Artificial Intelligence: Yajayo yanatisha!

Artificial Intelligence: Yajayo yanatisha!

AI haiwezi kureplace programmers...

Ni hofu isokuwa na maana.

Ni lazima muhusika ajue coding kwanza ndipo AI impatie muhusika msaada kulingana na shida yake...
 
Kama kuna project moja naifatilia ndiyo ipo kwenye development, jamaa wanatengeneza cooking pots zinakuwa integrated na AI & Camera. Maana yake unaweza kuwa na watoto nyumbani ukapika chakula kupitia simu kikaiva wao wanaenda kupakua tu.
Mmh, kwisha habari yetu
 
Hakuna umatatani wowote wa kazi, kwahiyo wala usiogope na uendelee kujifunza namna ya kuitumia kwa usahihi kwa maana hiyo ni tool ya kurahisisha kazi.

Binafsi tangu CHATGPT iwepo nimekua sishindi sana kule stack overflow au GitHub ni kuweka maelezo na kusaidiwa directly.

Na ndani ya hii miezi miwili kuna project naifanya ya reactjs, firebase na MySQL, ndio nimejifunza kwamba haiwezi kureplace kazi ila inarahisisha kazi.

Kwa maana kwa vilanding pages labda Kila mtu anaweza kutengeneza kupitia hizo AI ila kwa project serious ni lazima ujue unachokifanya ndio uweze kwenda nazo sawa hizo AI.

Kuna makosa mengi sana zinafanya, kwa maana unaweza ukauliza swali au ukataka itengeneze logic fulani ila majibu yakawa ndivyo sivyo kwa mara ya kwanza ila mara ya pili ndio inaweza kugenerate code yenye kumake sense.

Kwahiyo kama haujui unachofanya na haujui namna sahihi ya kutoa maelezo ya namna unavyotaka logic itengeneze unaweza ukashtukia unakua na mfumo ambao kimuoneiano ni sahihi ila kiufanisi ikawa na upumbavu mtupu.
Huu ni uhalisia 💯
 
Back
Top Bottom