Hivi Sherehe ya kupitishwa kwa jina la Siyoi inafanyikia wapi?
Kwa hapo kura ni kuchagua kati ya Uadilifu na uongozi uliotukuka kwa upande mmoja au ushoga na urithi wa uongozi wa mambo ya kibunge ki-ukoo kwa upande mwingine. Vijana wenzetu sasa tuingieni msituni rasmi kazi ianze mpaka kieleweke!!!
BAWACHA tungependa kuona cheche zenu zaidi na zaidi kama ambavyo wafanyavyo BAVICHA kila mahali penye uchaguzi; sote tucheze kama timu moja ili kuwarahisishia kazi uongozi wa juu kuleta ufanisi Arumeru Mashariki.
naomba kujua wadau wamezidiana kwa kura ngapi....nassar amepata ngapi kati ya ngapi na sumarry amepata ngapi kati ya ngapi?Baada ya vyama hivi vikubwa kupitisha majina ya wagombea wao, macho na masikio ya wananchi yapo kati ya wagombea wawili kutoka CCM na CHADEMA.
Joshua Nassari na Siyoi Summari.
Pamoja na kuwa kulikuwa na pingamizi kwa jina la Siyoi Summari kutokutaka kupitishwa na CC ya CCM kutokana na tuhuma za Rushwa zilizokuwa zinamkabili, sasa imedhihirika kwamba kumbe Mkono wa aliyekuwa anatuhumiwa kutoa rushwa kwenye kura za maoni (EL) ndiye mmiliki na ana mkono mrefu unaoweza hata kufikia CC ya CCM.
Siasa ya Tanzania jama!
naomba kujua wadau wamezidiana kwa kura ngapi....nassar amepata ngapi kati ya ngapi na sumarry amepata ngapi kati ya ngapi?
siasa mchezo mchafu
siasa mchezo mchafu
Feedback, nipo nimejinyamazia kimya!. Ila pia nimegundua ni wanabodi wachache sana huwa wanaukubali ukweli halisi!, wengi zaidi huogopa ukweli halisi na badala yake kung'ang'ania ukweli wa kujifariji nafsi zao kwa kujipa matumaini ya uwongo na mwisho wa siku huishia kulia lia tuu!.Pasco uko wapi kwa hili?....
Feedback, nipo nimejinyamazia kimya!. Ila pia nimegundua ni wanabodi wachache sana huwa wanaukubali ukweli halisi!, wengi zaidi huogopa ukweli halisi na badala yake kung'ang'ania ukweli wa kujifariji nafsi zao kwa kujipa matumaini ya uwongo na mwisho wa siku huishia kulia lia tuu!.
Baada ya kupitishwa Sioi, uchaguzi Arumeru ndio umemalizika!. Kinachoendelea sasa ni kwa NEC kukamilisha tuu taratibu kukidhi matakwa ya kidemokrasia kusubiria kumtangaza rasmi!.
Wenye akili wataisoma hii post na kujinyamazia kusubiria April 2!. Ving'ang'anizi wa maubishi mtaanza kubisha na kuendelea kujifariji kuwa mtu yule yule toka chama kile kile aliyeshindwa na mahututi kitandani, sasa anaweza kushindana na mwana mfalme wa mtu yule yule aliyewashinda mwanzo na akashinda!.
Wengi wanategemea zaidi kura za chuki za wana CCM dhidi ya siasa za uchifu, usultani na ufalme za CCM kwa mtoto kumrithi baba yake bila kutambua asili ya Wameru ni ufalme wa koo fulani fulani!. Jerry alikuwa ni mfalme wao na Sioi ndiye mwana mfalume!.
Kwa wapenzi wa demokrasia ya kweli mtanisamehe sana kwa kuwadondolea ukweli mchungu!. Ili kuupata ukombozi wa kweli, lazima tukubali kukimeza "the bitter pill"- Sioi ndiye Mbunge Mteule wa Arumeru akisubiri kuapishwa!.
Pasco (wa jf).