Argentina yaizamisha meli ya Uchina Saa 3 zilizopita

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,369
8,072
ImageUploadedByJamiiForums1458133931.596439.jpg

Meli ya China iliozamishwa na walinzi wa pwani ya Argentina

Walinzi wa pwani nchini Argentina wamesema kuwa wameifukuza na kuizamisha boti moja ya Uchina iliokuwa ikivua samaki kinyume cha sheria katika maji ya taifa hilo siku ya Jumatatu.
Katika taarifa ,walinzi hao wa pwani wamesema kuwa mojawapo ya boti hizo iliionya boti hiyo ya Lu Yan Yuan Yu 010 kwa kuifyatulia risasi iliopukwa ikielekea katika maji ya kimataifa.
Walinzi hao wanasema kwamba waliionya kupitia kipaza sauti.
Wafanyikazi wote 32 wa boti hiyo waliokolewa.
Uchina imeonyesha wasiwasi wake kuhusu kuzamishwa kwa boti hiyo.
Msemaji wa wizara ya kigeni wa taifa hilo Lu Kang alisema katika taarifa kwamba Beijing imewasilisha wawakilishi wake nchini Argentina ikitaka uchunguzi kamili kufanywa kuhusiana na kisa hicho.
Uvuvi haramu ni tatizo la kawaida katika eneo hilo.
Mara nyingi boti zinazopatikana zikifanya uovu huo hutafuta mbinu za kugongana na walinzi hao na hivyobasi kuhatarisha sio maisha ya wafanyikazi wake bali hata yale ya walinzi hao wa pwani,ambao waliamrishwa kuifyatulia risasi meli hiyo,taarifa hiyo ya walinzi wa pwani hiyo walizungumza kwa lugha ya kihispania.
Hatua hiyo inajiri licha ya uhusiano wa Argentina na Uchina kuimarika katika siku za hivi karibuni.
 
Mhh wachina bhana..hata argentina wanafika umbali wote ule, duh njaa hii itawamaliza
 
Wangewazamisha na wao
Tuliwachekea sana hapa kwetu ona walichotufanyia
 
Wanaizamishaje sasa meli??? Wanaitoboa toboa ama vipi mana nimeshikwa bumbuazi hapa
 
Ukimkalibisha mchina nyumbani kwako ni sawa na kumkalibisha panya kwamaana lazima atakualibia kila kitu.
 
Ilikuwa yao,na hadi sasa. Ni yao,maana tuailipa senti hadi senti,na samaki wake,na nyavu zao,na Muda wao.
 
Wachina wanakera kitu kimoja tu hawana ustaarabu hata kidogo!! Yaani wakipita ujue wameharibu kila kitu, wapangishie nyumba ndiyo utaamini nisemayo!! Na hapo si ajabu walikuwa wanavua kiharamu haramu
WANAMALIZA TEMBO WETU NA SISI, KWA UJINGA, TUMEFUKIA VICHWA MCHANGANI KAMA MIMBUNI! NI SHIDAA!
 
Back
Top Bottom