As a nation.... We are on the loosing batle

notradamme

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
2,009
452
Baada ya TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI kuahirisha uchaguzi mkuu katika mkoa wa Dar es salaam mwaka 1995, nilahidi na kuapa kuwa'' sitamuamini mwanasiasa yeyote, sitashabikia siasa,sitapiga kura na nitaiangalia siasa na wanasiasa kwa umakini mkubwa'''''
nashukuru nimesimamia hapo hapo tangu kipindi hicho na sijayumbishwa wa kutetereka. Palivyoibuka mgogoro ndani ya NCCR-MAGEUZI hadi kufikia hatua ya akina MARANDO/LAMWAI kwa upande mmoja na MREMA kwa upande mwingine kupigana kule tanga katika mkutano wa chama, nikasema YES i saw it coming na ule ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa NCCR na mrema mwenyewe kisiasa.
ninapojaribu kuyatafakari matukio ya kisisasa ndani ya vyama vyetu vyenye wawakilishi na ushawishi mkubwa kwa watanzania(CCM,CUF na CHADEMA) napata picha inayosikitisha na kukatisha tamaa kwani hakuna chochote kati ya hivi vyama kinachoyeelekea kuenenda na mustakabali wa taifa hili bali ni watu wenye malengo binafsi tena hatarishi kwa usalama wa taifa letu na ustawi wake. na kwa kuliona hili, ni wazi kuwa kama ni vita ya kujikwamua kutoka hapa tulipo, watanzania tunapigana A LOOSING BATTLE.
Kwa kifupi labda nianze na CUF... hiki kimekuwa ni chama cha upande mmoja wa muungano(zanzibar) na hata mienendo ya siasa zake unaonyesha uwepo wake huku bara ni kwa mujibu wa katiba tu lakini kama katiba isingekuwa inawafunga basi ni wazi siasa zao wasingeziendesha huku bara.
kwa hii miaka yote cuf imekua ikwategemea wale wazanzibar MASHOMBESHOMBE wenye asili ya umangani na ndio uungwaji mkono wake unapopatikana, wakati chama cha siasa kinatakiwa kihubiri mshikamano na utangamano miongoni mwa wananchi, tumeona CUF ikihubiri uvunjaji wa muungano, kumkashifu baba wa taifa na kutaka kutuaminisha kuwa nchi hii inaendeshwa kwa mfumo kristo.
pale walipotokea watu wakataka kuleta changamoto ndani ya chama tena bila hata ya kuvunja katiba, panga la sultani wa chama likamshukia na kuwashukia wale wapenda mabadiliko na tukashuhudia HAMMAD RASHID na wenzake wakitupwa SHIMO LA TEWA. KWA UJUMLA DEMOCRASI NDANI YA CUF ni ndoto na hivyo kuindoa kabisa CUF katika orodha ya vyama vyenye hadhi ya kuitwa chama tawala.
kwa kuingalia CCM japo kwa ufupi, hapa ndipo panapokatisha tamaa zaidi. nilikuwa naangali LIVE bunge jana. aliposimama EDWARD NGOYAI LOWASA, ukumbi wa bunge ulirindima kwa shangwe na vigelegele. nikajiuliza nini chanzo???!!! lakini jibu liko wazi.''' mkono mreeeefu wa rushwa umefikia mioyo ya wengi kati ya wale tuliowapa mamlaka ya kutuongoza'' rushwa hii ya kisiasa imefifisha dhana nzima ya uzalendo,imedumaza akili za wasomi, imeua morali ya wanasiasa na imejaza tamaa mioyo ya viongozi.
