Arusha: Mfanyabiashara afariki kwenye ajali ya gari

MFANYABIASHARA AFARIKI KWENYE AJALI ARUSHA, TAJIRI ALIYEMVUNJIA MWANDISHI KADI ALAZWA ICU KWA KUJERUHIWA VIBAYA

Mfanyabiashara Cuthbert Temba anayemiliki CET GARDEN iliyopo kwa mrefu barabara kuu ya Moshi Arusha amefariki dunia yeye na dereva wake wakitoka kwenye maziko Old Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Wengine waliokumbwa na ajali hiyo ni pamoja na mfanyabiashara maarufu, Mekline Temu maarufu kwa jina la DENSO na Ngarasoni ambao wapo mahututi hospItalini wakipatiwa matibabu.

Katika ajali hiyo iliyotokea maeneo ya kwa Mrefu Arusha ni eneo hilohilo ambapo alifia mtoto wake akiwa na mchumba wake huku ikielezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kwamba mtoto huyo akiwa na mpenzi wake walikuwa wamelewa.

Ikumbukwe kuwa Denso aliyepata ajali na kulazwa ICU alishirikiana na watoto wake kumletea vurugu Mwandishi wa Ayo Tv Arusha na kumvunjia kadi yake ya camera akizuia kutokuripoti habari hiyo ambayo ilikuwa na utata.

Tajiri huyo ambaye amekuwa mtata alipata ajali akiwa anatokea kwenye Mazishi ya mzee Mshiu wa TFA huku taarifa zikiwa zinadai kwamba walikuwa wamelewa kwenye gari hiyo ndogo ambayo imeua watu wawili hapohapo na kujeruhi wengine.
Na itakua walilewa mana sehemu yenyewe imenyooka na hakuna kona wala nini
 
Yule mwandishi alizingua yani unaenda msibani unaanza kupiga picha hutoi hata pole wala kuomba ruhusa.
Wapumbavu sana wale, walishakuja kwny msiba wa ndugu yangu maeneo ya Ilboru huko juu wakaanza huo upumbavu wa kuhojihoji na kupiga kiboya bila kutoa pole au kuonana na Wafiwa

Tuliwatimua wote, walikuja wanne na wa Radio 5 ya Lowassa
 
Huyu Cuthbert ndo yule mmiliki wa Aksante Tours?
 
MFANYABIASHARA AFARIKI KWENYE AJALI ARUSHA, TAJIRI ALIYEMVUNJIA MWANDISHI KADI ALAZWA ICU KWA KUJERUHIWA VIBAYA

Mfanyabiashara Cuthbert Temba anayemiliki CET GARDEN iliyopo kwa mrefu barabara kuu ya Moshi Arusha amefariki dunia yeye na dereva wake wakitoka kwenye maziko Old Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Wengine waliokumbwa na ajali hiyo ni pamoja na mfanyabiashara maarufu, Mekline Temu maarufu kwa jina la DENSO na Ngarasoni ambao wapo mahututi hospItalini wakipatiwa matibabu.

Katika ajali hiyo iliyotokea maeneo ya kwa Mrefu Arusha ni eneo hilohilo ambapo alifia mtoto wake akiwa na mchumba wake huku ikielezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kwamba mtoto huyo akiwa na mpenzi wake walikuwa wamelewa.

Ikumbukwe kuwa Denso aliyepata ajali na kulazwa ICU alishirikiana na watoto wake kumletea vurugu Mwandishi wa Ayo Tv Arusha na kumvunjia kadi yake ya camera akizuia kutokuripoti habari hiyo ambayo ilikuwa na utata.

Tajiri huyo ambaye amekuwa mtata alipata ajali akiwa anatokea kwenye Mazishi ya mzee Mshiu wa TFA huku taarifa zikiwa zinadai kwamba walikuwa wamelewa kwenye gari hiyo ndogo ambayo imeua watu wawili hapohapo na kujeruhi wengine.
hilo eneo walilofia itakuwa walishawahi kufanya kitendo kibaya hapo na wenye kulipiza kisasi wakaweka tego!
familia imeishia hapo kwa awamu
 
Back
Top Bottom