Marry Diana
JF-Expert Member
- May 5, 2025
- 970
- 2,360
Nakumbuka mwakajuzi nilitoka na kwenda karume kutafuta nguo za mtumba hasa zile zinazobana kama taiti pamoja na vijisketi vifupi.
Hii ilikuwa ni miezi kama mitano baada ya mimi kuachwa na mume wangu akiwa amechukia baada ya mtoto wetu wa Kwanza kufariki siku tatu tu tangu azaliw.mume wangu alichukia mno akihusisha ushirikina,kumbe ni mtoto alizaliwa njiti.
Sasa baada ya miezi mitano nikaamua mm na marafiki zang tukapanga kufanya kazi kwenye mabaa,wenzetu wawili walikuwa wazoefu halafu Mimi na mwenzangu tulikuwa hatujawahi kufanya hiyo kazi,basi tukapanga kwenda karume kutafuta mitumba baada ya wenzetu kutwambia kaz ya ubaamed ina nguo zake ili kuvutia wateja.licha ya kuwaambia sina pesa nina elfu 20 tu, waliniambia hiyo pesa ni nyingi naweza kupata vitu vizuri.
Tukiwa karume mm nilichagua taiti fulani ndefu na nzuri yenye rangi ya pink,bei ilikuwa elfu 6 lakini muzaji akasema mpaka 4000 naweza kuchukua,nikasogea nyuma ya mapazia yaliyokuwa yananing'inia pale, nikajaribu,ikanitoa kiasi cha muzaji kunisifia huku wenzangu wakitabasamu,tulinunua nguo nyingine kisha tukarudi nyumbani . wenzangu walinisaidia Sana kwamba Nina Sura ya mauzo hivyo nikiwa kule nitapiga pesa toka Kwa masponsa mbalimbali,tamaa ikaniingia nikawa Nina hamu na hao watu.kwanza wenzangu walikuwa Wana smartfoni ni Mimi tu nilikuwa natumia simu ndogo,huku zile Tecno zao zikinitoka mate
Shida moja ilikuwa ni wazazi hasa mama ninayekaa naye ,je angekubali.nikawaza nikasema nitafosi tu,bas kesho nikizifua zile nguo na kisha siku ya kwenda kazini ikafika,
Nilivaa ile tait ,juu nilikuwa na tishet nyeus niliyoletewa na wenzangu ikiwa na jina la bar napoenda kufanya kaz ,chini nikavaa raba nyeus maana niliambiwa kule natakiwa kuwa mwepes,hivo kiatu rafiki ni raba,
Akiiii nilipendeza Sana ,wakati natoka mtaani kwetu na kuingia barabara kubwa huku nikitembea Kwa madaha na kuenjoi vifijo na usumbufu wa watu wa vijiweni kuna boda ilifunga breki za ghafla miguuni kwangu kugeuka alikuwa ni mama yangu akiwa anatoka kwenye zahanati moja alikokuwa anafanya kazi,kumbe alinichora tangu nikiwa nyumbani akawa ananifuata nyumanyuma alivoona nitapotea akachukua boda.
Alishuka na kuuliza Maria unaenda wapi (huku akinigeuza na kusoma maandishi kwenye fulana niliyovaa)
Baada ya hapo hakusema neno akashika fulana akaichana, nikabaki na bra tu yaani kama karatas,kisha akaanz kunipiga Ile siku sitasahau baadhi ya wapita njia walinisaidia na kunitoa mikonon mwake nikapandishwa kwenye boda na kurudi nyumban nikiwa nimevimba ,Ile nakaa chini mama naye akafika na kufunga geti akaanza kunipiga , kiukweli kama si Baba mzazi kuingilia Kati sijui ningekuwaje .wiki tatu nilikuwa ndani siwezi kutembea.
Lakini nashukuru kwani ndoto za ubaamed ziliishia pale, hakika Mungu ni mwema siku zote