa ninaishi bongo na huyo waifu na watoto niko nao hapa Bongo. Nakubaliana na wewe majina yapo, ila hawakubaliani nayo kwa sababu ya nani anayatoa. Wazulu, WaXhosa, Waswati, Wandebele wanaiita Mzantsi Africa, Watswana, Wasotho na Wapedi wanaiita Africa Borwaa, Watsonga wanaiita nDizimu Africa, WaAfrikaneer wanaiita Zeid Afrikanche, na Waingereza wanaiita South Africa. Maana ya majina yote hayo,ni moja yaani Africa ya Kusini. Ila, kuna jina ambalo wote wanalikubali ambalo inasemekana lilikuwa linatumika sana enzi za kugombania uhuru wao,nalo ni Azania. Tatizo hilo jina lilitumiwa sana na wapigania uhuru wa vyama vya Azapo ( Azanian Peoples Organization) na PAC ( Pan Africanist Congress of Azania) wakati ANC ( African National Congress) walitumia South Africa. Sasa ANC haitaki kutumia jina la Azania kwa sababu itavipa hivyo vyama credit zaidi. Kwa kweli kuna mgongano na mgogoro mkubwa sana huko juu ya jina la Africa ya Kusini. Weusi wanataka nchi yao itambulike kwa jina la asili yaani Azania badala ya eneo la kijiografia yaani Afrika ya Kusini. Inasemekana pwani ya kuanzia Durban kwenda Xhluxhluwe, Port Alfred, Port Shepstone, mpaka Port Elizabeth, hadi Cape Town zamani sana ilijulikana kama Pwani ya Azania.
Quiniso Nkosi. Ngiyabonga kakhulu ongqongqoshe wami.
 
Mzee wa alizeti umeeleza vema sana. Hongera. Lakini kuna dosari kidogo. Hii inaitwa Afrika Kusini (South Africa), na si Afrika ya Kusini yaani Southern Africa. Ni hilo tu.
 
Duh!!!! Dizonga!!!! Hilo ni jina wabongo wa Sauzi wanapenda kuiita ile nchi. Mie nimeishi huko kwa muda mrefu na nimeoa huko, japo kwa sasa ninaishi bongo na huyo waifu na watoto niko nao hapa Bongo. Nakubaliana na wewe majina yapo, ila hawakubaliani nayo kwa sababu ya nani anayatoa. Wazulu, WaXhosa, Waswati, Wandebele wanaiita Mzantsi Africa, Watswana, Wasotho na Wapedi wanaiita Africa Borwaa, Watsonga wanaiita nDizimu Africa, WaAfrikaneer wanaiita Zeid Afrikanche, na Waingereza wanaiita South Africa. Maana ya majina yote hayo,ni moja yaani Africa ya Kusini. Ila, kuna jina ambalo wote wanalikubali ambalo inasemekana lilikuwa linatumika sana enzi za kugombania uhuru wao,nalo ni Azania. Tatizo hilo jina lilitumiwa sana na wapigania uhuru wa vyama vya Azapo ( Azanian Peoples Organization) na PAC ( Pan Africanist Congress of Azania) wakati ANC ( African National Congress) walitumia South Africa. Sasa ANC haitaki kutumia jina la Azania kwa sababu itavipa hivyo vyama credit zaidi. Kwa kweli kuna mgongano na mgogoro mkubwa sana huko juu ya jina la Africa ya Kusini. Weusi wanataka nchi yao itambulike kwa jina la asili yaani Azania badala ya eneo la kijiografia yaani Afrika ya Kusini. Inasemekana pwani ya kuanzia Durban kwenda Xhluxhluwe, Port Alfred, Port Shepstone, mpaka Port Elizabeth, hadi Cape Town zamani sana ilijulikana kama Pwani ya Azania.

Mkuu imebidi niangalie hela zao ninazo hapa Rand moja upande mmoja imeandikwa Afrika- Dzonga chini Ningizimu Afrika upande mwingine ina picha ya swala na maneno Soli Deo Gloria..Usitupotoshe mkuu hela nying hasa za zamani ziliandikwa hilo jina..
 
sisi ndo tunakosea kutafsiri,kuna tofauti kati ya afrika kusini na afrika ya kusini.south africa na southern africa.ile nchi ni afrika kusini au south africa.afrika ya kusini au southern africa inainclude nchi kama sa yenyewe,lethoto,swaziland,botswana,mozambique
 
Nilikaa cape Town, maeneo ya Belleville na Mitchell's Plain, sikuwahi kujua km kuna mgogoro wa jina la nchi
 
Nakushukuru sana kwa ufafanuzi wako wa kina, hakika najifunza na nitazidi kujifunza mengi.

Ahsante!

Duh!!!! Dizonga!!!! Hilo ni jina wabongo wa Sauzi wanapenda kuiita ile nchi. Mie nimeishi huko kwa muda mrefu na nimeoa huko, japo kwa sasa ninaishi bongo na huyo waifu na watoto niko nao hapa Bongo. Nakubaliana na wewe majina yapo, ila hawakubaliani nayo kwa sababu ya nani anayatoa. Wazulu, WaXhosa, Waswati, Wandebele wanaiita Mzantsi Africa, Watswana, Wasotho na Wapedi wanaiita Africa Borwaa, Watsonga wanaiita nDizimu Africa, WaAfrikaneer wanaiita Zeid Afrikanche, na Waingereza wanaiita South Africa. Maana ya majina yote hayo,ni moja yaani Africa ya Kusini. Ila, kuna jina ambalo wote wanalikubali ambalo inasemekana lilikuwa linatumika sana enzi za kugombania uhuru wao,nalo ni Azania. Tatizo hilo jina lilitumiwa sana na wapigania uhuru wa vyama vya Azapo ( Azanian Peoples Organization) na PAC ( Pan Africanist Congress of Azania) wakati ANC ( African National Congress) walitumia South Africa. Sasa ANC haitaki kutumia jina la Azania kwa sababu itavipa hivyo vyama credit zaidi. Kwa kweli kuna mgongano na mgogoro mkubwa sana huko juu ya jina la Africa ya Kusini. Weusi wanataka nchi yao itambulike kwa jina la asili yaani Azania badala ya eneo la kijiografia yaani Afrika ya Kusini. Inasemekana pwani ya kuanzia Durban kwenda Xhluxhluwe, Port Alfred, Port Shepstone, mpaka Port Elizabeth, hadi Cape Town zamani sana ilijulikana kama Pwani ya Azania.
 
Ndiyo hivyo aisee, nilikuwa najiuliza sana kuhusu hili suala, nashukuru nawe pia hukulijua hili na uliishi huko, ngoja wajuzi waendelee kutujuza.

Back
Top Bottom