Asanteni wakazi wa Gairo kwa kunitia nguvu

Dec 11, 2018
7
5
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe DC Siriel Mchembe ameendelea kutiwa nguvu na wakazi wa Gairo kwa kuitikia wito na kujitokeza kwenye huduma mbali mbali za kijamii wilayani humo.

Zaidi ya watu 400 walijitokeza katika uchimbaji wa msingi wa jengo la Dawa katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo.

Zaidi ya watu 315 walijitokeza kusawazisha eneo la uwanja katika hatua za awali za ujenzi, Jambo ambalo liliokoa zaidi ya pesa za kitanzania mil 65

Ushirikiano mzuri unaofanywa na watumishi wa Halmashauri wakiongozwa na DED, DAS na watumishi pamoja na wananchi umemtia nguvu Mkuu wa Wilaya kuendelea kuwapambania wakazi wa Gairo.

Pamoja na kuweza kuwahamasisha wananchi kuungana, Mhe Siriel amefanikiwa kurejesha Pesa za TASAF zilizokatwa kimakosa kutoka Kaya Masikini wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya pia amefanikiwa kuagiza na kusimamia mchakato wa kurejesha Pesa za Michango ya wananchi zilizotumika kutengeneza matofali yaliyobainika kuwa chini ya kiwango. Pesa hizo Mali ya wananchi zimerejeshwa kwenye Serikali ya Kijiji.

Kwa mshikamano huu, Tutegemee siku za usoni kuiona Gairo yenye mafanikio makubwa zaidi katika Mkoa wa Morogoro.
IMG_20181211_232212_737.jpeg
47488936_720125328362065_8048358685061152768_n.jpeg
47399573_720135405027724_1408985436159737856_n.jpeg
 
Mleta mada ndiye mkuu wa wilaya mwenyewe,ila siyo mbaya kujipa promotion.
Kwa upande mwingine tuwapongeze wanachi kwa kuitikia mwito wa maendeleo.
 
Back
Top Bottom