CCM ya sasa imesimama nje ya misingi iliyojengewa,inakula kile kilichoharamishwa na katiba yake,kinateua wale wasio na sifa kwa mujibu wa katiba yake na kinashangilia uovu/waovu badala ya kupambana dhidi yao.......
wakati wa mwalimu(japo sio kwa100%) ili uwe kingozi ilibidi kwanza ujikane,ujichunguze na kisha ujiridhishe kwamba unaweza kuyaacha ya dunia ili kwenda kuwatumikia watu lakini sasa anaangaliwa yule mwenye uwezo wa kuhonga zaidi(shame!!!) ndie mwenye kuchaguliwa na kukabidhiwa madaraka ya kuongoza watu(wahongwaji!!!??)
Kma taifa, hapa tulikofika ni pabaya na huenda ikawa ndio POINT OF NO RETURN na tukaolekea ndio kwenye maporomoko makali zaidi.
pale wafanyabiashara wenye ukwasi mkubwa ambao hauna FINANCIAL LAYOUT ya kuweza kujua chanzo cha ukwasi huo huku pakiwa na tetesi(ambazo hazijawahi kukanushwa na wahusika) kuwa ukwasi huo umetokana na UFISADI bamoja na biashara haramu(madawa ya kulevya,pembe za ndovu) wanapopata na kupewa nafasi ya kutoa rushwa,ni wazi tunapata chama kama CCM ya sasa.
CCM ya sasa ni ya MWENYE PESA MPISHE..
UKIPEWA CHUKUA...
CHAGUA KWA MISINGI YA HONGO
HATA SHETANI AKITOA HONGO ATACHAGULIWA
MASLAHI YA TAIFA SIO JAMBO LA MSINGI
MASLAHI YA MAKUNDI NA BINAFSI YANATANGULIZWA
WALE WANAPINGA MAOVU WANAPINGA KWA SABABU YA WIVU WA KUKOSA FURSA YA KUFANYA UFISADI.
CHEO SIO DHAMANA BASLI NI MCHONGO WA KUJITAJIRISHA NA KUJIJENGEA HIMAYA.
UNGOZI SASA NI SWALA LA KUFA NA KUPONA(bila kujali kama unaweza ama laa)
kwa machache hayo hapo juu ni wazi kwamba CCM haitafsiri tena uongozi kama utumishi bali uongozi unatafsiriwa kama ni bidhaa iliyo sokoni tayari kwa kuuzwa kwa mteja mwenye mapesa mengi. na kwa mantiki hiyo, UFISADI ndio uti wa mgongo wa chama kwani kupitia ufisadi watu wanapata uwezo wa kununua kila kitu(makasisi,mapadri,wachungaji,maaskofu,maulamaa,maustaadhi,masheikh na mamufti), ufisadi unaweza kununua watu wote(wabunge,madiwani,wakuu wa wilaya, makatibu,wenyeviti wa chama ngazi mbalimbali,wajumbe wa NEC na wajumbe wa mkutano mkuu). Kwa mantiki hiyo mafisadi hawazuiliki na mwishowe wanaweza kununua UONGOZI WA NCHI(URAISI).
Kwa yale tunayoyashuhudi ndani ya CCM, ni ashirio tosha kwamba fedha(halali/haramu) ndio zitaamua nani awe kingozi katika nafasi yoyote hata URAISI.
Kwangu mimi huu ulikuwa ndio muda muafaka wa kuipeleka CCM likizo ya mafunzo ili ikajihoji na kujitazama upya na ikibidi kujisafisha na kurudi katika misingi yake kabla haijaja tena kujaribu kuomba ridhaa ya watanzania kuongoza tena hii nchi. lakini swali la msingi linakuja,, ni nani wa kumkabidhi nchi wakati CCM ikipelekwa likizo ya mafunzo?????? hapo haswaa ndipo kwenye mtego mgumu kwa taifa letu.......
