Duble Chris
JF-Expert Member
- May 28, 2011
- 3,481
- 564
Tulipo anzisha mfumo wa vyama vingi tulitegemea kuona vyama vipya vinakuja na mfumo,sera tofauti na CCM lakini sasa vyama vingi vina mfumo na muundo sawa na CCM.
Wengi wanafiri katiba mpya ikianza kutumika tu basi upinzani utashinda
Wengi wanalalamika kuwa tume ya Uchaguzi si huru ukiwauliza si huru kivipi hawasemi wanashindwa kueleza
Hastahili hata hicho kiinua mgongo. Huyu alitakiwa apelekwe mahakamani kwa ufisadi aliotufanyia akafie jela. Tazama tunavyogharimia wezi wengine kama Lowasa eti waziri mkuu mstaafu wakati tunashindwa hata kutoa mikopo ya elimu kwa wanavyuo.Jamani nyie mlitegemea aseme nini !! kula yake na wastaafu wenzake wanaidhinishiwa na serikali hii hii na wamekuwa mzigo mkubwa kwa taifa letu. Ni bora wangepewa kiinua mgono tukaachana nao leo hii wasingekuwa na mawazo mgando kiasi hiki.
Dadavua mkuu maana hata BWM hakueleza kwa undani zaidi tusaidie kutujuza...Ameongea ukweli sana katika haya...
Kwa mwendo unavyoenda hii katiba inavyoundwa siielewielewi vileanajua kuwa katiba ikibadilishwa kama wanavyotaka wananchi basi yeye atakuwa ni victim namba moja
...Ameongea ukweli sana katika haya...
Kwa mwendo unavyoenda hii katiba inavyoundwa siielewielewi vile
Pia ndiye aliyeweka ripoti ya Mzee Paul Sozigwa kapuni kama alivyosema EL hayo yote yanayofanyika sasa yasingekuwepo kama ile ripoti ingetumika.Huyu mzee kwanza akae kimya maana hatujasahau alivofanya biashara akiwa ikulu kinyume na katiba!! halafu bila aibu ansema watu hawawezi kueleza kwa nini tume sio huru?? Alimuuliza nani akashindwa simply tume inayoteuliwa na rais wa jamhuri ambaye pia ni mwenyeketi wa CCM na mgombea urais kwenye uchaguzi utakaosimamiwa na tume aliyoteua, tume hiyo itakuwaje huru?
Katiba inasema matokeo ya urais yakishatangazwa na tume hakuna mahali au taasisi yoyote inayoweza kuyahoji hata mahakama, tume ipo juu ya mahakama?? huko nako ni kuvunja katiba maana katiba hiyohiyo inasema mahakama ndicho chombo pekee cha kusimamia na kutoa haki!!
Mzee anatetea katiba mbovu na CCM maana anajua siku ikiondoka madarakani lazima afikishwe mahakamani kujibu tuhuma za ANBEM, EPA, RADA, KIWIRA n.k kweli sasa amekuwa mvivu wa kufikiri!!
Siamini matusi yote hayo alfajiri ya mungu ! Mzee ameamka vibaya leo.