Asanteni kwa kuja,ila cha moto mmekiona

mkolaj

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
3,020
1,087
"ASANTENI KWA KUJA..... ILA CHA MOTO
TUMEKIONA....."
MAMBO 10 NILIYOYAGUNDUA BAADA YA MECHI
YA YANGA UGENINI:
1. HANS VAN DEL PLUJIM
kiukweli hapo zamani sikuwahi kumkubali huyu
mzee hata kidogo kutokana na "unazi" niliokua
nao kipindi hicho nadhani,ila kwa jana
kani"prove" wrong na mawazo yangu "mgando",
kuanzaia kikosi cha jana jinsi alivyokipanga na ile
"Formation" aiseee kiukweli unastahili heshima
mzee ni vijana wako tu wachache jana
wamekuangasha... tumezoea mara nyingi timu
zetu zikienda "ugenini" huwa tuna-defense tu na
"vishambulizi" vichache sana vya kushtukiza,laki
ni jana "YANGA" kashambulia muda mwingi na
mpira pia kaucheza japo haukuwa wa kiwango
kikubwa sana. # ShikamoBABU.
2. KAMUSOKO,DONALD NGOMA,BOSSOU,TA
MBWE na HARUNA:
Kiukweli jana mmeonyesha nini umuhimu wa
kuwa na "Maproo" wengi katika ligi yetu ya
kibongo,bila ya uwepo wenu jana sidhani kama
"YANGA" wangepata jeuri ile ya "ku-process"
mpira atleast kwa muda hat wa dakika 3 hadi
4,lakini jana mpira ulipokua unakuja kwa
"HARUNA" lazima kwanza atulize kisha aangalie
mtu sahihi wa kumpasia,hali hiyo pia ilionekana
kwa "NGOMA" na "KAMUSOKO" ila kwa
"TAMBWE" kidogo jana katuangusha nahisi
pengine ni kutokana na kukabwa sna,big kwa
"DONALD" bonge la bao lile mwanangu.
3. JUHUDI BINAFSI ZA JUMA ABDUL:
Huyu "Mshikaji" majuzijuzi tu hapa niliwaambia
anaujua mpira kweli kweli ila tatizo lake moja tu..
HASIRA na "BANGE" tu ndo vinamsumbua,mfano
jana kaupiga mwingi mno,kateneneza "Bao" safi
sana kwa "NGOMA",alichokifanya mbele ya yule
beki wa AL AHLY ni juhudi binafsi tu,yaani huku
kwetu tunaita "Kujiongeza" mshikaji alijiongeza
alipoona hawezi kumwaga maji (kupiga krosi) ya
moja kwa moja akaamua amfinye yule beki na
kumwaga "kakrosi" kadogo tu kalikotua moja kwa
moja kichwani kwa "NGOMA".. kwa tukio hili la
jana mshikaji wangu JUMA hongera sana,hiyo
ndio type ya beki namba mbili wa kisasa.
4. MBINU ZA ZIADA ZA MWARABU:
Ujue kiukweli "Mwarabu" alizidiwa "maarifa"
kidogo na YANGA hasa ule muda wa kipindi cha
pili baada ya kuingia lile goli,wakaanza kutafuta
goli kwa nguvu,walipoona hawafanikiwi wakaanza
kutumia mbinu za "ziada" kuwaaharibu YANGA
"kisaikolojia" na hili walifanikiwa kwa asilimia
kubwa tu,hasa lile tukio la "fujo" lililosababisha
"NGOMA" kupata kadi ya njano,lile tukio sio la
bahati mbaya aisee mkae mkijua lile tukio ni
sehemu ya mipango yao wakishaonaga mambo
magumu wanakuja na style ile,maara huyu
kakupiga kibao,mara huyu kakutemea mate,mara
huyu kakutia kidole yaani wanakufanyia visa vya
kila aina ili mradi tu "upaniki" na kutoka kwenye
mchezo,hili lilifanikiwa kwani baada ya YANGA
kudili na soka sasa wakaanza kudili na fujo za
mwarabu matokeo yake wakampa nafasi ya
kujipanga upya kwa mashambulizi na muda
mchache uliofatia wakapata goli. (how to be a
professional)
5. KILIO CHA OSCAR JOSHUA....
Hivi kwanza unajua kwa nini "Oscar" alilia sna
kwa uchungu baada ya kuingia kwa lile goli???
jibu ni simpo tu,jamaa alicheza vyema sana hii
game na sidhani kama kuna mtu alitegemea
hilo... wengi waliamni huu ndo ungekuwa
uchochoro wa "mwarabu" lakini UBAVU na
UZOEFU vimembeba sana OSCAR jana,na mechi
kama hizi uzoefu ni bora zaidi kipaji,namaanisha
hivi HAJI MWINYI ana kipaji cha hali ya juu
kumzidi OSCAR ila hana uzoefu wa game kubwa
kama hizi kama unabisha hili juzi juzi tu tuliliona
pale TANZANIA ilipokula WIKI kule ALGERIA,haji
hakuwa mzoefu na jama mashambulizi mengi
waliyatumia upande wake na walifanikiwa
hilo,kwa hiyo jana kwa oscar alistahili kulia kwa
kweli hata ningekua mimi ningemwaga chozi zile
dakika zinauma sana bora ufungwe hata
mwanzoni kiukweli.
6. REFA:
Kwa mara ya kwanza tangu nianze kuangalia
mechi za "Waarabu' wakiwa kwao namuona
"REFA" yupo "FAIR" kabisa na maamuzi yake