wakati WILBROD SLAA na ZITO KABWE wanalitetemesha bunge la tanzania wakiwa kama wawakilishi toka majimbo yao, wengine tulisema'' huenda sasa ule muda umewadia'''.. waliweza kulipeleka bunge na kulishinikiza lifikie maamuzi waliyoyataka wao kwa kupitia hoja nzito na zenye kueleweka mpaka ikafika mahali wananchi wakawa wanajua kabisa kwamba watetezi wao ni wa kina nani.
hapakuwa na malumbano ya kutaka sifa binafsi(kama wakina MNYIKA) bali ilikuwa ni taifa dhidi ya watawala,ukweli dhidi ya uongo,uzalendo dhidi ya mafisadi,haki dhidi ya batili na weledi dhidi ya ukanjanja.
2010 Ikawa turning point, uteuzi wa W.SLAA kama mgombea wa uraisi kupitia chadema ikwa turufu nzuri ya kisiasa, kutokana na background ya utendaji wake uliotukuka bungeni wananchi wengi wakaona ngoja tumuunge mkono yeye na chama chake. kama maandalizi ya kumuweka SLAA yangefanyika mapema ndani ya chama nina hakika idadi ya wabunge wa chadema ingekuwa kubwa kkuliko sasa na hata idadi ya kura za uraisi zingeongezeka na hivyo basi chama kingefaidika na ruzuku kuliko ilivyo sasa.
kwa wale wenye ufahamu tulikuwa tunaelewa fika tatizo lililopo ndani ya CHADEMA kabla hakijapata huu umaarufu iliyonayo sasa. tatizo hilo lilikuwa ni chama kuendeshwa kwa misingi ya KISACCOS,KIKABILA na KIFAMILIA. kwa umaarufu wa W.SLAA baada ya uchaguzi 2010 tulidhani kuwa W.SLAA atakiteka chama toka mikononi mwa wanafamilia na kukipa taswira ya utaifa(na niliwahi kuliandika hili humu jf) lakini badala yake nae akaangukia kuwa mfuasi wa kikundi kile kidogo cha kikabila na kuicha status yake ikitumiwa na watu wengine kukijenga chama ambacho sio chake na kuwajenga watu wengine kisiasa wasio na malengo kama yake.
Labda niwakumbushe kidogo historia ya vyama vya kupigania uhuru nchi mwetu tangia AFRICAN ASSOCIATION(AA)..
By then Nyerere alikuwa ni mgeni hapa dar es salaam ni mwalimu kule pugu secondary, kwa uwezo na uzalendo wake akawa anakuja kwa mguu hadi maeneo ya kariakoo kukutana na akina SYKES NA MTEMVU kwa ajili ya kujadili ukombozi wa tanganyika. pamoja na ugeni wake, mwalimu alijikuta anakubalika miongoni mwa wahafidhina watoto wa mjini na mpaka kuja kuundwa kwa TANU. ni walewale watoto wa mjini waliokuwa wanajua wapi pa kupata fedha, walikuwa wanajua na wana ndugu katika takriban mikoa yote ya tanzania na ndugu hao wa mikoani walikuwa na influence katika miji husika. wakachanga fedha na kumsafirisha mwalimu kwenda mikoani na kumpa mabarua yenye ujumbe mzito kuwapelekea wenyeji wake huko mikoani na mwalimu akajikuta kila anapoenda anapokelewa vizuri,anakula na kulala vizuri na kupewa nafasi ya kueneza ujumbe wa ukombozi aliokuja nao..
hadi nyerere anarudi dar es salaam, akajikuta yeye ndio nembo ya TANU na mikoa yooote wanamtambua yeye. na kwa sababu kimtazamo alikuwa amewaacha wenzake mbaali na kwa sababu alihisi wenzake hawako serious na mipango ya uhuru, Nyerere aliamua kuiteka TANU na mpaka uhuru yeye ndio akawa nembo ya TANU na kiongozi wa nchi.......

