Asili na Sayansi

kafumo

Member
Joined
Aug 30, 2026
Posts
26
Reaction score
15
ASILI NA SAYANSI


Katika maisha haya ya leo tunajua na kufahamu uwepo wa asili na sayansi, asili ni nini na sayansi ni nini, haya ni maswali mtu anapaswa kujiuliza katika safari ya utambuzi binafsi.


Asili ni namna yenye sifa nyingi sana zisizo na mwanzo wala mwisho zenye muunganiko usio kufa daima, wakati sayansi ni taaluma ya kusoma na kuchunguza namna ya asili na imegawanyika katika sehemu nyingi.


Moja ya sifa za asili ni ufahamu mkubwa sana usio weza kuelezeka, ufahamu huu unafanya asili iwe ya siri pamoja na kuwepo kila mahali, asili ni tajiri wa vitu kuliko sayansi, sayansi inafanya kazi ya kuhangaika ili kupata jinsi asili ilivyo katika ukamilifu wake.


Sayansi imefanikiwa kidogo sana kwenye kusoma ufahamu wa asili.

Sayansi imefanya jitihada ya kuiga ufahamu huo na kuunda au kutengeneza mambo mengi tunayo sema ni mambo ya kisayansi au tuna tumia lugha ya ni mambo ya kitaalamu.


Asili kuu haijadiliki kabisa lakini kiufupi hapa tuiseme kwa sifa hizi ni uhai mkuu ,uweza ukuu, wema mkuu wenye viumbe vinavyo onekana na visivyo onekana vyenye namna zinazo onekana na zisizo onekana , vilivyo fanywa na asili kuu yenyewe kwa sheria zake.


SABABU YA SAYANSI KUWEPO NI NINI HASA.

Huwezi kujadili sababu ya kuwepo na sayansi bila kujadili uwepo wa viumbe katika ulimwengu yaani kiumbe mtu na viumbe wengine wa asili.

Sayansi ni maendeleo ya maisha zidi ya kiumbe mtu. Inaweza kuwa ngumu kuelewa hili, ila kwa utulivu na utaratibu, unaweza kuelewa kwa kutambua uwepo wa viumbe wa asili wa jinsi walivyo wa namna nyingi katika asili ukiachana na kiumbe mtu.


Nikisema sayansi ni maendeleo ya maisha zidi ya mtu nina maana ujiulize au ufahamu umaalumu wa kiumbe mtu na thamani aliyopewa na asili kuu na kwa nini viumbe wengine wafanye maendeleo kumlenga.


Kiumbe mtu pamoja na sifa zake lakini kuna jambo la pekee kuhusiana na nishati yake au roho yake, ukiachana na mwili wake.


Utakatifu wa nishati ya kiumbe mtu ndio sababu ya kuwepo kwa sayansi.


Asili kuu ina mamlaka juu ya kila kiumbe chake kinacho onekana na kisicho onekana, kiumbe mtu nishati yake ina sifa kuelekea asili kuu, mamlaka ya asili kuu kidogo ipo ndani ya nishati ya mtu na hivyo kwa kibali cha asili kuu. Mtu ana uwezo na mamlaka kwa viumbe wengine wanao onekana na wasio onekana kwa sababu ya upekee wa nishati yake ya asili kuu iliyo ndani yake.


Siri kuu kwenye nishati ya kiumbe mtu siyo nyingine zaidi ni nishati inayoweza kufikia kiwango cha juu sana kuelekea asili kuu, tofauti na nishati za viumbe wengine viwango vya nishati zao haziwezi kufika kiwango hicho.


Kiwango hicho ni wepesi wa nishati, nishati ya kiumbe mtu inaweza kufikia wepesi ambao sehemu sahihi ya kuishi ni karibu na asili kuu.


Nishati za viumbe wengine hata kwa wema gani haziwezi kupata wepesi huo labda kwa kibali cha asili kuu yenyewe.


Namna ya nishati hizi zinatofautiana kwa asili, nishati ya mtu kwa asili zinasifa ya moja kwa moja na kibali cha kukaa karibu na asili kuu , wakati nishati za viumbe wengine zina nafasi isiyo ya moja kwa moja ya kukaa karibu na asili kuu.


