ARUMERU UKITAJWA TU MIEZI TISA MAHABUSU,

ARUMERU UKITAJWA TU MIEZI TISA MAHABUSU,

PRINCEd

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2015
Posts
862
Reaction score
625
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Jerry Muro amesema mtuhumiwa yoyote atakayetajwa kuhusika na kumpa mimba mwanafunzi (mtoto) katika wilaya hiyo hatapewa dhamana na badala yake atakaa mahabusu mpaka Binti huyo atakapojifungua

Amesema akijifungua ndipo atapimwa DNA kuona kama yule mtoto ni wake ndio hatua zingine zifuate, na kuongeza kuwa hilo litawahusu wanaume wote watakaotajwa bila kujali ni kweli ama wamesingiziwa

Unakubalina naye?
Sheria zinasemaje?
 
Hivi hii serikali inabuni sheria tofauti na za bunge? Maana tunashuhudia matamko yenye viashiria vya udikteta.

Tufuate sheria mama ambayo ni katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Kwamba akitajwa na yeye awekwe kwanza akisubiri mtoto ajifungue,bas hapo sawa
 
Back
Top Bottom