Tulidhani W.slaa atafanya hivi, ataipora chadema toka uchagani(familia) na kuifanya kama nembo ya kitaifa.
hilo limemshinda na ameamua kugeuka kuwa mwanafamilia na mfuasi wa mmoja wa wanafamilia.
-------- yeyote atahoji"eti mbona chadema kina matawi na wanachama kila kona ya nchi ambako sio uchagani????'''
tunapoongelea wenye chama, hatuongelei wanachama na washabiki, tunaongelea wale wenye mamlaka ya kutoa maamuzi ya chama(vikao vya juu vya kimaamuzi kama vile MKUTANO MKUU,KAMATI KUU NA HALMASHAURI KUU)
huku ndiko utawakuta wenye chama na huku ndiko haswaa ile familia na lile kabila lilipojikita.halitaki kuachia nafasi kwa yeyote na yule atakayeachiwa nafasi lazima atangaze ufuasi na utii..hawakubali kukosolewa na yeyote anayejaribu kuwakosoa ataitwa MSALITI. hawakubali mapato na matumizi yao yahojiwe na atakayejaribu atakuwa AMETUMWA.wameisigina na kuipiga teke democrasia kiasi cha kutishia uhai wa chama. hakuna anaestahili kugombea nafasi yoyote bali awe ameshateuliwa na babamwenyekiti. wanapigana vikumbo na kutishiana maisha,wanaapizana na kushikana uchawi, wako walio tayari kuwatosa wengine baharini na wapo walio tayari kugawana mbao za jahazi wakidhani bila ya uzima wa jahazi wanaweza wakaivuka bahari.imefika mahali michango iliyotukuka ya baadhi ya makada haithaminiki kwa sababu tu hawatoki KASKAZINI. wasiotoka kaskazini wanaitwa majina yote mabaya. wanapakwa rangi ya shetani na kupuliziwa harufu ya kinyesi.
chama kimegeuka danguro, kila mwenye mpenzi wake atatafutiwa nafasi(wame copy na kupest toka CCM!!!), chama kinafanya HARAKATI badala ya kufanya siasa, kimegeuka kuwa chaka la wanaharakati njaa badala ya wanasiasa mahiri
. kinataka matokeo makubwa sasa(BIG RESULTNOW!!!) bila kuwekeza toka kweye mashina. hakina plani za kuchukua majimbo zaidi(kumbuka zaidi ya 2/3 ya wabunge ni CCM) BALI KINA NDOTO ZA KUSHINDA URAISI.
haya ni mapungufu yasiyomithilika, mapungufu yanayowanyima watanzania nafasi ya kuwa na mbadala wa CCM hapo miaka 15 mbeleni(ni ndoto kuishinda CCM in next 10 years). ni mapungufu yanayotuonyesha udhaifu mkubwa wa wanasiasa wa kitanzania na kwa ujumla ni mapungufu yanayokatisha tamaa.
nikiulizwa mimi nitoe msimamo kuhusu mapungufu ya hivi vyama vitatu na kulazimishwa kuchagua mapungufu yenye afadhali, bila kumung'unya maneno ntasema''WE BETTER OPT FOR A DEVIL WE KNOW THAN AN ANJEL WE DONT KNOW'''
AAcha tutawaliwe na MAFISADIi kuliko kutawaliwa na WABAGUZI WA RANGI(CUF) na WABAGUZI WA KIKABILA(CHADEMA).
NAKARIBISHA MATUSI
 
