Wazee wana haki ya kuchagua kama wameelimishwa faida ya kuchagua kwao.
Lakini kwa kuwa hawakuipata elimu hiyo ambayo ingewaletea faida ya kuchagua kwao, vijana waendelee na huo mkakati ili ukombozi upatikane. hiyo tunaweza kuiita kama mpango wa dharura, kwani kwa mpango wa muda mrefu itatakiwa wazee kuelimishwa ushiriki wao wa kupiga kura.
wazee tulionao kwa asilimia kubwa wamekuwa wakidanganywa kwa vitu vidogo, ama kutishiwa kwa uongo kuwa ccm ni chama kilicholeta uhuru, na kamwe wasithubutu kukipigia kura chama kingine.
Ukombozi wa kweli nchi hii haujawahi kupatikana, hivyo ni jukumu la vijana kuhakikisha ukombozi wa nchi hii unapatikana kwa gharama yoyote, maadam iwe ya amani. vile vile vijana wana jukumu kubwa sana kuwaelemisha wazee wetu katika kushiriki kwenye chaguzi zozote zile. kura moja ina thamani kubwa sana.