Asante waziri wangu wa fedha, Zitto Kabwe

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,193
1,434
Wafanyakazi wa serikali tulilipwa mishahara yetu ya April,2011 tarehe 7 May,2011. Hii haikuwa kutokea katika miongo ya hivi karibuni. Chama dume (CDM) kikiwa kinaunguruma nyanda za juu kusini, HE Zitto Kabwe aliichana LIVE serikali chovu ya CCM kwamba imefulia na inakopa benki za ndani ili kulipa mishahara. Waziri wao wa fedha (Mkullo) akakiri kwamba kweli wanakopa benki za ndani kulipa mishahara lakini kuna chenji inabaki. katika hali ya kujishaua, mshahara wa mwezi May,2011 watumishi hao wamelipwa jana tarehe 18 May,2011. Hii nayo haijawahi kutokea.

Hii inanikumbusha Rais fulani ambaye katika kukanusha habari kwamba afya yake ni dhoofu, aliwaarika waandishi wa habari nyumbani kwake na kuwathibitishia kwamba yupo fit akataka kuogelea...weee kama si uhodari wa walinzi wake,angekufa. Sasa wanajifanya kujibu mapigo ya CDM kwa kuficha maradhi hakika mauti yao haiko mbali.

Asante sana HE Zitto Kabwe na CDM...wapelekeni puta hivyo hivyo!!
 
Vizuri ila usishangilie sana tumia vizuri huo mshahara maana serikali yetu haiaminiki unaweza kuta mshahara wa mwezi wa sita ukapata trh 18 july.
 
kweli kabisa tumpe pongezi zake Zitto lakini tujiangalie tule kwa machale tusije ishiwa na mshahara mwingine uje kati ya July.
 
kheeeeee....mbona mkulo alikanusha?hivi hii nchi ina rais kweli aua ni mautumbo ya bata haya jamani!!!! halafu yuko bize kufanya mavikao ikulu kazi kutafuna makaranga na kashata tu wakati wa vikao...yaani....
 
wanawalipa wafanyakazi kwasababu watu wameongea hali za wanafunzi elimu juu ni mbaya kuliko boom mpaka sasa.
 
wanawalipa wafanyakazi kwasababu watu wameongea hali za wanafunzi elimu juu ni mbaya kuliko boom mpaka sasa.
Kama wamelala wasahau kabisa. Off course serikali imefilisika kabisa ila this time watakuwa wamekopa benki mapema
 
Back
Top Bottom