Asili kuu ni ya namna ambayo haielezeki namna ambayo kila nishati ina hitaji kuwa karibu nayo, pamoja na kuwa na hiyo namna isiyo elezeka lakini hakuna majivuno na sifa sitahili ni usafi(wepesi) wa kiwango cha juu.


Uumbwaji wa nishati safi ya mtu hauwezi kuaminiwa moja kwa moja, kama ambavyo hata zana yako mpya ukiitengeneza lazima uifanyie majaribio mengi yakutosha kuiamini katika matumizi yako ya kila siku


Namna ya Asili ni ya ajabu kuu sana isiyo elezeka kabisa, Dunia yetu ni kiumbe kwenye asili. Kiumbe hiki ni kiumbe kina milikiwa na ukuu mdogo unaitwa jua, yaani nyota ya jua , nyota hii ina miliki ukuu zingine ndogo ndogo kwa viwango tofauti kwa idadi isiyo elezeka pia kila ukuu na mambo yake vikiwa na kusudi maalumu kwa jinsi ya asili kuu.


Viumbe huwa katika namna kulingana na mazingira kiumbe kilipo, kwa maana hiyo mwili sio muhimu kwa kiumbe, mwili ni kwa ajili ya makusudi flani kwa kiumbe huyo kwenye namna kinapo takiwa kufanya jambo ambalo utendaji wake katika mazingira hayo unahitaji mwili wa namna hiyo inayoweza kuwa yoyote kutokana asili yake.


Kama unavyo jaribu zana yako ili uiamini kwa ajili ya matumizi ya kila siku, Nishati safi ya kiumbe mtu, ikawepo kwenye mwili ili ifae kukaa mahali karibu na asili kuu , na kufaa huko kufanyike duniani.


Hivyo duniani hapa mtu ana mwili ili roho au nishati yake safi ifae kukaa yalipo makazi yake.


Changomoto na zoezi kubwa ni kufaa huko, maisha ya kiumbe mtu yanaweza kuifanya nishati yake iwe nzito au nyepesi.

Nishati nzito mfano wa moshi mzito ni vigumu sana kupaa, lakini nishati safi mfano wa moshi mwepesi ni rahisi sana kupaa.

Ndio hapa tuna pata hisia na matendo ya namna mbili Wema na Ubaya, pia tunapata semi mbili Mungu na Shetani.

Matendo na maisha ya wema kwa kiwango hicho hicho hufanya roho au nishati iliyo ndani ya mtu huyo kuwa nyepesi kwa kiwango hicho hicho.


Elewa matendo na maisha ya mtu ndio jinsi ya nishati yake. Nishati nzito ni kama moshi mzito itabaki duniani, Nishati nyepesi ni kama moshi mwepesi itapaa haraka kwa kasi iliyo zaidi ya mwanga muda na wakati wa asili unapo fika.


Hivyo unaweza kuona jinsi kiumbe mtu alivyo pendelewa.

Na kupewa nafasi ya kuishi duniani ndio mtihani pekee wa kupata kibali cha kuwepo karibu na asili kuu tofauti na viumbe wengine wa asili hawajapata nafasi hiyo ya moja kwa moja.


Viumbe hao wengine pia wanautambuzi na fahamu za juu kuhusu asili kwa viwango vyao, habari ya kiumbe mtu pia wao wanaifahamu na kuielewa sana.


Viumbe hawa wengine wametii na kukubali jinsi walivyo umbwa na kutii na kuheshimu kuwepo katika namna hiyo, lakini wengine wamepata wivu sana kwamba asili zao hazina nafasi ya moja kwa moja za kuwepo karibu na asili kuu.


Roho hawa ambao wameshindwa kutii na kuheshimu jinsi walivyo umbwa ndio hao waleta shida kwa kiumbe mtu lengo lao kubwa likiwa ni kuhakikisha kiumbe mtu abaki bila kwenda anapo takiwa kwenda na awe kama yalivyo maisha yao hao roho wasio watii kwa asili kuu, na jambo hili wanalitekeleza kwa mbinu nyingi sana hapa duniani.


