Uchaguzi 2020 Arusha bado inamhitaji Godbless Lema?

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kuna taarifa kwamba Arusha imejengwa kwa kasi kubwa ikiwemo miundo mbinu ya barabara za Lami ,Shule na Zahanati ikiwa ni mkakati wa maksudi wa kumng'oa Mbunge wa Upinzani Godbless Lema.

Wataalamu wa kuchonga vibarazani,vijiwe vya kahawa na wanasiasa wanadai kwamba nguvu kubwa inayotumika na serikali jijini Arusha ya kujenga miradi mikubwa ukiwemo mradi wa maji wa bilioni 525 ni ishara tosha kwamba Lema hatakiwewi tena .

Lakini wanasiasa wanadai kwamba bila Lema jiji la Arusha lisingejengwa hivi .ukweli wa hii story ukoje wadauuu?????na Arusha bado inamhitaji Lema?

Mara nyingi Lema pale anapokuwa akiulizwa kuwa umewafanyia nini wanaarusha hujibu kuwa nimefanikiwa kuwajengea ujasiri na kuwatoa woga jambo ambalo amefanikiwa kutokana na sifa yake kuu ya ushawishi wa haraka pale anapokuwa akizungumza na wananchi.

images%20(4).jpeg
 
Mtafutieni lema kazi acheni kumdanganya atadhalilika mwaka huu
 
Nawaonea sana huruma wabunge watakaopoteza majimbo yao maana kwa mikopo mikubwa waliyochukua watabaki kukimbizana na watu wa mabenki.
 
Ukweli usiopingika ni kweli bila lema arusha isingejengeka hivyo linganisha na majimbo yanayoongozwa na ccm na ndio kazi mojawapo ya mbunge kusimamia maendeleo ya jimbo lake mbunge yeyote hana fungu la kufanya maendeleo bali ni kulazimisha sera zilotangazwa na chama kilichoshika dola zinatekelezwa
 
Back
Top Bottom