GE2025 Arusha: CCM yatangaza wagombea 160, Olasiti na Ererai kusubiri uamuzi wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

GE2025 Arusha: CCM yatangaza wagombea 160, Olasiti na Ererai kusubiri uamuzi wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha kimeingia katika hatua mpya ya mchakato wa uchaguzi, huku hali ya kisiasa ikichukua sura mpya baada ya kutangazwa kwa majina ya wagombea 160 kutoka Kata mbalimbali watakaowania nafasi kwa tiketi ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Arusha, Saipulani Ramsey, amesema kuwa mchakato wa kuchuja na kupitisha majina umekamilika rasmi, na kuwa majina ya wagombea hao yameidhinishwa kwa ajili ya kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi ujao, Oktoba 2025

Hata hivyo, hali si shwari kwa baadhi ya waliokata rufaa kupinga mchujo wa awali, baada ya taarifa rasmi kuthibitisha kuwa rufaa zao zimefutiliwa mbali na kwamba Kata ya Olasiti na Tarafa ya Ererai "Tunasubiri uhakiki wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na tutatangaza aliyepewa ridhaa hiyo."

 
Back
Top Bottom