GE2025 Asha Hussein Saleh wa CCM ashinda kiti cha Ubunge Fuoni

GE2025 Asha Hussein Saleh wa CCM ashinda kiti cha Ubunge Fuoni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Joined
Dec 9, 2025
Posts
50
Reaction score
84
1767180430201.png


Chama Cha Mapinduzi kimeibuka na ushindi katika uchaguzi mdogo wa mbunge Fuoni Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.

Matokeo ya uchaguzi huo yalitangazwa usiku wa jana Desemba 30, 2025 katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Wilaya ya Magharibi B, Msimamizi wa uchaguzi wa wilaya hiyo, Miraji Mwadini Haji alimtangaza Asha Hussein Saleh kuibuka mshindi.

Katika matokeo hayo, Asha amepata kura 9,861 akifuatiwa na mgombea wa ACT Wazalendo, Khamis Shaib Mussa ambaye amapeta kura 503 ya kura zote zilizopigwa.

Kwa mujibu wa msimamizi huyo, waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 14,130, waliopiga kura ni 11,024, kura halali 10,930 na zilizoharibika ni 94.

"Kwa mantiki hiyo namtangaza Asha Hussein Saleh wa CCM kuwa mshindi wa jimbo la Fuoni," alisema Miraji.

Soma pia PostGE2025 - Wananchi Zanzibar wajitokeza uchaguzi mdogo Fuoni
 
Znz mnawakilishi na wabunge wengi unnecessary,yaani wapiga kura 14K...MZAHA HUU!
 
Hakuna uchaguzi nchi hii chini ya serikali ya CCM Wala haujawahi kuwepo ni kupeana tu madaraka na kuiba pesa za umma.
 
Back
Top Bottom