Asiepokea mshahara vs viongozi wasiotangaza mali zao hadharani

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,852
Kama mtu kutopokea mshahara imekuwa ni sababu tosha ya kumuhisi vibaya,vipi kuhusu mali wanazomiliki viingozi ambazo hazijulikani kwa umma na wala taarifa hizo hazijathibitishwa?

Kama kweli awamu hii ni ya wazalendo,kwanini viongozi wa serikali hii wasitangaze mali zao hadharani ili umma ujiridhishe kama wanachomiliki kinalingana na kipato chao?

Kwanini taarifa za mali na madeni yao zinazopelekwa kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma(kama sikosei) zinakuwa za siri?

Kama mtu kutopokea mshahara kwa muda mrefu ni kosa.

Je,vipi kuhusu wanaomiliki mabilioni nje ya nchi?

Vipi kuhusu wanaomiliki mali nyingi kuliko vipata vyao?

Mama Kairuki angeamua kutumia fedha zake hizo za mshahara kuwekeza badala ya kuziacha bank,leo hii haya yote yangetokea?

Je, kupitia tukio hili,serikali sasa haio kuwa ni muhimu viongozi wote sasa watangaze mali zao hadharani na kutoa fursa kwa umma kuhoji mali hizo na pia kutoa taarifa ambazo kiongozi anaweza kuwa ameficha kwa lengo la kufanyiwa uchunguzi?

NB:Kama viongozi hawatangazi mali zao hadharani, wanapata wapi uhalali wa kuhoji ni kwanini mtu fulani hapokei mshahara kwa muda mrefu au ni kwanini mtu fulani anamiliki nyumba 17, n.k
 
Magu amechemka sana kumsimamisha kazi Mrs. Kairuki mtu amefanya kazi muda wote huo bila mshahara na ameleta chachu kubwa TIC leo hii anamtumbua ati ni jipu, kweli Nyani huoni kundule.
 
Kwani sababu zilizoelezwa zilikuwa ni mshahara tu? Tuwekee na sababu zingeni ambazo serikali haikutaka kuzisema hadharani!
 
Mtawayawaya sana kipindi hiki! jitanabaishe kwanza uko upande upi! aliyepoteza ulaji au ukawa?
 
Poleni sana. Mtasubiri sana kwa Magu. Zigo lenu la mavi halibebeki tena
 
Kama mtu kutopokea mshahara imekuwa ni sababu tosha ya kumuhisi vibaya,vipi kuhusu mali wanazomiliki viingozi ambazo hazijulikani kwa umma na wala taarifa hizo hazijathibitishwa?

Kama kweli awamu hii ni ya wazalendo,kwanini viongozi wa serikali hii wasitangaze mali zao hadharani ili umma ujiridhishe kama wanachomiliki kinalingana na kipato chao?

Kwanini taarifa za mali na madeni yao zinazopelekwa kwenye tume ya maadili(kama sikosei) zinakuwa za siri?

Kama mtu kutopokea mshahara kwa muda mrefu ni kosa.

Je,vipi kuhusu wanaomiliki mabilioni nje ya nchi?

Vipi kuhusu wanaomiliki mali nyingi kuliko vipata vyao?

Mama Kairuki angeamua kutumia fedha zake hizo za mshahara kuwekeza badala ya kuziacha bank,leo hii haya yote yangetokea?

Je, kupitia tukio hili,serikali sasa haio kuwa ni muhimu viongozi wote sasa watangaze mali zao hadharani na kutoa fursa kwa umma kuhoji mali hizo na pia kutoa taarifa ambazo kiongozi anaweza kuwa ameficha kwa lengo la kufanyiwa uchunguzi?

NB:Kama viongozi hawatangazi mali zao hadharani, wanapata wapi uhalali wa kuhoji ni kwanini mtu fulani hapokei mshahara kwa muda mrefu au ni kwanini mtu fulani anamiliki nyumba 17, n.k
Uzi huuu uwe maalum kwa mazuzu wote wa lumumba
 
unataka mambo yote yafanyike ndani ya nusu mwaka! ndo maana kuna strategic plans!
 
Back
Top Bottom