Are spies made or born?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Special thread for discussing espionage business and other closely related issues:

Bila shaka wote mu wazima wa afya humu JF.

Kama ambavyo heading inavyojielezea hapo juu ni swali nililokuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sasa kama uwezo wa hawa watu (spies/intelligence officers) huwa ni wa mafunzo au wanazaliwa wakiwa tayari ni spies?

Ninawasilisha mjadala.
==========

Mchango kutoka kwa mdau
 
Katika uasilia, angalia mfano wa wadudu wadogo mfano sisimizi na jamii yake, nyuki nk.

Utajifunza kuwa askari huzaliwa.

Ukiwa na bahati ukaonwa na kutimiza vigezo vingine utapatiwa mafunzo...

Tunao 'askari' wengi mitaani lakini hawakubahatika kuonwa au kupata mafunzo ama vigezo havikukamilika lakini ikiwaona tu utahisi wangefaa kazi ya uaskari...

Kwa 'spies' vivyo hivyo lakini lazima uwe 'flexible' na 'little more intelligent'. Vyoye hivi ni kwa kuzaliwa, mafunzo huwaongezea uweledi...

Kujibu swali, '...spies are born and made...'

However: Katika nchi corrupt kuna uwezekano wa kukuta spies wasiostahili, yaani ambao IQ zao zipo chini sana...
 
Nadhani huwa kunakuwa na vyuo vya kuwasuka hawa jamaa..sasa kama hao wa secondary wanakuwa wapitaje katika hivi vyuo?
Wanajua wao wanawatrain muda gani, mtu unaandaliwa kufanya kitu fulani mapema, ndio maana form three unachagua science, form five unachukua PCB ili Chuo ukasomee Udaktari, uwezi ukachukua HGL form five Chuo ukataka ukasomee Udaktari, maandalizi ni mapema, ingawa kwa hawa watu ni wao wanaokuappriciate na kukuingiza humo taratiibu mpaka unaiva na kuwafaa, sio unajiingiza mwenyewe, unaamua kusomea mwenyewe au kama unavyoenda kuomba kazi Bank, no, unaweza ukawa hata mtu mwenye Masters, wasikufagilie, kwa kuwa hauwafai, lakini wakamtrain form four leaver akawafaa, but unafuatiliwa muda sana mpaka kuingizwa huku, hawakurupuki, yawezekana anayekufuatilia ni mwanafunzi mwenzako ama Mwalimu wako ambaye naye yumo tayari
 

Sasa nimeanza kupata picha kwa mbaaaali lakini bado ninajiuliza how do they get to train teenagers? Au hawa wanafunzi wanakuwa recruited unknowingly?
 

Thanks mkuu nimepata uelewa kidogo hapo!
 
Mkuu wale jamaa kwa nchi za wenzetu huwa wanazaliwa wakiwa na baadhi ya attributes/tabia fulani hivi kisha wanaongezewa tradecraft/ujuzi wa kimafunzo...baada ya hapo weeee wanakuwa ni moto wa kuotea mbali...!

Daaah kweli balaaa..nimekusoma mkuu!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…