*TAARIFA-CHADEMA KANDA YA KASKAZINI*
Waziri mkuu mstaafu na Mjumbe wa kamati kuu Chadema Taifa Mhe.Edward lowassa pamoja na Waziri Mkuu mstaafu Mhe.Fredrick Sumaye wataongozana na Katibu wa kanda ya Kaskazini Mhe.Amani Golugwa na Madiwani wa Jiji la Arusha wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe.Kalist Lazaro siku ya kesho watamtembelea Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema katika Gereza la Kisongo .
Kama ingekuwa ni MIMI ningempigia simu DPP na kumwambia aweke NOLLE PROSEQUI/Serikali haina haja ya kuendelea na kesi hii.
Hapo ANGEZIMA UKAWA!
Si kwamba LEMA hajakosa bali Magufuli angekuwa amecheza KARATA ya kisiasa kubwa sana na FAIDA kwa upande wake.
Maana the more LEMA anahangaika kupata DHAMANA, ndivyo Magufuli ANAVYOUJENGA na kuupa NGUVU upinzani.
Wazungu walimfunga Mandela ili kumnyamazisha kwa miaka 27.
Ilibidi De Klerk amsamehe na kusema aruhusiwe kugombea URAIS na hatimaye akawa RAIS.
NGUVU na VITISHO havisaidii. bali ni UJANJA na HEKIMA za kisiasa ambazo ni LAZIMA Magufuli ajue kuzicheza!
Kubalansi kati ya USOMI, UTAWALA, Na more importantly kuwa MWANASISASA mjanja.
Kiasi kuwa unaweza kufanya kazi hata na yule aliyekuwa anakuombea mabaya.
Nchi ya jirani zetu. Moi wa Kenya alimfunga Odinga mara nyingi sana akijaribu kumnyamazisha.Lakini Haikumsaidia mpaka ilibidi Moi kuwa mwana siasa MWELEVU na MJANJA.
Akamwingiza katika chama chake cha KANU na kumfanya kuwa katibu mkuu.NCHI IKATULIA KIASI.
HUO NDO UJANJA wa KISIASA.
KUTUMIA NGUVU na mamlaka na vyombo vya dola mara nyingi HAKULIPI bali huzaa REBELLION/UASI na political tensions ambazo HAZINA maana na impact zake ni kubwa sana kitaifa!
Kwanza CV yetu kama taifa na ya RAIS kimataifa INAHARIBIKA sana!!!
Rais Magufuli AKIMSAMEHE Lema hatakuwa AMEPOTEZA chochote bali atakuwa amewafunga wapinzani MAGOLI.
Hata hivyo akili ni nywele kila mtu ana zake!