Asili kuu ikampa kiumbe mtu mazingira hapa duniani na zana zote zimfaazo ili afae atahitaji azitawale azitumie kwa namna yake kila mmoja.


Viumbe au roho wasio watii wakatumia maarifa yao ya asili kuzaliwa na kujifanya viumbe watu katika miili inayo fanana na mtu halisi wa asili, yote ili kumchanganya kiumbe mtu kwa maana kwa namna zao na vitimbwi visivyo onekana, mtu wa asili ni mwenye zana na maarifa ya kuwazibiti kwa kiwango kikubwa sana hapa duniani.


Na hivyo kwa kujifanya kama watu imekuwa rahisi kufanya vitimbwi wakitumia miili kama ya watu wa asili, wanatumia maarifa yao ya asili kuzaliwa kama watu lengo ni kuwa namna hiyo ya mwili, ili kumpoteza mtu wa asili katika usawa wake ili wafanikishe kusudi lao la kufanya mtu wa asili nishati yake isiende pale ambapo wao hawana kibali cha moja kwa moja.


Asili na mazingira ya ulimwengu mahali mtu alipo yana tii mamlaka ya nishati safi ya mtu wa asili, kiasi mtu wa asili akiwa katika uwiano wake wa asili anaweza kutumia zana zote kwenye ulimwengu alipo kwa jinsi na namna ya mpangilio wake.


Asili na mazingira ya ulimwengu mahali mtu wa asili alipo haimtambui mtu asiye wa asili. Na hivyo maisha yake hapa duniani huyo mtu mwenye mwili wa mtu bilia nishati safi ya kiumbe mtu wa asili yangekuwa ya shida sana na rahisi kwa mtu wa asili mwenye nishati safi.


Zamani za kale hapakuwa na vifaa vya sayansi na teknolojia ya sasa lakini kila kitu kilifanyika, watu walitibiwa , walisafiri, waliwasiliana walifanya mambo mengi sana.


Hivyo roho waasi kwa kutumia mwili wa mtu wamefanya mazingira rahisi kwa ajili yao na kumshawishi mtu wa asili kutumia mazingira hayo kuwa ni halali na kuwaaminisha watu wa asili kuwa mazingira ya asili yao hapa duniani ni upotofu, kumbe kwa kuwa roho waasi wenyewe mazingira ya asili hawana mamlaka nayo.


Hivyo ndani ya jamii ya sasa tuna nishati za viumbe watu wa asili na nishati za viumbe wasio watu katika miili ya watu tena kwa kuzaliwa. Nia zao hawa viumbe ndio utofauti na sio kuangalia miili ya watu hii tuliyo nayo.


Kama unaelewa habari hiyo hapo juu basi utatambua kuwa sayansi ni zidi ya mtu wa asili ,na nikwaajili ya viumbe wasio na uwezo na mamlaka kwenye mazingira haya maalumu kwa ajili ya kiumbe mtu halisi.


Wamekuja na vitu vingi ili viumbe hawa wapate kibali mbele ya watu wa asili, mfano haki za binadamu kwa kuwa viumbe hawa wanamionekano na miili kama ya watu , ili waonekane na wapate vibali mbele ya mazingira ya macho ya nyama mbele za watu wakasema kuwe na haki za binadamu.


Na mambo mengine eti Hati miliki, kuwa taifa flani haliwezi kuwa na sheria za kutengeneza kitu flani isipo kuwa taifa flani.


Ili kuzibiti kabisa wakaleta sheria za umoja wa mataifa. Ili kutoa azabu wanazo jiskia kwa uhuru kwa mtu anaye kiuka matamanio yao.


Wakaleta Sayansi ili ndio iwe halali na asili ya duniani waifanye halamu, Waka leta dini ili kupindisha asili na mambo mengine mengi katika wakati huu, wakaleta Elimu ili wafundishe wanavyo taka.


Mambo mengi wanayo yafanya viumbe hawa lengo kuu ni kuhakikisha nishati safi ya kiumbe mtu isipae kwenda sehemu ambayo wenyewe hawana kibari napo cha moja kwa moja.


