kwedikwazu
Member
- Dec 17, 2016
- 18
- 15
Kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaofaulu kidato na Nne na namna ambavyo shule zilizopo zinavyopokea idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha Tano Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro amemuagiza Mkurugezi Ndg. Athumani Kihamia kuhakikisha anaongeza shule za Kidato cha Tano kufikis mwaka 2018.
Daqaro ameyasema hayo wakati akipokea taarifa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Tano kuanzia July mwaka huu na kueleza kuwa wanafunzi waliochaguliwa ni 578 kati ya hayo wasichana ni 322 huku wavulana wakiwa 256.
Aidha amempongezs Mkurugenzi Kihamia pamoja na Menejinent kwa kusimamia Upatikanaji wa Elimu bora kwa wanafunzi mpaka kupelekea kiwango cha ufaulu kuongezeka.
Naye Mkurugenzi wa Jiji Ndg. Athumani Kihamia amesema amepokea agizo hilo na atatekeleza haraka iwezekanavyo kutokana na kuwekwa kwenye bajeti itakayoanza July 2017 na shule hizo ni Korona(bweni) na Suye(Kutwa).
Ameongeza kuwa ataendelea kusimamia maslah ya Walimu ikiwa ni pamoja na kulipa Stahiki zao kwa wakati na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ili waweze kuwa na moyo zaidi ya kufundisha kwa weledi wanafunzi wanaosoma katika Jiji hili.