Arusha ,mji ulionifanya kukosa amani.

Arusha ,mji ulionifanya kukosa amani.

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Posts
23,372
Reaction score
55,027
Nimekumbuka sana mji wa Arusha ambao kiukweli ulikuwa mji mzuri na wenye hali nzuri ya hewa ila gharama za maisha zilikuwa juu sana (nadhani sababu kuu ni utalii)

Nikiuzungumzia mji huu sitoacha kukumbuka tukio hili ambalo liliniacha na maswali mengi,Mnamo mwezi june mwaka 2015 wakati nikiwa chuoni katika mji wa Arusha nilikuwa naenda kwenye bar moja "kilimanjaro bar" ipo mkabala na city link.

Siku hiyo nilifika hapo kuangalia mechi na katika bar ile ulikuwa ukinunua kinywaji na kuangalia mtanange wako bila wasiwasi.

Wakati naingia kwenye hiyo bar mimi na mwenzangu moja kwa moja hadi kaunta nikatoa wallet nikanunua take away Mbili (soda),Ila wakati nipo kaunta pembeni yangu alikuwepo ndugu mmoja anaweza kuwa na umri kati ya miaka 35-45 alinisalimia "vipi kaka" nikamjibu nikachukua soda zangu mbili,moja yangu na nyingine ya mwenzangu ile nataka kuondoka akaniita akamwambia mhudumu mmoja kuwa "huyo kaka mpe pombe nitalipia mimi" nikamwambia "situmii kilevi chochote"

Akaonekana kutahamaki ila akasema nile chochote nachotaka maana pale bar kulikuwa na nyama choma na vitu mbalimbali ila nilimwambia "Nashukuru",kiukweli mimi ni ngumu sana kumzoea mtu kwa muda mfupi ,yote hii ilinifanya nione kama naboreka kuendelea na maongezi yale.

Baada ya kukataa offer zile akampa mhudumu Tsh 1000/= akamwambia nikimaliza soda niongeze,basi wakati naangalia mpira alirudi ndani , yeye alikuwa amekaa nje ya bar akanichek akaniuliza "upo" nikamjibu na akaniambia "ukimaliza kinywaji chukua tena nimekwisha lipia",bado nilikuwa sijajua yule mtu ni nani na kwanini amenichangamkia kiasi kile.

Ilipofika mapumziko nikiwa nimeboreka kwa ukaribu ule nikaamua kumuaga mwenzangu na kurudi kulala ,ile natoka tu nje nikakutana nae akiwa mezani na wenzake kama wanne (wanaume 3 na Binti 1) walikuwa wanakula nakunywa pombe.

Alinishika mkono na kunisogeza mbele ya wale wenzake na kuanza kunihoji maswali " wewe ni mwenyeji wa arusha? Nilijibu natokea mkoa mmoja kanda ya ziwa akasema "kweli kwa mwili huo sishangai kutokea huko" nilizidi kujiuliza yeye ni nani na anataka nini baada ya muda nikamwomba tuzungumze moja ya lugha iliyopo mkoani mara ila akasema yeye si wa huko ni mtu wa Kigoma (ila awali aliniambia yeye ni mzaliwa wa mkoani mara )

Nikiendelea na mazungumzo mmoja kati ya wale wenzake akasimama na tablet na akaanza kutupiga picha nikiwa na yule mtu,alipiga picha kama Tano (akili ilianza kwenda kasi ikizidi kutaka kujua wale ni wakina nani na wana nia gani na mimi hadi kufikia kunipiga picha).

Baada ya cameraman kufanya yake jamaa aliomba namba za simu na akaomba nimtafute kesho yake (saa nne asubuhi,huku akisisitiza) nilichukua zile namba ila mimi sikumpa namba zangu.

Aliniuliza napoishi nikazidi kusema uongo kwani huwa sipendi kujivua nguo kwa mtu nisiyemjua ,basi nikaagana nae kisha nikaondoka ma kwenda kulala baada ya kuona mwili wangu umekataa kukaa sehemu ile.

Kesho yake na mimi sikumtafuta nilichana karatasi yenye namba zake nakumbuka zilikuwa za Airtel.

Sikumwambia mwanachuo yeyote juu ya tukio lile hadi leo na huwa nikilikumbuka huwa nakosa sana amani kwanza zile picha zilikuwa na maana gani !!! Hali hii ilinifanya kukosa amani kwa muda mrefu nikiwa jijini Arusha.

Kama kuna mdau JF ashakutana na watu wa aina hii basi unaweza funguka ili niangalie nia na lengo lao kwangu lilikuwa ni lipi.

Natanguliza shukrani.
 
Kwa maelezo yako hapo juu,nimeyatambua yafuatayo.

1. We ni mtu mnene na mrefu uliyejengeka kwa Misuli
2. Wewe una kila mfanano na kabila la Wasukuma.

Kutokana na hayo niliyoayaanisha hapo juu,haya ni baadhi ya mawazo.

Mosi,wale hawakua watu wazuri kwako. Walikua na njama yoyote ya Uhalifu na muonekano wao uli-match shughuli zao za kihalifu.

Pili,zile picha zilipigwa makusudi either ni ili wakikaa sawa kuanza kupanga madili yao waamue wakupange katika nafasi gani. Au ungewatafuta alafu ukakataa kujumuika nao,wangekua na picha yako na popote pale wangekusaka kutokana na labda wangeshakuambia madili yao.

Tatu,labda walikua na lengo la kujipatia fedha kwa njia za Kitapeli. Kwamba,ungewatafuta tu wangeambatanisha picha zako na namba zako za simu na ungetafutwa.

Nne,hao ni Waganga njaa tu labda. Watu wazito na madili mazito hawatoi buku kukushawishi au kutumia njia za kitoto hivyo kukupata. Njia nyingi ni technical na za kutumia akili ya juu yaani Daraja la Kwanza.

Tano,huenda walikufananisha na mtu wanayemhitaji ambao hawamjui na badala yake tu walipewa dili la kumtafuta na pengine walikufananisha.

Sita,Kamshukuru MUNGU alikuepushia njama na hila zao.

Haya ni mawazo yangu tu na naomba yasifungamanishwe na upande wowote
 
Asante sana kaka kwa uchambuzi wako juu ya tukio hili , naamini Mungu alikuwa upande wangu.
 
Back
Top Bottom