Asanteni wabunge wetu kwa umbumbu wa kuisifia NHC na kusahau kuwa ndo chanzo cha foleni Dar

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
66
Wakati wa bajeti ya Magufuli wabunge walilalamikia foleni za Dar. Nikajua wamejipanga vizuri
kumuuliza Mama Mtambuka juu ya NHC na ujenzi wa maghorofa POSTA bila nyumba hizo kuwa
na mahegesho kabisa/ya kutosha idadi ya ghorofa zinazobebwa juu.

Mf. Maeneo ya Mosque, Bustani-India St, Aggrey na kitumbini leo huwezi kupata parking masaa
ya kazi na bado majengo yanajengwa kama uyoga na hayana parking au parking hazitoshi kabisa.

Hata ukiwa na barabara zinapita mbinguni, kama hakuna eneo la kupark magari bado foleni
zitakuwa pale pale.

Je, Mama Mtambuka anatuambia nini sisi wakazi wa Dar juu ya mipango miji (POSTA)?
 
Ijulikane kuwa makusanyo makubwa ya NHC lazima yanatokana na Kodi kubwa sana
(ingawa wajenzi wa nyumba hizo si wao ila wabia wao wenye hisa 75%). Pia kodi hiyo imo VAT.
 
Kila nikiangalia maghorofa makubwa na marefu yanayojengwa ktkt ya jiji la Dsm huwa najiuliza kama wamiliki wa hayo majengo na mamlaka husika wanawaza mbele ya pua zao! Barabara ni nyembamba sana,na hakuna namna ya kuzipanua tena. Mji umeanza kuwa giza na ujenzi usio na mpangilio! Haishangazi kwamba kampuni kubwa zimeondoa ofisi zao kwenda nje ya mji. Muda simrefu haya majengo marefu ktkt ya jiji yatakua makazi ya popo!
 
Lakini huoni kama imesaidia kidogo kupunguza msongamano/foleni imagine kama wahindi wote wanaoishi Posta na Upanga tungekuwa tunapanga nao foleni kutokea Tegeta kuja mjini kwenye foleni asubuhi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom