Arusha: Mfanyabiashara adai kupigwa na kubambikiwa bangi na Polisi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
MFANYABIASHARA mtanzania na Mkazi wa Marekani na Arumeru Mkoani hapa,Ombeni Palangyo(36)amedai kutendewa unyama na askari polisi jiji la Arusha,kupigwa na kubambikiwa misokoto ya bangi wakitishia kumpa kesi ya uhujumu uchumi iwapo hata wapatia pesa .

Akiongea kwa uchungu Palangyo ambaye alikuja nchini kwa shughuli za kibiashara ikiwemo kuzindua mgahawa wake eneo la Mianzini,alisema kuwa siku ya tukio Machi,23 mwaka huu alitekwa na askari wawili eneo la Mianziani katika bucha la nyama baada ya kutoka kuchukua fedha kwenye ATM iliyopo eneo hilo .

Alidai kuwa akiwa katika bucha hilo la Kitimoto majira ya saa 2.35 usiku,alifuatwa na askari wawili ambapo mmoja alimpiga ngumi usoni na kumjeruhi mdomoni na baadaye walimfunga pingu mikononi na kumburuza hadi kwenye Gari dogo waliyokuwa wakiitumia(sio gari la polisi)

Alisema akiwa ndani ya hiyo gari watu hao ambao walijitambulisha kwake ni askari polisi walikuwa wakimpiga na kumtukana matusi ya nguoni wakimwambia unajidai mjanja sana leo tunakupoteza.

Alisema walimzunguka.naye maeneo mbalimbali na baadaye katika mzu guko wa Florida (Florida round bout) jijini hapa mara tatu baada ya kushituka kwamba kuna watu wanawafutiliwa kwa nyuma ambao walikuwa ni jamaa zake na Palangyo waliopata taarifa juu ya kukamatwa kwake .

Alidai kwamba askari hao waliamua kumpeleka kituo kidogo cha polisi kilichopo Kaloleni na walipomfikisha mmoja ya askari hao alichomoa burungutu la misokoto ya bangi akidai kwamba mtuhumiwa huyo amekutwa na bangi.

"Waliponifikisha Kituo cha Polisi mmoja ya askari hao alichomoa bangi mabunda matatu na kudai wamenikamata na bangi huku wakinitukana matusi makubwa wakidai huyu jamaa ni jeuri sana"

"Niliwaambia kuwa mimi ni mwanasheria na nina tiketi ya ndege na kesho nasafiri kuelekea Marekani , sitaruhusu mnibambikizie bangi niliwaambia wachukue silaha zao waniulie palepale kituoni"alisema PALANGYO.

Aliongeza kuwa baada ya kulalamika kwa muda mrefu huku akipiga kelele kituoni hapo wale askari polisi waliendelea kumtukana matusi makubwa huku wakimtishia kumpeleka kituo kikuu cha polisi(police Central)ili akafunguliwe kesi ya uhujumu

Hata hivyo mmoja ya askari hao alimfuata na kumtuliza akimwambia apunguze jazba ila atafute shilingi laki moja ili wamwachie aende zake.

"Niliwambia kuwa pesa hiyo nitawapatia ila wanipatie ritisi kwa sababu mimi sio mhalifu na sijui hii pesa naitoa kwa ajili gani ila nimeamua kuwapatia ili kuondoa usumbufu kwa sababu kesho yake nilikuwa nasafiri kuelekea Marekani "alisema.

Alisema askari hao walipokea kiasi hicho cha pesa na kumwamuru aondoke eneo hilo .Hata hivyo alidai kwamba hakuweza kutoa taarifa polisi kwa kuwa aliingiwa na hofu baada ya kubaini kwamba polisi hao walimtishia kumfuatilia.

Palangyo ambaye kampuni yake hushughulika na masuala ya kutafuta watalii na kuwaleta nchini ,aliamua kutoa taarifa kwa ubalozi wa marekani nchini ,ambao walimshauri aondoke mkoani hapa na aende katika ubalozi huo kwa msaada zaidi .

"Niliamua kukimbia Arusha kwa siku saba nikihofia maisha yangu ila juzi ndo nimeondoka kurejea nchini marekani"alisema.