uwanjani,kama kuna shabiki wa YANGA atadiliki
kusema "Waarabu" wamebebwa nadhani huyo
atakua kaangalia mpira kupitia "STAR TV" au
kwenye simu ya mkononi,jana bhana kiukweli bin
haki mwamuzi alikua yupo fair kwa maamuzi ya
pande zote mbili.
7. CAPTEEEEIIIIIIN NADIRI:
Jamaa amezihirisha badi tunamuhitaji sana tu
kwenye soka letu kibongobongo,jana ka-perfom
vizuri tu,kautendea haki unahodha wake,naamini
hata kule ALGERIA kwenye zile 7 kama
angekuwepo basi zingepungua idadi,sio kwamba
anacheza peke yake kwenye timu hapana bali
anajua kuhamasisha wenzie ni mzoefu wa
michuano ka ile pia,so jana tumeona alivyojitahidi
sana kuhamasisha wenzie nini cha kufanya...
# MKWASA kama unanisikia huyu jamaa mtake
radhi bado tunamuhitaji National Team aiseeeee.
8. WENGI WALISAHAU KUWA AL AHLY NI TIMU
YA AINA GANI:
YANGA jana imekutana na timu bora na kubwa
barani AFRKA,time yenye wadhamini zaidi ya
10,ina kikombe cha kila aina,ina uwanja wake wa
mazoezi,ina vitega uchumi vya kuiongezea
mapato,ina wachezaji bora na kocha bora,pasipo
sahau ina "sapoti" kubwa nyuma ya mashabiki
wake,so kuitoa timu kama hii yatakiwa ujipange
kweli kweli na ujue mpira kweli kweli,bado
TANZANIA tuna safari ndefu ya kufikia mafanikio
makubwa katika hii michuano na hilo litachukua
muda mrefu sana,kila siku tutakuwa tunafurahia
kupanda ndege na kusindikiza wenzetu
tu,mipango madhubuti inahitajika,viongozi
wanaojua soka wanahitajika pale TFF na hizi
timu za SIMBA na YANGA ifike mahala
ziruhusiwe tu kuendeshwa na "boss" mmoja tu
naamini,tutapata wachezaji bora wa kupambana
huko siku za usoni.
9. TUNAHITAJI WALIMU WA "SAIKOLOJIA"
KWENYE TIMU:
Kwa "YONDANI" Nahisi jana bado ile hali ya
"ubaridi" ilikua inamsumbua na bado
hajachanganya kwenda sawa na wenzie,maana
kwa style ya lile goli lililofungwa mpigaji kichwa
akitokea nyuma upande wake ilidhihirisha
hili,mchezaji anatakiwa muda wote awe
mchezoni aisee..na ndio maana timu zetu
zinatakiwa kuwa na watu maalumu wa
"saikolojia" mfano jana uliona yule namba 10
mgongoni wa "waarabu" kabla hajaingia
alichokua anafanyiwa na yule kocha wao wa
viungo???alikua anamuinua kila dakika
anamuambia apashe misuli,anama ushauri wa
hapa na pale,ile ndio inatakiwa hata kwenye
vilabu vyetu..sasa kumbuka kabla ya "kelvin"
kuingia nani aliketi ae chini na kumkumbusha
wajibu wake??maana naamini wajibu wa
kuingizwa kwa kelvin jana ni kwenda "kukaba" tu
ila walau matokeo yabakie vile yaani 1-1 ile
waende kwenye hatua inayofata lakini kilichofatia
mtu aliyetumwa hiyo kazi ya kukaba ndio "kanya"
yaani boko limetokea kwake.
10. GAME ZIISHIE NYUMBANI/ASANTENI KWA
KUJA:
Kuna umuhimu wa kumaliza "MECHI"
nyumbani,hivi kwa mfano jana YANGA ile game
ya kwanza yaani home wangeshinda zaidi ya goli
2 unadhani nini kingetokea na ile "spirit"
waliyokua nayo jana????jamani sio kuwa jana eti
mwarabu kafanya makusudi zile 2-1,hapana jana
alishikwa kimbinu kweli kweli na ndio maana hao
wenyewe mpaka muda huu wanawaambia yanga
kuwa "ASANTENI KWA KUJA...ILA CHA MOTO
TUMEKIONA..." ni dhahiri kama tutakua
tunamaliza game zetu nyumbani hizi za igenini
zitakua ni kumalizia tu vita...somo kwa vilabu
vyetu vyote nchini.
MWISHO KABISA:
YANGA hongereni kwa kupambana kiume ila kuna
mtu hapa ananiambia eti afadhali mmetoka ili
tujue kuwa TANZANIA kisoka bado sana hasa
nyanja za kimataifa..anadai kuwa laiti kama
tungepita jana..leo tungejiona tushamaliza kila
kitu.
">.....MUNGU IBARIKI TANZANIA... MUNGU
IBARIKI YANGA IRUDI SALAMA KUMALIZIA
# VIPORO VYAKE VYA # VPL ..."
 
Manenoo mengiii...!

Niambie, Yanga jana walipiga "SHOOTS ON TARGET" ngapi na Al Ahly walipiga ngapi?
 
Watanzania kama kawaida yetu "tumetolewa kwa mbinde sana"
 
tz_1000shs_mkapa_2.jpg
safi sana, nakukubalia namba moja hadi 4 na namba sita kuonesha kwamba nimesoma kwa makini muda tu hauniruhusu kukakavua zaidi
 
Back
Top Bottom