Hebu fupisha habaari yako, japo umefanya kazi ya copying & pasting not bad, ungejitaidi kuandika in summary by writing sam points.
 
Ukweli mtupu Mkuu na uyasemayo yote nilikwishayaona ni juu yao sasa Viongozi wa Chadema aidha wabadilike na waijenge Taasisi yenye sura ya kitaifa/yenye kujali uwazi na demokrasia/yenye kuheshimu maelekezo ya Katiba/yenye kuheshimu maoni ya Wanachama.Kama wakijirekebisha kwenye hayo nadhani hapo tutaitoa CCM madarakani 2015.
 
Ni kweli kabisa kiongozi!
Watz tumekwisha changanywa kiasi kwamba huwezi jua umuamini nani, umsikilize nani na umfuate nani! Waasisi wa nchi hii walitumia nguvu ya ziada kuweka mikakati ya muda mrefu ya kuhakikisha wanaendesha nchi hii kwa malengo ya kutawala......na mikakaati hiyo imeota mizizi ambayo kuingoa kuna kazi ya ajabu.........Ndani ya mikakati hiyo ndio kuna hao kina Mrema, na wanafiki wengine. Dawa yake ni moja tuu, lishuke tetemeko hapa na kufagia woote tuliopo, kianze kizazi kipya!
 
ukweli mtupu, wajiandae kuona U TURN kwa the so called nguvu ya UMMA
 
Hebu fupisha habaari yako, japo umefanya kazi ya copying & pasting not bad, ungejitaidi kuandika in summary by writing sam points.

Uvivu wako wa kusoma utakusababisha kupitwa na mengi sana.

Back to the topic, wengi wanakata tamaa, but I don't think it is the right attitude. This merely underlines that you (wanachama) have failed to connect with the party leaders. Because they benefit from the status quo they are not likely to notice (or recognize) that adjustments are required. What should the people do to send the message accross and get the train back on track? Uchaguzi bado, nafasi ya kuleta mabadiliko bado ipo.
 
Any change just begins from within and then goes outward affecting all the things around it positively!It's necessary to overhaul the whole system now i mean our thinking system,political system,economic system,administrative & government system as well as security system from our own political entity (Chadema) in order to distinguish them from the ruling party (CCM) and once we put them on power we should expect them to run things differently and make a difference to our Country.
 
The problem now (IMO) seem to be the leaders' priorities vs the party members priorities. On paper they are still aligned (poverty reduction, democracy and accountability, natural resource management etc) but there is not a single sustainable party plan to advance these agenda. Each mp or party leader is working on his own when he talks about them.
I don't think the leadership would just wake up and start focusing on these issues as they used to, unless the grassroot level speaks out loudly.
Chadema has the unique advantage of having local leadership. Party members should start asking updates on these questions from there (not on jf or twitter) and then leaders will understand that their little fights over personal interests (positioning or financial interests) is of little interest to the average Tanzanian.
I believe it starts with the people. Don't expect the leadership to take bold action without pressure.
 
Ni kweli kabisa kiongozi!
Watz tumekwisha changanywa kiasi kwamba huwezi jua umuamini nani, umsikilize nani na umfuate nani! Waasisi wa nchi hii walitumia nguvu ya ziada kuweka mikakati ya muda mrefu ya kuhakikisha wanaendesha nchi hii kwa malengo ya kutawala......na mikakaati hiyo imeota mizizi ambayo kuingoa kuna kazi ya ajabu.........Ndani ya mikakati hiyo ndio kuna hao kina Mrema, na wanafiki wengine. Dawa yake ni moja tuu, lishuke tetemeko hapa na kufagia woote tuliopo, kianze kizazi kipya!

mapinduzi ya kijeshi.. tumpate KAGAME WETU,TUMPATE THOMAS SANCARA WETU,TUMPATE ABEID AMAN KARUME WETU....
walioko shule wasome kwa lazima(kwani taifa linawategemea)
walioo mashambani walime(wawezeshwe na waambiwe kwa mtutu wa bunduki kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa)
walioko maofisini wafanye kazi inayowapasa(pawepo monitoring system ya ANIHILATION ya wote walio wavivu)
ufisadi na mafisadi wasipelekwe mahakamani( panapo ushahidi adhabu ya kifo itekelezwe bila kuchelewa)
piga chini siasa za vyama(na yeyote mleta chokochoko auwawe)
itangazwe hali ya hatari kiuchumi(hapa hakuna kufunga mikanda bali ni kufanya kazi kwa kupenda ama kwa lazima)
futa mikataba yote(iwe ya madini,wanyama,gesi na maliasili nyingine) na kuchukua uelekeo mpya
KWA UFUPI TUNATAKIWA TUONGOZWE '''KIDIKTETA'... tupate dikteta mzalendo ambaye akitoa tamko kule KIBONDO basi mwangwi wakehata mtu wa kule MWEMBELADU pemba atausikia.akikohoa UKEREWE WATASIKIA WATU WA MTO RUVUMA
 
