Arusha: Mama mzazi amchanachana Mwanae kwa Wembe

Zapa RadioFm

Senior Member
Feb 12, 2016
112
171
Mtoto Eugen Godfrey anayesoma shule ya Msingi Engira Darasa la Pili mwenye miaka 10 (Kata ya Themi Jijini Arusha), leo amesaidiwa na Diwani wa Themi Melance Kinabo kwa Kushirikiana na Polisi wameweza kumkamata mzazi huyo kutokana na kitendo alichomfanyia mwanae.

Mzazi huyo ameweza kujulikana kwa jina la Anna Kileo anafanya kazi katika kiwanda cha Sunflag, anaishi Osterbay kata ya Ungalimited jijini Humo Arusha.

Baada ya polisi kumbana mzazi huyo amedai amefanya kitendo hicho baada ya mtoto kushindwa kwenda kuteka maji bombani.

Mpaka Mwandishi wa habari hizi anakwenda mitamboni Mama huyo wa mtoto alikua baado anashikiliwa na Polisi.
 

Attachments

  • IMG-20160216-WA0043.jpg
    IMG-20160216-WA0043.jpg
    118.2 KB · Views: 106
Duuh! kama naona vile pressure kubwa ya wembe due to small surface area,inavyosababisha majeraha na maumivu kwa mtoto.

Pole sana mtoto.
 
dah jaman mama ndo huwa mtu wa huruma lakin kitendo alichofanya kwa mwanae ni cha kikatili..
 
Hata juzi ndio somo tulilopewa kanisani
Kwahili uko sahihi kabisa.
Imagine yule dada aliyewapa wanae wawili sumu wakafariki nae akajaribu kujiua.
Au yule aliyewapa juice ya sumu then akawafukia shimoni na kuwaacha huko mpaka wakafa....
Japo nanyi mna ukatili wenu kama huu
SAMAHANI PICHA ZINAOGOPESHA
IMG-20151119-WA0022.jpg
IMG-20151119-WA0021.jpg
 
Kwahili uko sahihi kabisa.
Imagine yule dada aliyewapa wanae wawili sumu wakafariki nae akajaribu kujiua.
Au yule aliyewapa juice ya sumu then akawafukia shimoni na kuwaacha huko mpaka wakafa....
Japo nanyi mna ukatili wenu kama huu
SAMAHANI PICHA ZINAOGOPESHA
View attachment 323559 View attachment 323562
Sielewi kuhusu hili Madame B naomba uni brief ilikuwaje na wapi? mbona kichwa cha huyo mama kimepondeka hivyo na ubongo kumwagika? kujiua gani huko? na mbona kichwa cha huyo mtoto kipo wazi kama dafu au kifuu? sumu gani hiyo?
 
Mtoto kukataa kutumwa tu!

Ndio umfanyie unyama umchane chane namna hiyo?

Huyo Mama wa Mtoto akili yake haijakaa sawa.

Mtoto ni mtoto anahitaji mafunzo, ingekuwa hivyo basi mie HARUFU ningekuwa na majeraha tele, kwa kukataa kutumwa.

Maana hizo kesi udogoni kwangu zilikuwa nyingi sana, na yote sababu nlikuwa napenda sana kucheza mpira wa miguu, naweza kutwa nzima kama siku ya Jumamosi na Jumapili ni mpira tu, tena kuna mida nikiona, ni mida ya chakula, niko tayari niende mbali ili nitafutwe mida ya chakula.

Nijuavyo mimi mtoto akikataa kutumwa anatishiwa, mfano hai mimi mwenyewe nilikuwa natishiwa (kwa kipindi hiko sikujua kama nilikuwa natishiwa) ninapokataa kutumwa, natishiwa "huli chakula kwa kuwa umekataa kutumwa".

Walipogundua nikitishiwa hivyo inakuwa tiketi ya mimi kutoonekana nyumbani muda wa chakula, ikawa inatafutwa mbinu mpya.

Na mbinu kwa mtoto ni nyingi na haziishi.

Mtoto anatishiwa tu, hata huo wembe angetishiwa "wewe nitakukata vidole vyako".

Hiyo mtoto lazima atii, huyo Mama wa mtoto hakuhitaji kufika mbali kote huko
 
Back
Top Bottom