Mambo mengi wanayo shawishi watu wayafanye ni ya kuifanya nishati ya kiumbe mtu baada ya maisha ya mwili iwe nzito kiasi cha kushindwa kupaa.


Katika masomo ya asili roho safi ya kiumbe mtu isipo faa na kupaa huwa na nafasi kadhaa za kuzaliwa tena duniani ili iweze kujifunza tena kupitia mwili mwingine mpya.


Kwahiyo kiumbe mtu ana vita isiyo onekana zidi ya viumbe waasi.

Yaani sehemu ya mtu halisi kujifunza ili afae ipo lakini viumbe waasi kupitia miili ya watu wana fanya vitimbwi.


Lakini siyo kila nishati ya asili ya jamii ya hao waasi ni waasi hapana.

Roho wengine pamoja na kuwa wananguvu na nishati isiyo na kibari cha moja kwa moja kama nishati safi ya kiumbe mtu lakini wamekubali kuwa jinsi walivyo na kulizika na maamuzi ya asili kuu ,yaani asili kumfanya mtu na kumpa upekee huo wakati wao hawana huo upekee.


Itoshe kusema Sayansi ni zidi ya kiumbe mtu na si kwa ajili ya kiumbe mtu.


Na hii ndio maana ya sayansi yao: Ni mfumo wa kufuata taratibu maalum ili kutafuta, kukusanya, na kupanga maarifa kuhusu ulimwengu na vitu vyote vilivyomo kupitia uchunguzi, majaribio, na upimaji wa kiukweli.


Katika uwepo huu unatakiwa kutambua kuwa hakuna dunia peke yake, bali kuna sayari nyingi sana ikiwemo sayari za mfumo wa jua letu.


Kumbuka jua ni nyota, na basi hata nyota zingine zinamiliki sayari zake. Tambua pia kila sayari ni kiumbe hai chenye sifa na tabia fulani za kiasili.


Sayansi ya kisasa haina jipya lolote zaidi ya kufundisha utendaji wa nguo za kiroho. Hivyo, pamoja na mengi yote ya sayansi ya kisasa, bado sayansi hii ya kisasa ni sayansi haba. Haiwezi kuwa na utajiri wa vitu kama ilivyo asili kuu isiyo na mwisho.


Sayansi ya kisasa inaeleza mambo mengi na imegawanya katika sehemu nyingi ikiita jiografia, fizikia, kemia, na baiolojia. Kila sehemu ina mambo yake yenyewe ya kujitegemea ikifanya kazi ya kujadili asili kuu kwa kivuli cha maneno eti ni sayansi, na kujaribu kuaminisha watu habari za sayansi hiyo ili wasiwazie kuhusu asili iliyo asili yao na wakae wasubiri ugunduzi kutoka kwa watu wachache.


Sayansi hii ya kisasa imekaa kama daraja kati ya mtu—wewe wa sasa usiyefikiria kuhusu asili yenyewe. Sayansi ya kisasa imekuwa kama mtafsiri wako wa asili kuu kubwa kuliko chochote yenye sifa isiyoelezeka.


Mfumo wa Atom na Sifa Zake​

Sehemu ya sayansi ya kisasa inaeleza kuhusu atom. Atom hii inajaribu kusimulia kiini cha mambo ya asili kuu kwenye sayansi ya kisasa. Sayansi ya kisasa kwenye sehemu ya kemia inatuambia kuwa atom ina sehemu tatu:


  • Moja ni protons
  • Mbili ni neutrons
  • Na tatu ni electrons

  • Proton ina sifa chanya.
  • Neutron ina sifa ya ganda.
  • Electron ina sifa hasi.

Uhusiano wa vitu hivi vitatu ni kama ifuatavyo:

Proton ni kama sehemu nzuri ya kuvutia sana na kitu chenye sifa isiyoelezeka ambacho ni mvuto wa ajabu usioelezeka; ni sehemu isiyojivuna kwa jinsi ilivyo. Kila kitu kinatamani kuwa karibu na sehemu hiyo.

Sasa, neutron kwa wivu mkubwa inasimama kama ganda aminifu kwa proton kiasi chochote kinachotamani kugusana na proton kisigusane moja kwa moja.