Pole sana wewe ndio tataizo unatukwamisha kwa kutaka kutuaminisha kwamba chadema ni mtei ,mbowe,slaa,zitto,lema nakadharika nadhani hasira zako zipooze tu ,unajulikana huwa unachanganyikiwa sana unapoadhiriwa ni vizuri tofauti zenu muziweke wazi jamii tujuwe manake munavyofanya kwenye vikao vyenu vya chama kila mtu huwa anatoa uongo wake sasa wekeni mengi tuu kama wewe unavyotishia watu hapa baada ya siku mutafika mahala mutaona muyafanyayo ni mchakato ili mufike mahala muwe na moja la kulisimamia, chadema imejengwa na imepokelewa na wananchi ndio wanaaokilinda kwa sasa sio hao hapo juu
 
Pole mission failed mumeshindwa kuvisambaratisha pamoja na NCCR kupatwa na misukosuko bado ipo vile vile TLP kw a hiyo sasa munakata tama kwa sababu wanasiasa munaanikana tulieni
 
Pole mission failed mumeshindwa kuvisambaratisha pamoja na NCCR kupatwa na misukosuko bado ipo vile vile TLP kw a hiyo sasa munakata tama kwa sababu wanasiasa munaanikana tulieni
DO I SOUND LIKE A POLITICIAN?????!!!!!!
so sorry but i am sure'""WE DON'T SHARE THE SAME LEVEL OF THINKING"" keep on believing in them(politician) and death awaits you right there
 
Pole sana wewe ndio tataizo unatukwamisha kwa kutaka kutuaminisha kwamba chadema ni mtei ,mbowe,slaa,zitto,lema nakadharika nadhani hasira zako zipooze tu ,unajulikana huwa unachanganyikiwa sana unapoadhiriwa ni vizuri tofauti zenu muziweke wazi jamii tujuwe manake munavyofanya kwenye vikao vyenu vya chama kila mtu huwa anatoa uongo wake sasa wekeni mengi tuu kama wewe unavyotishia watu hapa baada ya siku mutafika mahala mutaona muyafanyayo ni mchakato ili mufike mahala muwe na moja la kulisimamia, chadema imejengwa na imepokelewa na wananchi ndio wanaaokilinda kwa sasa sio hao hapo juu
na wewe ni mmoja kati ya wananchi na wafuasi wa chadema, can you tell me who will be your next CHADEMA chairman???
ndugu, hata wana CCM wasingependa kuona watu kama LOWASA wakiwa viongozi. lakini hawana ubavu wa kuwazuia ... unajua ni kwa nini!!!??? kule kwenye vikao vya maamuzi ndiko lowasa alikowekeza.
utatoa povu kubishana lakini huo ndio ukweli kwamba"""SISI WENGI NI WASHABIKI,WAFUASI,WANACHAMA TUTAKAOISHIA KUANDAMANA NA KUPIGA LONGOLONGO TUUU LAKINI WENYE VYAMA WALA HAWATHAMINI MAWAZO NA MAONI YETU"""
 
DO I SOUND LIKE A POLITICIAN?????!!!!!!
so sorry but i am sure'""WE DON'T SHARE THE SAME LEVEL OF THINKING"" keep on believing in them(politician) and death awaits you right there

Waste no time with partymen!!!!!

Let us steadily analyse this situation for the better future of our Nation and not mere political parties!!!!!
 
Siwaoni wanaojiita Pro-CHADEMA wala Pro-CCM humu hope wanakuja wanachungulia halafu wanaondoka kimya kimya kwa maumivu ya ndani kwa ndani baada ya kugundua kuwa walifanywa mazuzu kwa muda mrefu na viongozi wa vyama vyao
 
wachache sanaaa party followers huwa wanasimamia ustawi wa nchi kwa ujumla wao ni vyama tu hata kama ni kwa gharama ya Watanzania!!!!!!

Cc Aspirin, gfsonwin, Gagnija, Pasco

Mkwamo upo hapo kaka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom