Ashauri maswali kwa wagombea urais katika kila chama

Ashauri maswali kwa wagombea urais katika kila chama

Mtaka Haki

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Posts
492
Reaction score
149
Waheshimiwa katika baadhi ya makundi ya What'sapp niliona pendekezo moja la Kiongozi wangu mmoja wa dini ambaye Baadaye niliamua kuwasiliana naye kwa UFAFANUZI.
AMETOA USHAURI UFUATAO KWA VYAMA VYA SIASA
VIWE NA FOMU MAALUM YENYE MASWALI MUHIMU KWA WAGOMBEA WOTE. KILA CHAMA KITENGENEZE MASWALI YAKE.
WANANCHI TANGU MWANZO WAONE UMAKINI WA MASWALI YA KILA CHAMA NA JINSI KILIVYOJIRIDHISHA NA MAJIBU YA WAGOMBEA. Haya ni nje na sera, ilani NA mipango ya CHAMA. ( haya ni yale niliyoweza kuandika wakati wa mawasiliano. Kama nitakuwa nimepunguza natumaini atanielewa.

Mfano wa MASWALI
1. Ni kwa nini unagombea nafasi kubwa hii? Unafuata NINI ikulu ambacho huwezi kukifanya ukiwa nje ya Ikulu? Je ikitokea hatukukuteua kisha akateuliwa mwingine tutakayemuona Ana uwezo wa KAZI HII wewe utafanyaje?

2.Utafanya NINI kuinua Uchumi wa nchi yetu

3, Mahusiano yako na majirani zako yakoje?
4. Tafadhali eleza juu ya uadilifu wako na uaminifu wako kwa maisha ya na mahusiano ya NDOA
5. Je umewahi kuwa na tuhuma zozote za rushwa, udanganyifu, ubadhirifu au kuhojiwa juu ya uadilifu wako KWA mambo ya fedha?
6. Endapo watu wangeulizwa kuhusu mke/ mume wako au watoto unadhani wanasema NINI kukuhusu? Tunaomba uweke sahihi Hapa chini kuruhusu uchunguzi wa kina juu ya Maisha yako.

7. Utafanyaje kuondoa udini, ukabila unaonyemelea taifa letu , Je utafanya NINI kuzuia ubaguzi mwingine wowote KATIKA taifa?
8. TAIFA hili hupoteza mamilioni ya Fedha KWA njia mbalimbali umewahi kufanya NINI kuzuia upotevu wa FEDHA ? Utafanya NINI kubana matumizi ya Serikali ? Utafanya NINI kuhakikisha ufisadi unakoma Tanzania?
9. Ni NINI Tafsiri yako ya ucha Mungu? Je wewe waweza kuitwa mcha Mungu?
10. Utatumia mbinu gani kuhakikisha raslimali za taifa hili hazipotei na zinatumika sawa sawa-
11. TUPE MPANGO WAKO WA MIAKA MITANO
12. Tueleze mambo ambayo unadhani una udhaifu kwayo. ( UDHAIFU WAKO NI NINI?).

13. Una mpango wa KUTOA NINI KWA taifa lako. Una hakika kutoka moyoni mwako hakuna unachotafuta kupata Kutokana NA nafasi hiyo? Kama kipo unachotaka kupata tafadhali eleza.
KULINGANA NA MAONI YAKE HAPO TUTAONEKANA TUNAELEWA THAMANI YA KAZI YA URAIS KWAMBA SIO URAHISI.

Majibu ya wagombea yawekwe wazi kabla ya uteuzi.

NAOMBA KUWASILISHA NA NAOMBA NYONGEZA YA MASWALI.
 
Sasa hivi urais inaanza kuonekana kuwa ni kitu cha mchezo. Nadhani seriousness ni muhimu mno.
 
Hayo maswali angeweza kujibu NYERERE tu.wengine wange weza kujibu moja tu na mengine yange wagaragaza.
 
kwa kuwa ccm ni Futuhi watacheza michezo yakuigiza mingi kwenye kila sekta ukanjanja ukanjanja ni jadi ya ccm
 
Back
Top Bottom