Asante CCM kudhihirisha kuwa bila kuwasomba hawaji

Asante CCM kudhihirisha kuwa bila kuwasomba hawaji

IamPrince George

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2014
Posts
412
Reaction score
168
Asante sana, msije mkasahau kuwarudisha na mkumbuke kuwalipa 😀😱
 

Attachments

  • 1443615377424.jpg
    1443615377424.jpg
    42.8 KB · Views: 2,361
  • 1443615549877.jpg
    1443615549877.jpg
    73.7 KB · Views: 2,196
  • 1443615565046.jpg
    1443615565046.jpg
    48.5 KB · Views: 2,101
  • 1443615579202.jpg
    1443615579202.jpg
    72.3 KB · Views: 2,105
Hapa Kazi Tu..

Na Mtaelewa Tu.
Hatuwalipi Ng'o Kudadadekii..Tumeshindwa kuwalipa Walimu wa ajira mpya itakuwa hawaa..!

Magufuli For Change.
 
traffic mko wapi, kwa nini mnaruhusu watu wabebwe Kama nguruwe kwenye lori
 
Hawa CCM lazma wakae msimu huu. Hapo bado kuna na wasanii!! Sasa kunge kuwa hakuna wasanii wala kusafirisha mikutano yao ingekuwa na watu wangapi!? 😃😃😃😃
 
Hivi magari ya aina hii yanaruhusiwa kweli kubeba abiria ?

Hayaruhusiwi sema ubishi tu

traffic mko wapi, kwa nini mnaruhusu watu wabebwe Kama nguruwe kwenye lori

Yanaruhusiwa kuwabeba wanaccm tu wengine wakibebwa ni kosa kubwa sana.

KWA Iringa back 2014...............
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa awapiga marufuku CCM Kubeba Watu Kwenye Malori na Kuwapeleka Mikutanoni. Habari za Uhakika zilizodhibitishwa na Kituo Cha Utangazaji Cha ITV Kwenye Taarifa yake ya Habari ya Usiku wa leo, zimemkariri Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake. Katika Taarifa yake, Kamanda huyo ametoa Onyo Kali Kwa Wanasiasa Wanaotumia mwanya wa nafasi za Uongozi wao Kwa Kuvunja Sheria za Usalama Barabarani, bila Kumung'unya maneno, Kamanda huyo amesema Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wamekuwa wakitumia Madaraka yao Kukodisha Magari yakiwemo Malori Ili Kuwabebea Wafuasi wao Kutoka maeneo ya Vijijini yenye Miundombinu mibovu ya Barabara, na hata Wakati mwingine Viongozi hao huwatelekeza baada ya Mikutano yao, Jambo ambalo limekuwa likiwapa tatizo Polisi Katika Kuwahifadhi, Kuwalisha na hata Kuuhangaikia Usafiri wao Ili Kuwarudisha Makwao. Pia amesema, Jeshi la Polisi halitayavumilia tena Matendo ya Wanasiasa hao.
 
Hawa CCM lazma wakae msimu huu. Hapo bado kuna na wasanii!! Sasa kunge kuwa hakuna wasanii wala kusafirisha mikutano yao ingekuwa na watu wangapi!? 😃😃😃😃

Mafisiem mwaka huu yanatafutana. Mengine yanajaribu kukikana chama maana hakiuziki. SITAWAANGUSHA kwani tupo juu ya miti?
 
Ila kuna kitu mimi nadhani CCM kinawapa point kutokana na kuwasomba watu kwenye maroli. Hebu fikiria kama wamesomba watu kutoka katika vijiji kumi vinavyozunguka eneo husika na kila kijiji kikatoa watu 50, kwenye roli moja , wale 50 wakirudi kijijini wakasimulia wenzao waliobaki kule kijijini hali ilivyo kuwa kule mjini , hamuoni hapo itakuwa kampeni kubwa watakuwa wamefanya kwenye jimbo husika? kwa hiyo tusiwabeze watu hawa na kwa taarifa tu vijijini ndipo penye wapiga kura wengi zaidi. tusindanganyike na mafuriko ya mijini.
 
Back
Top Bottom