Arudishiwa mahari muda mchache kabla ya kufunga ndoa

SDG

JF-Expert Member
Feb 28, 2017
7,631
8,072
Hii imetokea kwa kijana mwenzetu,

Alimchumbia binti akapeleka posa kisha mahari. Taratibu za ndoa zikaanza kwa pande zote mbili, yaani upande wa bwana harusi na bi harusi.

Siku ya siku ikafika ili ndoa ifungwe, upande wa mume wakajiandaa ili waende kuoa, hapo wakiwa wameshajipamba, wamepaka piko, hina na vikorombwezo vyote, kabla ya kutoka nyumbani kwenda kubeba jiko. Unakuja ujumbe kuwa ndoa imekufa na mahari yao imerudishwa.

Bado haijawekwa wazi sababu za kubatilishwa kwa ndoa dakika za lala salama, ila huenda wana familia wanajua.

Tanbih picha hiyo haihusiani na stori husika
_20170526_100101.JPG
 
Nini chanzo cha mahari kurudishwa?
Hakikuwekwa wazi, japo kuna sababu ilitolewa lakini ilionekana haina UZITO.
Inasemwa kwamba Baba Mkwe mtarajiwa (baba wa mke) alimwomba kijana (bwana harus mtarajiwa) aende mara moja akamuone,lakini bwana harus mtarajiwa alisema kuwa ameshikwa na majukumu so wataonana siku ya HARUSI,jambo hilo INASEMWA lilimkera BABA MKWE.
 
Hatari sana. Ngumu kumeza hiyo
Hapa kuna cha kujifunza.
Kwamba mke/mume au ndoa kwa ujumla hupangwa na Mwenyezimungu.
Lakini pia wapo waliotendwa,wapo walioachwa wakalia,kumbe hayo ni mambo madogo sana,fikiria ndoa inavunjwa mda mchache kabla ya kufanyika na protocals zote zilifanyika.Jamaa au Bibie alikuwa kwenye hali gani?Walishajiandaa kwa kila kitu,halaf ndoto inakatizwa ghafla.

Tuendelee kumuomba Mungu tu kww kila mtihani anaotupa na kumshukuru

Pamoja na hayo,maisha lazima yaendelee hakuna kujilizaliza hapo,maisha lazima yasonge hasa kwa mwanaume ambaye ndo aliathirika zaidi
 
Hii sio hadithi.
Hadithi huwa na mwanzo maalum.
"HADITHI HADITHI"
Fasihi simulizi kidato cha II
Story inayoisha bila mantiki inakuwa ni hadithi nayompa nafasi msomaji kujifunza chochote kadiri ya uelewa wake
 
Back
Top Bottom