Arusha - Mbowe aandaa jeneza la CCM rasmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arusha - Mbowe aandaa jeneza la CCM rasmi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, May 6, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Umati wa wananchi waliofurika wakisikiliza hotuba za
  viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)
  kwenye uwanja wa NMC mjni Arusha jana,viongozi mbalimbali na
  wanachama wa CCM walijiunga rasmi na Chadema.

  MBOWE ASEMA MAWAZIRI 7,WABUNGE 70 WAOMBA KUJIUNGA,
  10,000 WAKABIDHIWA KADI ARUSHA

  MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuna zaidi ya wabunge 70 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameomba kujiunga na chama hicho cha upinzani.Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya NMC, Unga Ltd, jijini Arusha jana, Mbowe alisema katika orodha hiyo, wamo mawaziri saba waliotajwa katika Baraza lililotangazwa juzi na RaisJakaya Kikwete.“Sasa wanaowataja akina Ole Millya, Bananga na wengine watashangaa kusikia orodha na majina ya wana CCM watakaojiunga Chadema,” alisema Mbowe.

  Alitumia mkutano huo kuwatoa hofu wana Chadema wanaotilia shaka wimbi la viongozi na wana CCM wanaojiengua na kujiunga na chama hicho kikuu cha upinzani kuwa Chadema iko imara na hakiwezi kuhujumiwa wala kupenyezewa mamluki kama baadhi wanavyodhani.

  Mbowe alitamba kuwa ameongoza harakati za upinzani kwa zaidi ya miaka20 sasa ambayo imeanza kuzaa matunda kwa Watanzania kukiamini Chadema hivyo hawezi kukubali kuruhusu mtu yeyote yule anayetumia njia ya wazi au ya kificho kukidhoofisha.“Kuna watu walipata hofu na kunitumia hadi sms kuhoji iwapo akina Ole Millya wametumwa na Lowasa (Edward Lowasa, Mbunge wa Monduli) kuja kukipeleleza Chadema, najua baadhi mko hapa na ninawatoa hofu kuwa
  chama chetu ni taasisi imara isiyoweza kuhujumiwa na mtu au kundi la watu kwa nguvu wala mbinu yoyote,” alitamba Mbowe.Aliwataka wanaofikiri Lowassa na wengine wenye ukwasi kuweza kununua viongozi wa Chadema kujiuliza kwanini hawakuweza kufanya hivyo kipindi chote walichokitumia kukijenga chama hicho ambacho ni tishio kwa CCMna mafisadi wote nchini.

  Mbowe alitumia fursa hiyo kuponda uteuzi wa Baraza la Mawaziri akisema Rais Kikwete amevunja katiba kwa kuwateua watu ambao hawajaapishwa kuwa wabunge kushika nafasi za uwaziri.
  Licha ya kuvunja katiba kwenye uteuzi, Rais pia amekiuka kwa kuwateua Wazanzibari kwenye wizara ambazo siyo za Muungano kama Afya aliyokabidhiwa na Dk Husein Mwinyi.

  Makada wapokewa
  Waliokuwa makada wa CCM waliojiengua na kuhamia Chadema walipokelewa na wote kuahidi kutumia uzoefu, juhudi na maarifa yao kisiasa kukijenga chama chao kipya kwa kushirikiana na wanachama na viongozi
  wote.

  Ole Millya aliahidi kudhihirisha kuwa hakua mzigo CCM kama wanavyodai baadhi ya viongozi mara alipotangaza kujiunga upinzani kwa kukifanyia chama hicho kitu ambacho hakitasahaulika milele akianzia na kuipenyeza
  Chadema kwa jamii ya Wamaasai.“Vijana wengi walioko ndani ya CCM wanaishi kwa matumaini ya kupewa vyeo kama ukuu wa wilaya na nyadhifa mbalimbali badala ya kusimamia haki na ustawi wa taifa,” alisema Ole Millya

  Mila na laana kwa Ole Millya akigeuka
  Kabla ya viongozi kuanza kuhutubia, wazee wa kimila wa jamii ya Wamaasai waliendesha sala ya Mila hiyo kwa kumkalisha kwenye kigoda Ole Millya na kumpa laani iwapo atageuka na kukisaliti Chadema.“Mungu amekutuma wewe Ole Millya kuwakomboa Wamasaai kutoka kwenye utumwa waliokaa nao kwa miaka 50 kama ambavyo alimtuma Mussa kuwakomboa Waisraeli kutoka kwenye utumwa wa miaka 40 Misri. Usiwe kinyonga kwa kugeuka, angalia huu umati ulioko mbele yako,” alisema Mzee Naftali Mollel

  Kwa upande wao aliyekuwa Diwani wa Kata ya Sombetini, Alphonce Mawazo na Ally Banganga aliyekuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM waliojiunga Chadema walisema chama hicho tawala tayari imekufa na kinasubiri kuepelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kusubiri mazishi.“Wanaohoji kwanini tumetoka CCM kwanza watueleze hicho chama kilipo kwa sababu tayari kimekufa mioyoni mwa wa Watazanania,” alisema Mawazo huku akishangiliwa.

