VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Mawakili hatutanii. Mawakili hatutishiki. Mawakili tutaamua hatma ya chama chetu-TLS Jumamosi kwa kumchagua Wakili Tundu Lissu kuwa Rais wetu. Yote yanayosemwa na kutendwa dhidi ya TLS na Lissu yanatuimarisha zaidi na kutufungua macho,masikio na fikra zetu. KUKAMATWA KWA LISSU HAKUBADILI MATOKEO HAPA ARUSHA. AJE AU ASIJE;AWEPO AU HASIWEPO, TUTAMCHAGUA.
Sasa,umuhimu wa Lissu unajidhihiri. Sasa upekee wa Lissu unajionesha bila kificho na jina lake lazidi kung'ara. Mawakili tulio wengi tuna nia,sababu,ari na wajibu wa kumchagua Lissu. Mawakili watasema kupitia sanduku la kura Jumamosi. Mawakili watautuma ujumbe kutokea hapa Arusha.
Maneno na matendo ya Waziri Mwakyembe juu ya TLS yametujenga na kutuimarisha. Tukilazimishwa kuwa chama cha siasa,mgombea wetu wa Urais atakuwa Tundu Lissu. Kwasasa mtu huyu hakwepeki. Kwasasa mtu huyu hahujumiki. Kwasasa mtu huyu hazuiliki kuwa Rais wa TLS. Asante Waziri Mwakyembe na Serikali nzima kwa kututangaza na hata 'kutushangaza'.
Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha kumchagua Lissu kuwa Rais wa TLS)