Migomba
JF-Expert Member
- Nov 30, 2013
- 945
- 1,334
Majina mawili ya Dk. John Pombe Joseph Magufuli yana historia yake ya jinsi yalivyopatikana.
Majina hayo mawili ‘Pombe’ na ‘Magufuli’ yalitokana na bibi na babu wazaa baba yake Magufuli.
Jina la ‘Pombe’ alipewa na bibi yake kwani wakati anazaliwa bibi yake alikuwa amepika pombe siku
hiyo.
Jina la ‘Magufuli’ lilitokana na babu yake ambaye alikuwa shujaa wa kucheza ngoma za asili aliyepewa jina Magufuli kwani kila alipokuwa akicheza ngoma alikuwa anawashinda wengine hivyo kitendo hicho kilifananishwa na kufuli linavyofungwa mlangoni.