Kiukweli hata mi namkubali huyu dogo Ngeleja. Jamaa ana uwezo wa kazi balaa,we fikiria lile liwizara ambalo ni kama wizara mbili kamili alikuwa analiendesha na Naibu Moja tu,pia Katibu Mkuu alikuwa 1 tu. Tangu alipotoka ilibidi Muhongo akabidhiwe Naibu Mawaziri wawili, Katibu Mkuu naye akaongezewa Naibu Katibu Mkuu.
Ngeleja alikabidhiwa wizara Feb 2008,ingawa Kabla ya hapo alikuwa Naibu kuanzia January 2007.
Kumbukeni Ngeleja alikabidhiwa wizara ikiwa katika hali mbaya sana. Kwenye sekta ya nishati,Tanesco ndo ilikuwa imetoka kuondolewa kwenye orodha ya mashirika yaliyokuwa yamekusudiwa kubinafsishwa tangu mwaka 1997. Hii maana yake ni kwamba tangu Mwaka 1997 Serikali au sekta binafsi hazikufanya uwekezaji wowote wa maana. Miundombinu ya Tanesco iliishazidiwa sana ndiyo maana mgawo wa umeme ulikuwa hauepukiki kila maji yalipopungua kwenye dams au mitambo ilipoharibika hata Kosovo tu.
So Ngeleja alipoingia ndo kaanza kurekebisha mambo ikiwa ni pamoja sera,Sheria,miongozo na kuibua na kuanza kutekeleza miradi mbalimbali Kama mlivyoiainisha humu.
Kwa hivyo kiukweli kwa kigezo cha legacy hakuna anayeweza kulingana Na Ngeleja Kati ya wanaotajwa kugombea urais awe from CCM au UKAWA,anayebisha alete hapa sifa Na utetezi wa hao wengine.
Sisi kama wachambuzi tusiendekeze mapenzi binafsi kwenye issue ya urais. Moja ya sifa kwa nafasi ya urais ni legacy,cyo porojo tu eti za maono ya mbele, hiyo halitoshi,lazima kila mgombea atudhihirishie legacy yake so far.
Wote tunakumbuka wakati anaondolewa uwaziri Mei 2012, Ngeleja aliishafanikisha kudhibiti mgawo wa umeme tangu Nov 2011 kupitia ule Mpango Maalum wa Dharura wa kudhibiti mgawo wa umeme ulioidhinishwa na Bunge mwezi Agosti,2011 kwenye bajeti ya Mwaka 2011/12. So mgawo wa umeme ulikuwa umedhibitiwa miezi 7 Kabla Ngeleja hajaondolewa. Mpango huo ulioanzishwa Na Ngeleja bado unaendelea hadi Leo.
Pia ni muhimu kujikumbusha kwamba tangu Ngeleja aondoke Serikali imekuwa ruzuku kwa Tanesco kissing cha shilingi 2.4bn a day kwa ajili ya kugharamia ununuzi wa mafuta ya mitambo ya kikoi. Ruzuku hii ndo iliyochangia national budget deficit for the last 2 yrs!
Lakini pia wakati Ngeleja anaondolewa hasara kwa Tanesco ilikuwa just shs 43bn,leo ni zaidi ya shilingi bn 467.
Nakadhalika n.k