Waziri2025
Senior Member
- Sep 2, 2019
- 149
- 380
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Iddy Kimanta amemvaa vikali mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo kutokana na kauli ambazo amekuwa akizitoa za kutetea watu wasilipe Kodi na hivyo kuikosesha mapato serikali.
Akiongea katika semina elekezi ya madiwani wa jiji la Arusha ,Kimanta bila kutaka jina la mlengwa alisema kuwa kumeibuka watu kutetea watu wasilipe Kodi na hivyo kukinzana na maelekezo yanayotolewa na serikali kuhusu ukusanyaji wa mapato katika halmashauri.
Hivi karibuni mbunge wa Gambo akiongea na wafanyabiashara wa maduka katika eneo la Kilombero ambao maduka yao yalifungwa na mkurugenzi wa jiji kutokana na malimbikizo ya Kodi ,ambapo Gambo alikosoa hatua hiyo na kuwahimiza wafanyabiashara kuendeleza na biashara zao kwa sababu mwenye mamlaka ya kufunga maduka ni Baraza la madiwani.
Aidha Kimanta amewataka madiwani wa halmashauri ya jiji la Arusha kushirikiana na mkurugenzi wa jiji hilo katika kuhakikisha mazingira mapato ya halmashauri yanaongezeka .
Aidha pia aliwataka kusimamia sheria,kanuni na taratibu za halmashauri hiyo katika kuwatumikia wananchii ili kuweza kuleta maendeleo kwa jamii hivyo wasiwe watu wa kupinga serikali katika ukusanyaji wa mapato na atayetokea kupinga asipewe nafasi.
Alisema wasipokusanya mapato maendeleo kama miundombinu ya maji,barabara na afya haviwezi kuendelea kwani hawapo kufurahishana bali kusimamia serikali katika kufikia malengo yake ya kuwaletea maendeleo wananchi.
"Mpaka itakapofika mwezi Juni halmashauri inatakiwa iwe imekusanya billioni 22 laki hadi sasa imekusanya bilioni 6 kwa maana hii mnatakiwa kuongeza juhudi katika ujusanyaji wa mapato ili kufikia malengo haya kwani nguvu ya halmashauri ya jiji ni uwezo wake wa mapato," Alieleza.
Pia alisisitiza usimamizi wa miradi uendane na thamani halisi ya fedha kwani wananchi hawakufanya makosa kuwachagua bali walitegemea watawawakilisha vyema na kuleta maendeleo katika maeneo yao.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha Kenani Kihongosi aliwasihi madiwani hao kuwana upendo na kuepuka migogoro isiyo na maana bali wasimamie mapato kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri ya jiji la Arusha.
Kenani alisema wote kwa pamoja wanajenga nyumba moja wanatakiwa kupendana na kufanya kazi pamoja na endapo akitokea mmoja au wawili watakaona wao ni zaidi ya wengine akiwa kama kiongozi wa wilaya hata sita kushughulika nao.
"Tupendane, tusiingie kwenye mambo ambayo yatapasua halmashauri hii, kumbukeni wakati mnaomba kura mliwaahidi nini wananchi, itakuwa ni fedhea na aibu baraza hili likiingia katika mgogoro,"Alieleza.
Naye Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Dkt John Pima alisema watahakikisha wanasimamia mapato pamoja na usafi wa mazingira huku akiwataka wananchi kutekeleza wajibu wao bila kusubiri mkono wa serikali.
Alisema kuna suala la watu kuchukua uchafu na kubeba kwenye magari yao na kuutupa barabarani na wengine wanajua mahali pa kutupa lakini wanatupa mahali popote jiji litawachukulia hatua za kisheria laki pia alitoa rai kuwa usafi ni afya hivyo waache kutupa taka hovyo bali wafuate taratibu na sheria za utupaji wa taka katika maeneo husika.