  Akihutubia mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema aliwataka wanaCCM wanaotaka kukihama chama hicho na kujiunga Chadema kufanya haraka kwasababu mlango wa ‘neema’ unakaribia kufungwa.“Kuna kipindi kinakuja siku siyo nyingi ambapo kujiunga Chadema itakuwa dili. Wanaotaka kuja na wafanye hivyo sasa kabla hatujafunga milango,” alisema Lema

  Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, alisema moto uliowashwa na Operesheni ‘Vua gamba, vaa gwanda’ ulioanzia Arusha, sasa umeanza kuenea nchi nzima akitaja matukio ya madiwani na wanachamakadhaa kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhamia Chadema.Golugwa alisema baada ya mkutano wa jana Jijini Arusha, mikutano ya Operesheni ya Movement for Change inahamia wilaya za Longido, Ngorongoro, Simanjiro na kumalizikia Monduli.

  Katika mkutano huo, Mbowe alikabidhi kadi za uanachama kwa Ole Millya, Bananga, Mawazo na viongozi kadhaa wana CCM waliojiunga Chadema ambapo kwa niaba ya wenzao.Hamasa kubwa iligubika umati uliohudhuria baada ya mwana CCM mwenye asili ya kiasia aliyejitambulisha kwa jina la Adil Dewji alipopanda jukwani kurejesha kadi ya CCM na kujiunga Chadema.

  Wengine waliojiunga Chadema kutoka CCM ni pamoja na wenyeviti kadhaa wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya za Arusha, Monduli, Arumeru, Ngorongoro na Longido ambao waliwakilishwa na Ignas Mfinanga aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Themi, jijini Arusha.
   
 2. J

  Jmushizoo Member

  #2
  May 6, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  wanachama wa CCM walijiunga ras
  MBOWE ASEMA MAWAZIRI 7,WABUNGE 70 WAOMBA KUJIUNGA,
  10,000 WAKABIDHIWA KADI ARUSHA
  [/B]

  [/QUOTE]
   
 3. J

  Jmushizoo Member

  #3
  May 6, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Karibuni sana kwenye chama makini chenye kumkomboa mtanzania toka miaka 50
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Umati huu ni dalili tosha watu wana njaa isiyo ya kawaida
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Vizuri hao 7 sio ambao wameondolewa Uwaziri
   
 6. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Uongo wa mchana, Mbowe atutajie majina ya ho Mawaziri saba-lazima itakuwa ni wale wezi.
  Hao ruksa kuuwachukua.
  CDM ilizaliwa Arusha na itafia na kuzikwa Arusha.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama anahitaji kutaja mtu, kwani Mallya angetajwa kwanza ninye wenyewe hapa mngeruka hatua zaidi ya mia kukana. Subirini kimbuka kinakuja mtakapokosa hata pa kujishikilia. Jeneza limeshaandali, kama hupendi kuingiamo, jiunge na Makamanda kwenye uwanja wa mapambano.
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  awe makini asije akashangaa yeye ndio anaingizwa kwenye hilo jeneza...there's still alot of work to do...cdm wasijione washachukua nchi...bado sana..ccm haitaondoka hivi hivi they will fight till the last drop
   
 9. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Nyie mnaosema CDM bado sana kuchukua nchi labda kama hiyo nchi mnayoisemea ninyi ni ya kwenu na wake zenu lakini kama ni hii Tz basi mjue kuwa CCM haina tena chake.

  Shardcole@Tabora1
   
 10. S

  Sir-mganah Member

  #10
  May 6, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mwambie nape kama ana ubavu aende arusha wakazipige kavukavu na lema
   
 11. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  amesema mawaziri 9 siyo 7 na wabunge 70,ebu rudia kuangalia hata clip
   
 12. h

  haki na usawa JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 476
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nadhani wenye macho na waone, wenye masikio na wasikie, wenye kunusa n wanuse, wenye muono na waone na wenye kuona mbali na waone mbali, na wazee wa Kimasai na makabila mengine waige ili kama maamluki akikengeuka tu laana imwendee na afe kwa kudhalilika maaana anawaona wanyonge wa nchi ni mazuzu na matahira. Na asiyekengeuka basi laana kwake naiwe mwiko
  NB
  Madam wengine wameachwa na wote walitakiwa kujiuzulu kama unaakili timamu uliondolewa jua waweza pia kuawa kwa faida ya wengine kwani wewe huna umuhimu kama ...........na pia ni jukumu lako kuchukua hatua na kujinusuru kama mligawana jua atakutosa na uuliwe ili ukosekane ushahidi wa kwake.
  USHAURI
  Tafakari na chukua hatua sasa
   
Loading...