The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 9,434
- 10,970
Wadau polenj na pilika pilika za Maisha..
Mfanyabiashara Oscar Nondo wa Arusha amewajengea mbwa Wake Hoteli yenye thamani ya Shilingi Million 80..
Kwenye Maisha usije kusema tuna maisha magumu Bali kila mtu ajisemee nafsi yake..
Soma habari kamili hapa 👇
----
DUNIA ina mambo! Ndicho unachoweza kusema baada ya Mfanyabiashara, Oscar Nondo wa jijini Arusha kujenga hoteli ya kisasa iliyomgharimu Sh. milioni 80 kwa ajili ya kulaza mbwa wake.
Makazi hayo ya mbwa ambayo hayakutegemewa na wengi kwenye Jiji la Arusha ambalo ni kitovu cha utalii nchini, yamejengwa eneo la Kwa Morombo jijini.
Akizugumza na Nipashe jana nyumbani kwake, Nondo alisema ameamua kujenga hoteli hiyo ya kisasa kama makazi ya mbwa wake kwa kuwa watu wengi wanaofuga mbwa, wanajenga vibanda visivyo na hadhi kwa ajili ya kuwalaza wanyama hao, jambo ambalo siyo sahihi.
"Mbwa wanahitaji kulala mahali pazuri na kula vizuri kama tunavyokula sisi binadamu, hivyo nimeamua kuwajengea 'Lodge' hii ili nao walale mahali pazuri," alisema.
Mfanyabiashara huyo alibainisha kuwa mbwa anaowafuga nyumbani kwake Kwa Morombo, anawachukua kutok Poland, ambao ni aina ya Shepherd na wengine waliopo kwa wingi wametoka Afrika Kusini.
"Mbwa wanahitaji mafunzo kama tunavyotunza watoto wetu na kila siku lazima kuamka kumjulia hali ili kama anaumwa unaita daktari mara moja anakuja kumtibu," alisema.
Chanzo: Arusha Zone