ARUSHA: Kinara biashara meno ya tembo anaswa

ARUSHA: Kinara biashara meno ya tembo anaswa

Twilumba

Platinum Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
13,472
Reaction score
16,177
Nimekutana nayo kwenye Gazeti la mwananchi;

Endendelea......


Arusha
Kikosi kazi Maalumu cha Kupambana na Ujangili, kimemtia mbaroni mtu anayedaiwa ni jangili hatari na sugu wa muda mrefu, ana mtandao mkubwa wa ujangili ndani na nje ya nchi na ndiye mnunuzi mkuu na mpangaji wa mipango yote ya ujangili,"alisema Kijazi.

Vyanzo huru vya habari ndani ya Jeshi la Polisi, vilieleza kuwa baadhi ya polisi wasio waaminifu walikuwa wakivujisha siri za mikakati ya kumkamata, hivyo kudhoofisha jitihada za kumnasa kinara huyo.

"Huyo jamaa ana pesa, kuna wenzetu walikuwa kwenye payroll (wanalipwa). Kwa hiyo mnaambiwa yuko hapa, mkienda mnakuta ametoroka, lakini walipogundulika ndiyo akakamatwa,"kilidokeza chanzo chetu.

Vyanzo hivyo vimedai kuwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na msukumo wa tuhuma zilizoibuliwa bungeni na kambi rasmi ya upinzani Aprili 29 mwaka huu kwa Wizara ya Maliasili na Utalii na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, baada ya kukamatwa, mtuhumiwa huyo alijaribu kuishawishi timu ya maofisa waliomkamata awape rushwa ya Sh10 milioni ili wamwachie, atorokewa kuwa kiongozi wa mtandao wa ujangili jijini Arusha aliyekuwa akisakwa kwa miezi miwili mfululizo.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa ndiye anayepanga mipango yote ya ujangili katika hifadhi sita za wanyamapori zilizopo Kanda ya Kaskazini, kununua meno yote zya tembo na kutafuta masoko nje ya nchi.

Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana, zilisema kuwa mtuhumiwa huyo alitiwa mbaroni Jumatatu iliyopita eneo la Sakina jijini Arusha na kikosi kazi hicho cha kupambana na ujangili.

Kikosi kazi hicho kinaundwa na maofisa wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(Tanapa), Kikosi cha Kupambana na Ujangili na Askari kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi (RCO) Mkoa wa Arusha.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi, jana alilithibitishia Mwananchi Jumamosi kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo akimwelezea kuwa ni jangili hatari wa kimataifa, waliyekuwa wakimsaka kwa muda mrefu.

Hata hivyo, kikosi kazi hicho, kilikataa kupokea rushwa hiyo na kumfikisha kituo cha polisi mtuhumiwa na sasa anashikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi mjini Arusha akihojiwa.

Habari hizo zinadai kuwa mtuhumiwa huyo (jina tunalo) ndiye aliyefanikiwa kuwatoroka askari wa Tanapa Januari mwaka huu, walipolikamata gari la JWTZ likiwa na meno ya tembo.

Chanzo:
Gazeti la Mwananchi!

 
Sasa meli za kinana ztasafirisha nini?
Anguko kubwa kwa Katibu Mkuu wa CCM kibiashara baada ya his "Right hand Man" kutiwa mbaroni.
 
Kinara anajulikana haiitaji jwtz kumnasa yupo lumumba wala sio arusha.
 
Twilumba habari hii ipo humu tangu tar 9 mwezi huu.

Yaelekea umekuwa mtoro humu!
 
Last edited by a moderator:
mhhh!alikua anatafutwa kwa miezi miwili,mara alikua anatafutwa kwa muda mrefu!tumeshawazoea,kwasababu kila kitu ni upepo,sahizi wanatengeneza mazingira ya upepo kupita!same old shit
 
Hana jina?!

Hii serikali inataka kutufanya mazuzu hivi kweli unaweza kumuokoa Kinana(Katibu Mkuu wa CCM)kwenye hii kashfa kwa taarifa kama hii!!

Mwananchi nao siku hizi limekuwa gazeti la ovyo kabisa!

Ujinga huu!.
 
CCM wanatumia kila mbinu kujisafisha. Kinana keshajamba lazima kinuke, no way out.
 
CCM kwa kutunga tunga mambo hawajambo. Sasa kama kakamatwa mbona hawamtaji maana keshakamatw? Wanaficha so what? Huu ni uongo mtupu. Kinana ndiye anayeratibu biashara hiyo na kusafirisha wasomali hapa Tanzania. Kwa nini hawamkamati?
 
Kesho atapata dhamana, keshokutwa ataachiwa huru na tutaambiwa kesi haina mashiko.
 
Hivi ile kesi ya wale TWIGA waliosafirishwa wakiwa hai imeishia wapi vile?!
 
Hivi ile kesi ya wale TWIGA waliosafirishwa wakiwa hai imeishia wapi vile?!
Hiyo ya TWIGA ilikua upepo tu, huoni ulipita?Kumbe safari ya kwenda kuwapa pole wahanga wa bomu la Ola City ilikua ya mafanikio makubwa, naombeni mnikumbushe viongozi gani walikwenda Ar last week
 
Mkiambiwa nchi ilishauzwa bila watz kujijua mnabwatuka,hii nchi inaliwa sana hasa vigogo/viongozi,usipime...
 
mhhh!alikua anatafutwa kwa miezi miwili,mara alikua anatafutwa kwa muda mrefu!tumeshawazoea,kwasababu kila kitu ni upepo,sahizi wanatengeneza mazingira ya upepo kupita!same old shit

Ni jangili wa kimataifa kwa vipi? Amefanya ujangili katika nchi zipi au mnamkweza tu?
 
mhhh!alikua anatafutwa kwa miezi miwili,mara alikua anatafutwa kwa muda mrefu!tumeshawazoea,kwasababu kila kitu ni upepo,sahizi wanatengeneza mazingira ya upepo kupita!same old shit

Ni jangili wa kimataifa kwa vipi? Amefanya ujangili katika nchi zipi au mnamkweza tu na Mkurugenzi wa TANAPA na anatoa taarifa za kipolisi?
 
Back
Top Bottom