VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Wakati mijadala na mipango ya 'kumkata na kumpeleka' Lowassa CHADEMA/UKAWA ikianza kusukwa chamani, nilikuwa mmoja wa waliopinga. Niliamini kuwa wapinzani wangetushtukia mbinu yetu ya 'kumpeleka' Lowassa huko kwa 'mission maalum'. Nikaelezwa sana, sikufanikiwa kuelewa kwa wakati huo. Sasa naelewa.
Lowassa, tangu ahamie CHADEMA/UKAWA amekuwa msaada mkubwa kwa CCM. Anafanya kazi kubwa na ya kutukuka akiwa huko kwa ajili ya chama chetu cha CCM. Anastahili tuzo isiyo na gumzo. Lowassa 'amewanyamazisha' CHADEMA na hoja yao ya ufisadi.
Kama hiyo haitoshi, Lowassa amewadhibiti na kuwaaminisha CHADEMA kuwa CHADEMA yapaswa kuwa chama cha kisiasa na kiachane na harakati-fujofujo za kuhojihoji na kukosoakosoa. Amewafanya CHADEMA wawe wapole. Ni jambo kubwa.
Nimeamini kuwa ni kweli MCHAWI MPE MTOTO WAKO AKULELEE. Lowassa ndiye aliyekuwa 'target' ya CHADEMA na UKAWA kwa ujumla. Ndiye sasa wanaye huko. Wapo wanaougulia ndani kwa ndani;wako wanaona aibu wakiwa naye na wapo waliokubali matokeo. CCM ni wabunifu na ni wanasiasa wakutusifu.
Asante Lowassa, chama kipo nawe.
Mwafaaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam