Margwe
JF-Expert Member
- Apr 30, 2008
- 255
- 48
Mbowe: Wananchi lazima wanufaike na Mlima Knjaro
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema Mlima Kilimanjaro hauna budi kuwaletea manufaa wananchi wa mkoa wa Kilimanajro ambao wanauzunguka mlima huo badala ya mapato yanayopatikana kuwanufaisha watu wengine.
Mbowe alisema Mlima Kilimanjaro umekuwa na mapato makubwa ambapo kwa mwaka 2010/11 zilipatikana sh bilioni 88, huku kukiwa hakuna kiasi chochote kile kilichorejeshwa kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanajaro.
Mbowe alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea udiwani wa kata ya Nanjara Rea, jimbo la Rombo, na kumnadi mgombe udiwani kupitia CHADEMA, Frank Salakana, ambapo maelfu ya wananchi walijitokeza.
Kampeni hizo zilihudhuriwa na wabunge mbalimbali akiwemo Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, Suzan Lyimo, Lucy Owenya, Meya wa Manispaa ya Moshi Japhary Michael, madiwani na mkurugenzi wa masuala ya Bunge wa CHADEMA, John Mrema.
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema wananchi wanaozunguka mlima huo wana haki ya kufaidi matunda yanayotokana na mlima huo, kwani hata mlima huo ukiwaka moto wananchi hao wanakuwa wa kwanza kuzima.
Serikali ya CCM haina huruma; mlima huo unazunguka maeneo kama Marangu, Mwika, Kilema, Rombo na Machame ambayo yako wilaya ya Hai na Siha. Ukiwauliza wananchi wa maeneo haya kama kuna fedha zozote zilikwishawahi kurudishwa kwa ajili ya kuwasaidia, watakuambia hakuna, zimeenda Dar es Salaam kuliwa na mafisadi, alisema Mbowe.
Alisema chama hicho tayari kilikwishakutana wabunge wa mkoa wa Kilimanajaro kujadili jinsi ya kuwatetea wananchi wanaozunguka mlima huo huku akisema hata kama ikishindikana wananchi wakiipa nchi CHADEMA lazima wananchi wanaozunguka mlima huo wanufaike.
Katika hatua nyingine, Mbowe alisema chama hicho kimejipanga kuhakikisha kuwa kati ya kata 29 ambazo zina kinyanganyiro cha udiwani lazima kata 20 ziende CHADEMA, Nanjararea ikiwa mojawapo.
Alisema safari ya kudai ukombozi wa nchi ina changamoto nyingi ambazo chama hicho kimekuwa kikikumbana nazo kwa kupambana na dola, polisi ambao wamekuwa wakiwapiga mabomu na risasi huku hata wengine wakipoteza maisha.
Hata hivyo Mbowe alikemea vikali kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi kuwakamata vijana ambao walikuwa waje kwenye mkutano huo wa CHADEMA kwa kuwafungulia mashtaka ya kudai rushwa na kusema polisi wako kwa ajili ya kulinda usalama wa raia wasiruhusu kutumika na CCM.
Kwa upande wake, mgombea udiwani, Frank Salakana, aliwaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua ili kuwawakilisha vema kwenye vikao mbalimbali vinavyohusu maendeleo ya wananchi pamoja na kushirikiana na mbunge wa jimbo hilo kuwaletea maendeleo.
Sikubaliani na Mbowe kwa hili:-
1. Hakuna watu ambao ni beneficiaries kama watu wa kilimanjaro wa utalii kwa ujumla Tanzania achilia mbali mlima klm. Akiwemo yeye mwenyewe Mbowe. Ni ukanda wa Kaskazini zaidi ambapo uwekezaji wa utalii upo kwenye mikono ya watz ukifananisha na maeneo mengine. This is too obvious to be proved.
2. Multiplier economic effect ya Mlima kilimanjaro na hasa value chain is far higher than any other tourism resource in Tz, labda kama Mbowe anatumia kama political tool kuwin audience yake thats something else. Soma study ya Tracing Tourism Dollar.
Tracing the tourism dollar in Northern Tanzania - ODI Project - Our work - Overseas Development Institute (ODI)
2.Mbowe anatakiwa aelewa kwamba Mlima Kilimanjaro ni urithi wa dunia na Tanzania tumebahatika kuwa custodians tu for the coming generations and for our current use. Na that is National icon.
This is too low for him, and can be easily mis-interpreted at his detriment. It will be rational if he will be addressing his public while he is well informed.