Asante Dkt. Msonde umeiacha NECTA pahala salama

Asante Dkt. Msonde umeiacha NECTA pahala salama

dega

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2012
Posts
3,171
Reaction score
3,086
Huyu mwamba ni Jemedari na Mzalendo namba moja anaumwa na maendeleo ya kielimu ya Nchi hii na anaechukia ubabaishaji na shortcuts.

NECTA aliyoipokea Dr Msonde toka Kwa mtangulizi wake Pro Ndalichako sio hii ambayo ameiacha juzi baada kupata uteuzi mwengine.

Ameiacha NECTA ikiwa NI miongoni mwa taasisi makini zaidi hapa Tanzania na zinazofanya kazi Kwa uweledi uliotikuka. Yote haya kutokana na upambanaji mahir WA kiongozi huyu miongoni MWA mafanikio ya NECTA chini ya Msonde ni haya yafuatayo

I- NECTA imeondoa msamiati WA kuvuja Kwa Mitihani ya Taifa yote kuanzia STD four mpka form six kabla ya Dr.Msonde uvujaji WA Mitihani lilikua swala la kawaida Sana mitihani ikitundikwa mpka kwenye nguzo za umeme.

2- Dkt. Msonde amefuta msamiati WA vyeti feki sasa hivi kutaka kujua cheti feki NI issue ya sekunde chachetu Tu hivyo hakuna nafasi ya UBASHITE maofisini au cheti kimoja kikatimika na Zaid ya mtu mmoja

3- Dkt. Msonde ameliondoa Baraza kutoka upimaji WA ukariri WA kikasuku,upimaji WA kimaudhui (content) na kulipeleka Baraza kupima Umahiri (competence base) Hivyo taifa kuw na wasomi wabobevu badala ya vilaza vinavyokunywa materials Tu

4-Dkt. Msonde amenza mchakato WA kutoka usahihishaji WA ki Manuela na kulipeleka Baraza upimaji WA E-MARKING ambapo Serikali inaenda Ku save mabiloni ya fedha za walipa Kodi baada kazi hizo kufanyika na computer Kwa umakini Zaid

5- Dkt. Msonde amefanya kazi na wadau wote WA Elimu na kuwahisisha juu ya kazi za Baraza na Baraza kuwa lipo wazi zaidi kujibu Kwa ufasaha kila issue inayoelekezwa kwao

6- Mfumo WA usajili wa watahiniwa upo makini Sana kiasi ambacho mtahiniwa aliekua Kesha MTIHANI NI ngumu Sana kufanya tena MTIHANI bila ya Baraza kumtambua

Yapo mengi aliyoywfanya MZALENDO huyu katika taasisi hii nyeti anastahili Hongera na kushukuruwa Kwa utumishi wake uliotikuka

Dkt. Charles Msonde umeiacha NECTA salama na tunategemea atakaepokea kijiti chako atafata nyayo zako.

NECTA ilikupenda Sana lakini TAIFA limekupenda zaidi tegemeo letu Moto huu utaendelea kuuwasha ktk nafasi yako mpya ya Naibu KATIBU Mkuu (Elimu) ktk wizara ya TAMISEMI.
 
Ni kweli iliyo dhahiri kwamba Dr Msonde ni JEMBE sana tutarajie mabadiliko hata huko alikoenda.
 
Nawaonea huruma saint Anne Marie baada ya mdonde maana aliwapa kila kitu

USSR
 
Back
Top Bottom