Mmoja ya shuhuda wa tukio hilo,Michael Palangyo, alisema siku ya tukio akiwa na Palangyo katika mgahawa wake alimsindikiza kwenda kununua nyama Buchani baada ya wateja kuhitaji.

Alisema akiwa Buchani majira ya usiku Palangyo alikuwa akivuta sigara kubwa(Siger)ambapo walitokea askari wawili na kumhoji Palangyo kuwa anavuta nini na alipowajibu kuwa ni sigara (Siger)hawakumwelewa na mmoja wa askari hao alimpiga ngumi mdomoni na kisha kumfunga pingu na kumpakia kwenye gari ndogo waliokuwa nayo na kuondoka naye.

"Wale askari walimhoji unavuta nini akawajibu ni Siger wakamwambia usitutanie hiyo ni bangi na mmoja wa wale askari alimpiga ngumi na kumfunga pingu na kuondoka Naye alisema

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justine Mesejo alidai kwamba tukio hilo bado halijaripotiwa kituo cha polisi ila alidai kwamba polisi wanafanya uchunguzi na amemtaka Palangyo pindi atakaporejea nchini afike kituo cha polisi kutoa maelezo yake ili Jeshi hilo lichukue hatua.

"Hizo taarifa nimezisikia ila tatizo hazijaripotiwa polisi wala taasisi zozote za serikali na yeye kama mtanzania anazifahamu kwahiyo hatuna uhakika kama ni kweli tukio hilo limetokea maana hajaripoti popote.

Lakini tutafatilia kama nikweli ila ajue kunasheria zitakazochukuliwa kama amefanya kuwachafua watumishi wa umma "alisema Kamanda

Hata hivyo uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba polisi mkoani hapa wameshawahoji watu kadhaa kuhusiana na tukio hilo akiwemo meneja wa Palangyo , Michael Palangyo ambaye alihojiwa kwa masaa kadhaa na kwamba baadhi ya watuhumiwa wa tukio hilo walikamatwa.

Ends..

 
PGO PGO PGO, Kamanda wa Polisi asisitize PGO izingatiwe na askari wake wanapomkamata mtuhumiwa, anapoingizwa kituoni na anapohojiwa kisha kuachiliwa kwani kwa namna hiyo itamsaidia kamanda wa polisi yoyote kuweza kufuatilia malalamiko ya raia yanapofika ktk ofisi yake.

Bila kuwepo utaratibu wa kufanya kazi kwa kutumia PGO lawama zote zitakuwa zinaliangukia jeshi la Polisi maana inaonekana askari hawataki kufuata PGO kwa sababu zao binafsi na siyo utaratibu wa jeshi la Polisi linavyotaka kuwa PGO iwaongoze ktk kutekeleza majukumu yao ikiwemo pia itatokea shutuma au malamiko basi mlolongo wa kilichotokea kitakuwepo ndani ya register, risiti, tape za kunukuu sauti na CCTV za jeshi la Polisi.

TOKA MAKTABA :

https://www.jamiiforums.com › pag...
PGO mwiba kwa maafisa wa Jeshi la Polisi, wanafanya kazi kwa ...


21 Sept 2021 — Polisi wetu wanajaribu kila kukicha kuzuia watu wasipate mahojiano na muenendo mzima wa kesi walioifungua dhidi ya Mbowe na

https://sautikubwa.org › kesi-ya-mb...
Kesi ya Mbowe: Shahidi wa 13 asema alifungua kesi kwa "hearsay"

8 Feb 2022 — (Shahidi anaipekua PGO). SHAHIDI: Kwenye PGO sioni. KIBATALA: Sasa nakuonyesha kile kifungu cha 10(3) cha Sheria ya Mwenendo wa
 
MFANYABIASHARA mtanzania na Mkazi wa Marekani na Arumeru Mkoani hapa,Ombeni Palangyo(36)amedai kutendewa unyama na askari polisi jiji la Arusha,kupigwa na kubambikiwa misokoto ya bangi wakitishia kumpa kesi ya uhujumu uchumi iwapo hata wapatia pes...
Sasahivi amsemi ni Samia ila ni Police, kipindi cha Magufuri ujinga kama huu ukitendeka ni Magufuri kawatuma,hama kweli nchi hii tenda wema huende zako,usingoje shukran
 
Back
Top Bottom