Ni kama ile sehemu inayotenganisha tofali na tofali—yaani ile sementi au udongo unaotenganisha tofali na tofali kwenye ujenzi.

Lakini electron ni kitu kinachojitambua, kinachojisikia vizuri sana kuishi na proton muda wote. Lakini sasa hakiwezi kuungana moja kwa moja, kinabaki kuzunguka proton daima, milele na milele.


Unatakiwa kuzingatia:

Proton (sifa chanya au wema katika maisha haya): Proton ni kama sehemu nzuri ya kuvutia sana. Yaani kitu chenye sifa isiyoelezeka ambacho ni mvuto wa ajabu usioelezeka, sehemu isiyojivuna kwa jinsi ilivyo, na kila kitu kinatamani kuwa karibu na hapo.


Neutron (sifa ya ganda au jeshi la ulinzi): Neutron kwa wivu mkubwa inasimama kama ganda la ulinzi, kiasi kwamba chochote kinachotamani kuungana na proton kisigusane moja kwa moja na kisiharibu kiini hicho. Ni kama ile sehemu inayotenganisha tofali na tofali—sementi au udongo unaotenganisha tofali na tofali kwenye ujenzi wa jengo.


Electron (sifa hasi au ubaya): Electron ni kitu kinachojitambua, kinachojisikia vizuri sana kuishi na proton muda wote, lakini sasa hakiwezi kuungana na proton moja kwa moja, kinabaki kuzunguka proton daima, milele na milele ndio asili yake hiyo.


Mundo huu au sifa hiyo utaikuta kwenye mamlaka za asili katika maisha yake na utendaji wake.

Kwa asili, kuna vitu vitatu hapa unatakiwa kuelewa:

  • Moja ni wema (protons)
  • Mbili jeshi la ulinzi (neutrons)
  • Na tatu ubaya (electrons)

Tambua kuwa atom inayozungumziwa ni kama kichembe kidogo sana ambacho hakiwezi kuonekana na macho ya kawaida, ila kukamilika kwake ni kuwa na vitu hivyo vitatu—yaani protons, neutrons, na electrons ndio atom.


Kitu hata kikiwa kikubwa vipi kinaundwa na vichembechembe hivyo vinavyoitwa atom.


Katika vitu vikubwa vya asili, protons hazina tabia ya kumezana na kuwa proton moja kubwa. Badala yake zinakusanyika pamoja na kutengeneza kituo kikuu kinachoitwa nyukilia.

Kwa kuwa protons zote zina sifa chanya (yaani wema), zikiwa na sifa hiyo moja uzingatie kuwa kwa asili, vitu vyenye asili ya kufanana huwa na tabia ya kukimbiana (na hapa ndio tunapata msemo wa "fahali wawili hawakai zizi moja").


Basi hapo neutrons (jeshi la ulinzi—kama unavyofahamu sifa ya jeshi kuwa na utii mkuu na kuwa halina sifa ya upendeleo zaidi ya kutii kinachohitajika ikiwa ni jeshi jema, au linakuwa ni kama mpatanishi mkuu).


Neutrons hizi huwa zinaingilia katikati yake sasa na kutengeneza nguvu kuu inayozifunga protons zote pamoja ili zisifukuzane.

Hivyo, kitu kikubwa kikiwa na atom nyingi kinatengeneza nyuklia yenye uzito mkubwa zaidi wa wema na ulinzi, huku electrons (ambazo ni nguvu hasi) zikiongezeka kuzunguka nucleus hiyo kwa usawa.


Kila atom ina matabaka au ngazi za nishati zinazozunguka kiini. Matabaka haya katika asili ni ngazi za mawimbi na vipimo vya nishati(Anga).


Tabaka la ndani kabisa lililopo karibu zaidi na kiini (yaani karibu na wema) lina uwezo wa kubeba electrons chache tu ni electrons mbili pekee zikiwa chini ya udhibiti mkali wa kiini.


Matabaka ya nje huzidi kuwa makubwa na yenye nafasi zaidi, huku nje electrons ziko na uhuru mkubwa wa kuzunguka au kuruka kwenda kwenye atom zingine.


