Arumeru biashara imeisha Vipi arusha mjini na Hatma ya CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arumeru biashara imeisha Vipi arusha mjini na Hatma ya CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicholas, Apr 12, 2012.

 1. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi wa Arumeru umeisha vyama vijogoo vilichuana kwa kila mbinu na CDM wakabana hadi pumzi ya mwisho. CCM waliingia kwa Nguvu kubwa iliyokosa ufanisi kutokana Upepo wa siasa,mbinu za wa CDM na mpasuko UNAOSEMWA.Hatujui km huo mpasuko ulizaa timu iliyoshindwa au iliyoshinda ktk CCM,ingawa kwa Ujumla CDM walishinda timu zote.
  SWALI MUHIMU HAPA NI JE kama Rufaa ya lema ita bounce?CCM wataingia km timu moja au wataamua kupiga mechi tena kati yao (katika Uteuzi na Uchaguzi ) kwa timu zilizopo ktk CCM km mpasuko unaovuma ktk minong`ono ni wa kweli?
  Kama Kweli timu za ndani ya CCM zipo, nani atakuwa tayari ipa ushindi timu ingine?Ushind ambao utaleta adui timu pinzani kuelekea uteuzi wa urais 2015?
  Kama kweli timu zipo na kila Mbunge ni faida kwa kambi husika ndani ya CCM na uchaguzi mwingine ktk jimbo ni kuigawa CCM zaidi. Ni CCM walikuwa na haja ya kufungua Kesi iliyomtoa Lema ktk ubunge?Chadema tayari wana ushawishi kwa watu wengi, wanaweza chukua kura za wana CCM waliopotea na kuchanganyikiwa na habari nyingi wanazozisikia ktk kambi za chama na hali ya maisha,wapo wana CCM wanaoona huruma kwa Lema.Na wapo wana CCM wanaopata mashinikizo toka kila pande hata kwa watoto wadogo waliopagawa na CDM.Mwanangu mdogo (2yrs)naye kila asubuhi ananikurupusha mapema anataka PEOPLE`s POWER ANTHEM, na nikichelewa ondoka kabla ya uji anataka tena Peoples Power ipigwe,bila tafuta cha kumdanganya anataka tuanze cheza na kazini sitoweza kwenda.
  NADHANI KM KWELI serikali iliingilia mahakama basi iendelee ingilia ili rufaa ya Lema ipite.Otherwise watajibomoa wenyewe.Km wana Kambi basi ni dhahiri kambia itakayomruhusu mwingine inakuwa itakuwa iajiua, na kuna uwezekano waliodhihakiwa meru nao wakawadhihaki wengine na tayari chama hapa hakina mashiko makubwa.Bora wakawekeze nguvu kule walipo nazo.Kuaibika tena Arusha kutawaamsha wanakondoo wa ngome za CCM hasa watakapowasikia wabunge wao wakiumbuliwa majukwaani.CCM pia watajikuta wanaishiwa na waendesha kampeni, kwani tayari Arumeru imewachafua wengi na waliobaki wakichemsha baishara ya CCM itakuwa over.Kila mtu itabidi ajinadi kivyake kwani kila mtu anaweza jiona yeye ana afadhali kuliko mwingine.
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi wowote utaofanyika saizi ukitoa Zanzabar unatija kubwa kwa CDM kuliko CCM kwa upande wa ujenzi wa chama.

  Ni bora CCM ingefanya hila zake mahakama imrudishie ubunge Lema kama ilivyofanya kabla ya hukumu ili kunusuru chama kisizidi kubomoka.
   
 3. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nimempenda huyo mwanao anayekuamsha na Peoples power anthem
   
 4. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Na anakomaa haswa.Kichwani nilikuwa na maswali mengi..ila nimepunguza maswali baada ya kuona ni watu wengi na watoto wengi wanavutiwa na huo wimbo.Kuna mitaa vitoto vina bendera za CDM na wanawazomea CCM.
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ukitaka kujua ilivyo ngumu kusimamia walevi jaribu kuanziaha timu ya mpira ya walevi.
   
 6. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  JF inasomwa na ujumbe unafanyiwa kazi sana hata kwa style ya kuiba agenda. Ukweli ni kuwa tusipovisaidia vyama vya kisiasa, taasisi za dini na hata raia.serikali itabaki ikiwa imehehuka na watafanya mambo ya kushangaza.
  Chadema wanawatembeza CCM na Serikali kwa vidole (rais alikiri kuwa chadema wanataka wasipate muda wa kutimiza agenda )na mawazo yao mapya na ya mfululizo,na vitisho vya kuchukua kila jimbo linalokuwa wazi.Sidhani km serikali inaweza tena fanya mambo kwa uangalifu.Kwa wanaojua last minute works zinavyokuwa ngumu.asiyeamini awaulize wabunge walioingia kwa hela,wanaoumia serikali inavyobadili nia ya kuwapa rushwa ktk nyongeza ya posho, halafu hawana hakika km wapo kambi sahihi itakayoweza wateua tena, halafu wakakutane na CHADEMA-tishio la wazi.<br>


  CCM wamekuwa wakitishiana mara waonapo mwenzao akitembea maeneo ya jimbo,sasa CDM hawaambiliki na hawatabiriki popote.Hata mahali hawajahi kuwepo wakifika wana adapt.Kwa mbunge wa CCM anahitaji hela kupita ktk uteuzi wa ndani, halafu hela nyingi tena za kuweza kimbizana na mziki wa CDM.Its too much.Anayebisha amuulize hata mtoto wa mkulima kila baada ya muda anajisikiaje CDM wakipita jimboni kwake?utaona kujiamini kunapungua...
  Tunahitaji kusaidia maendeleo ktk maeneo yetu.Sasa hivi wabunge na mawaziri wanaongea wakitembea, km vile mtu nayeota akitembea.So JF mzidishe dozi ya kuelimisha watu kujiletea maendeleo wenyewe ,huku wakijiandaa wachapa fimbo ktk kura.
  Msichoke kieleimisha chama tawala pale wanapotaka fanya maamuzi ya kipuuzi wakidhani kuwa wana kinga za plisi bongo, au chama chao kitakaa milele kikiwalinda wasikutwe na sheria.
   
 7. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Vijana CDM wanaomba Mzee wa Mvi agombee urais kuoitia CCM ili wakachukue jimbo, huku wakimlipua ktk urais
   
 8. L

  Laban Boaz Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee wa mvi agombee asigombee jimbo lake liko njiani kuelekea cdm.
   
 9. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  ha ha..mtakuwa mmemshika simba sharubu km atakuwa amebaki jimboni.....jamaa msimu undermine hat akm mmempiga bao mara 2 Atown,na Arumeru.teh teh .Tuangalie uchangaji karata wake.Jamaa yupo smart kiasi chake,anaweza waweka ccm wote upside down anytime akitaka.Uliza Arumeru.
   
Loading...