Msisimko wa nishati: Atom inapopata masafa ya juu ya nishati, electrons zake za nje zinaruka kwenda kwenye matabaka ya juu zaidi. Kitu chochote kikubwa hata kikiwa na ukubwa gani kinaundwa na mfumo huo wa matabaka.



Sasa tuendelee na elimu inayoweza kumfanya kiumbe mtu aweze kuungana na mazingira na zana za asili yake ili kuwa katika kufaa kwake katika uumbaji.

Ili kujitambua kukalibia na ukamilifu lazima ujadili ulipo sasa na mawasiliano na hali inayo kufanya uwepo , kiumbe mtu yupo duniani , kwenye sayari ya tatu kutoka kwenye mfumo wa jua letu.


Mfumo huu wa jua letu upo kwa kiasili ni muhimu kufahamu miondoko ya mfumo wa jua kwenye kundi la nyota lake.

Lakini pia mfumo wa jua letu sio mfumo pekee wa asili kwa maana hiyo ni tabia ambayo kila nyota kulingana na viwango na kufaa kwake kuwa na sayari kama ilivyo jua letu kiasili, hoja ya msingi ni kiumbe mtu yupo ndani ya mfumo wa jua.


Ndani ya mfumo wa jua kiumbe mtu anapatikana kwenye sayari ya tatu inayoitwa dunia.


Nyota ya jua na mambo yake vina mwendo na namna kwa utaratibu na oda ya asili , hata dunia ndani ya mfumo wa jua ina mwendo na namna kwa utaratibu na oda ya asili ndani ya mfumo wa jua.


Sasa umeelewa habari ya mwendo wa nishati kuwa kwa namna kulingana na mazingira ilipo kwa uwiano maalumu wa asili, ukaelewa habari ya nishati safi kupaa , ukaelewa matabaka kutoka na kufika duniani.


Lakini pia Kuna mlango au sehemu maalumu ya kuingia kwenye anga alipo kiumbe mtu na kutoka nje ya mfumo alipo kiumbe mtu.

Vilevile Sio kila wakati kutoka na kuingia kunawezekana, ndio maana pakawepo na majira na nyakati.



MAJIRA NA NYAKATI.


Dunia haija tulia ipo inakimbia angani kwa kasi kubwa ikilizunguka jua, kama ilivyo kwa gari linalokimbia kwa kasi kubwa -- ambapo ni mtaalamu pekee anayeweza kuruka na kupanda au kushuka akiwa salama bila kuumia--ndio pia roho na nishati za ulimwengu zinavyohitaji uelekeo, mpangilio na maagizo maalum ili kuingia , kutua salama na kufanya kazi duniani.


Dunia inapo kuwa kwenye pembe mbalimbali maalumu za njia yake ya kulizunguka jua inatengeneza madirisha ya nishati.

Kwenye kila dirisha, aina flani ya roho , nguvu za asili na nishati mpya hupokea amri kulingana na kasi na mjongeo wa Dunia.

Nishati zilizopo duniani hazifuati kalenda za karatasi za kileo bali zinatumia kutazama mwezi kama dira ya asili na ujuzi ili kujua wakati halisi dunia ipo na mwendo gani na sehemu gani ili kuandaa utakatifu, kulingana na mitetemo na kutekeleza amri kuu za Asili.


Dunia inachukua muda wa siku 365 ili kukamilisha mzunguko wake wa kulizunguka jua.

Siku hizo ni jumla ya miezi 13 yaani mwezi unapo zunguka dunia mara 13 ndipo mzunguko mmoja wa dunia kulizunguka jua hukamilika--yaani mwaka mmoja, ambapo siku 13 mara siku 28 za mwezi kuzunguka dunia mara moja ni sawa na siku jumla 364.

Inabaki siku moja siku ambayo ni takatifu sana, siku ambapo usiku na mchana huwa sawa, na pia jua huwa lipo utosini mtu anapo simama wima muda wa mchana kamili.

Siku hii ndio siku inayounganisha mzunguko wa zamani na mzunguko mpya bila kuhesabiwa ndani ya mwezi wowote wa Mwaka.

Siku hii ndicho kitovu cha msawazo wa ulimwengu, sumaku ya dunia inakaa kwenye msawazo na lango la ulimwengu linakuwa wazi kabisa, nishati za zamani zinakatika na amri mpya za asili zinaingia Duniani kwa ajili ya mzunguko unaofuata.


HAYA NDIO MAJIRA YA ASILI YA MWAKA KUTOKA SIKU YA MSAWAZO.

Ili uelewe majira haya tafakari unavyo rusha jiwe kwenda juu lina kuwa na kasi inaenda inapungua ikifika juu inasimama kidogo kisha inaanza kushuka.


  • Machipuo na wakati wa Nia , nishati hupanda na kuingia-mwezi wa 1-3
  • Upanuzi, kilele cha mwanga- mwezi wa 4-6
  • Msawazo, tathmini -mwezi wa 7 KATIKATI
  • Mavuno na Shukrani - nishati ya kuvuna na kushuka mwezi wa 8-10
  • Utakaso na Hekima -nishati ya kujiandaa na mzunguko mwingine -mwezi wa 11-13


MACHIPUO NA WAKATI WA NIA , NISHATI HUPANDA NA KUINGIA-MWEZI WA 1-3

Nishati ya dunia na mfumo wa jua hapa inaanza kusukuma vitu kwenda juu. Roho na nia mpya zinatua mwilini na ardhini.

  1. Mwezi wa Kwanza kutoka Siku ya Msawazo.
Kinacho faa hapa pamoja na mengine niKuweka nia, kupanga na kuandika maono ya roho yako kulingana na amri mpya zilizoingia.

  1. Mwezi wa Pili
Hapa nishati hutulia na kuanza kujenga umbo lake. Kinacho faa kufanyika wakati huu ni kuweka ulinzi wa kiroho, kuimarisha mahusiano ya familia na kufanya kazi za nguvu za mwili ili kuunganisha misingi ya maisha. Pamoja na yote ulinzi mzuri kuzunguka kitu ni kuishi vizuri na vinavyo zunguka kitu hicho.


  1. Mwezi wa Tatu
Mwezi huu ni wa mapito na mabadiliko, upepo unakuwa mwingi na miondoko ya hewa inakuwa na nguvu sana. Kinacho faa wakati huu ni kusafiri,kueneza mawazo, na kufanya mawasiliano. Katika mwezi huu siku ya 14 ya mwezi mpevu ni nzuri sana kwa maombi au mila za kuondoa vikwazo vya njiani.


UPANUZI, KILELE CHA MWANGA- MWEZI WA 4-6

Katika kipindi hiki nishati inatanuka na kutoa udhihilirisho wa nje.


  1. Mwezi wa Nne
Nishati huwa na nguvu sana. Hapa nguvu ya mwanga wa jua huzidi kuongezeka. Kinacho faa kufanyika hapa ni kujitanua kikazi, kuweka wazi mipango na kutumia nishati ya jua kuleta matokeo ya haraka kwenye kile unacho kipanda.


  1. Mwezi wa Tano
Mimea na asili hutoa matunda ya kwanza. Kinacho faa wakati huu ni kukuza na kupanua miradi na mahusiano. Mwezi mpevu wa mwezi huu ni mzuri sana kujianika kwenye mwanga wa mwezi ili kupokea maagizo ya akili ya ndani.


  1. Mwezi wa Sita
Mwezi huu nguvu za asili huwa na nguvu sana. Hiki ni kipindi cha maua na nishati thabiti. Kinacho faa wakati huu ni kutumia mitishamba ya dawa, kusaidia jamii kwa baraka ulizo pata, kufanya kazi za ushirikiano.


MSAWAZO, TATHMINI -MWEZI WA 7 KATIKATI

Kwenye mfano wa jiwe la kurusha jiwe ndio hapa jiwe limefika kileleni limeganda kidogo kabla ya kuanza safari ya kurudi chini.

  1. Mwezi wa Saba
Dunia ipo katikati ya safari yake ya kulizunguka jua. Kinacho faa ni kufanya tathmini ya kina ya nafsi na kuachilia kisichofanya kazi, kusamehe, na kusawazisha nguvu za kiume(nguvu za utendaji) na za kike(nguvu za ndani) ndani ya mwili wako.


MAVUNO NA SHUKRANI - NISHATI YA KUVUNA NA KUSHUKA MWEZI WA 8-10

Nishati inaanza kurudi chini kuelekea udongoni


  1. Mwezi wa Nane
Mfumo wa asili unaleta matunda yaliyo pepa. Kinacho faa ni kuvuna matunda ya kazi zako (mali, kifikra, na kiroho).


  1. Mwezi wa Tisa
Utulivu unaanza kuingia kwenye Asili. Kinacho faa ni kutoa sadaka za shukrani kwa asili, kufanya matendo ya hisani, na kusherehekea mafanikio pamoja na jamii.


  1. Mwezi wa Kumi
Mabadiliko ya msimu yanaanza kuingia; Asili inajiandaa kwa mapumziko. Kinacho faa ni kuweka akiba ya nishati, rasilimali, na chakula kwa ajili ya miezi ya utulivu inayofuata.


UTAKASO NA HEKIMA -NISHATI YA KUJIANDAA NA MZUNGUKO MWINGINE -MWEZI WA 11-13

Kipindi cha kurudi ndani(gizani), kipindi cha hekima na Utakaso. Mwanga wa nje unapungua; nishati yote inarudi ndani.

  1. Mwezi wa Kumi na Moja
Kupungua kwa mwangaza wa nje kunalazimisha akili kutazama ndani. Kinacho faa ni kupunguza shuguli za nje, kusoma na kujifunza hekima za kale kwa kina.


  1. Mwezi wa Kumi na Mbili
Mwezi wa roho waliotangulia. Pazia kati ya ulimwengu wa maada na wa roho linakuwa jembamba sana. Kinacho faa ni kuwakumbuka na kuwaenzi waliotangulia (mababu), kuomba hekima kutoka kwa Wazee, na kutakasa mazingira ya nyumba.


  1. Mwezi wa Kumi na Tatu
Mwisho wa mzunguko wa asili na maandalizi ya kurudi kwenye Mwanzo wa Mwaka Mwingine. Kinacho faa ni Utulivu wa hali ya juu hasa kipindi cha siku tatu za mwezi wa kumi na tatu ukiwa gizani. Kuchoma uvumba au mitishamba safi ya asili ili kuondoa athari zote za mwaka na kujiandaa kuingia tena kwenye Mwanzo wa mwaka mwingine. Kumbuka Mwanzo wa mwaka mwingine ni siku ya 365 Ambayo haipo kwenye mwaka wowote.


Hivyo kinacho fanywa na viumbe ni kukupishanisha na majira na wakati wa asili kwa kuwa viumbe hao hawawezi kubadilisha majira na wakati wa asili.


NINI CHA KUFANYA NDANI YA SIKU 28 ZA KILA MWEZI


Siku za MweziAwamu ya Mwezi Nishati InayotawalaTendo Linalofaa
Siku 1-7Mwandamo (Siku za Mwezi Mwandamo) Udongo(Nishati ya dunia)Kupanga, Kutafakari kwa ukimya sehemu tulivu, kuweka mbegu za nia zako
Siku 8 -13Mwezi UnakuwaMaji na Moto(Ukuaji)Kufanya kazi kwa bidii, kujenga,kusukuma mbele mipango
Siku 14Mwezi MpevuNguvu ya KileleniKufanya ibada za Asili, maombi ya shukrani, na kutakasa mwili.
Siku 15 -21Mwezi unapunguaHewaKufundisha wengine, kuwasiliana vizuri, kusafiri, kueneza matunda, kutoa ushauri
Siku 22-28Mwezi wa GizaRohoMazoezi ya ndani, kupumzisha mwili, na kuondoa sumu.

Unapo ishi kulingana na mzunguko huu wa miezi 13 na siku 28, mwili, akili, na nafsi yako vinakaa kwenye wimbi moja la nishati na mwendo halisi wa Mfumo wa Jua na Dunia.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…