Ardhi yenye mchanga mwingi, inafaa kujenga nyumba ya kuishi?

NZURI PESA

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
5,958
2,951
Wakuu naomba ushauri toka kwa wataalam wa ujenzi kuhusu ujenzi wa nyumba kwenye ardhi yenye mchanga mwingi. Je aina hii ya ardhi inafaa kwa ujenzi wa nyumba ya kuishi?

Natanguliza shukran.
 
Sehemu zenye udongo wa kichanga ni nzuri sana kwa ujenzi na nyumba huwa zinakuwa stable si kama kwenye udongo mfinyanzi ambapo utalazimika kuingia gharama za kuchimba msingi wa kina kirefu. Kwenye sehemu za mchanga ni nadra sana kukuta nyumba ina nyufa kama sehemu za mfinyazi. Udongo wa mfinyanzi una kawaida ya kutitia.
 
Inafaa ila ina hitaji msingi wa maana.. hivyo lazima pochi imetuna haswa..!

Ingawa bado inategemeana na kiwango cha mchanga, kuna kiwango kikizidi hautaruhusiwa kujenga hilo eneo.
 
ahsante kwa majibu mkuu
 
Inafaa ila ina hitaji msingi wa maana.. hivyo lazima pochi imetuna haswa..!

Ingawa bado inategemeana na kiwango cha mchanga, kuna kiwango kikizidi hautaruhusiwa kujenga hilo eneo.
sawa mkuu eneo hili lina mchanga mwingi hadi wenyeji huuza kwa wenye matipa lakini
mchanga wake unastawi kila kitu je hapo vipi mkuu
 
kama ni hivyo mkuu..!
Hakikisha unapesa ya kuzidi ili ujenge hapo, maana kila sehemu unaweza kujenga nyumba kama hauna pesa za mawazo..
tumeona nyumba zimejengwa majini, sembuse kwenye mchanga mwingi.
ila kama hauna pesa za kutosha na unataka kujenga ya kawaida acha. Fanya jambo mbadala.. aidha tafuta sehemu nyingine
 
Wakuu naomba ushauri toka kwa wataalam wa ujenzi kuhusu ujenzi wa nyumba kwenye ardhi yenye mchanga mwingi. Je aina hii ya ardhi inafaa kwa ujenzi wa nyumba ya kuishi?

Natanguliza shukran.

Nyumba popote inajengwa iwe kwenye maji,miamba,mchanga,kwenye tope au popote.Ni pesa yako tu.Jangwani nchi za kiarabu ni mchanga mtupu watu wamejenga majumba ya ajabu.nI HELA yako tu mkuu
 
poa na ahsante tatizo sio mpunga mkuu ni fundi tu wakuniridhisha kuwa.hata jangwani kama saudia penye mchanga mwingi itajengwa tu
 
Tena hiyo ndio nzuri hasa, maana mchanga huwa hauvimbi na kusinyaa kulingana na majira (mvua/kiangazi) kama ufanyavyo udongo wa mfinyanzi. Maan kuvimba na kusinyaa kwa udongo husababisha nyufa kwenye kuta, na ndio maana watu huweka 'blinding layer' ya mchanga kwenye msingi ili kuepukana na hali hii.
 
Inafaa ila ina hitaji msingi wa maana.. hivyo lazima pochi imetuna haswa..!

Ingawa bado inategemeana na kiwango cha mchanga, kuna kiwango kikizidi hautaruhusiwa kujenga hilo eneo.
Huu ni uongo, ardhi ya mchanga ni nzuri sana, maana mchanga ni kama mawe tu ila ya size ndogo, hayavimbi na kusinyaa kama mfinyanzi hivyo si rahisi kujenga nyufa. Kumbuka particles za mchanga zimesha 'settle', tofauti na mfinyanzi ambao hutitia kipindi cha kiangazi, na kuvimba ukinyonya maji kipindi cha mvua, na hapo ndio nyumba hupata ufa
 
Tena hiyo ndio nzuri hasa, maana mchanga huwa hauvimbi na kusinyaa kulingana na majira (mvua/kiangazi) kama ufanyavyo udongo wa mfinyanzi. Maan kuvimba na kusinyaa kwa udongo husababisha nyufa kwenye kuta, na ndio maana watu huweka 'blinding layer' ya mchanga kwenye msingi ili kuepukana na hali hii.
Sio kweli ukijenga kwenye mchanga unahatarisha maisha yako na nyumba yako soma Mathayo 7:24-27 usikie Yesu anasema nini kuhusu kujenga nyumba juu ya mchanga.
 
Toa maelezo ya kina, kivipi. Labda kama wanazungumzia kujenga nyumba juu ya kifusi cha mchanga kilichomwagwa na lorry na hakija-'settle' bado
 
Huu ni uongo, ardhi ya mchanga ni nzuri sana, maana mchanga ni kama mawe tu ila ya size ndogo, hayavimbi na kusinyaa kama mfinyanzi hivyo si rahisi kujenga nyufa. Kumbuka particles za mchanga zimesha 'settle', tofauti na mfinyanzi ambao hutitia kipindi cha kiangazi, na kuvimba ukinyonya maji kipindi cha mvua, na hapo ndio nyumba hupata ufa
Unakaribiana na ukweli, ingawa sio kweli. Clay is better than Sandy.
What type of soil is good for a foundation for buildings or houses?
 
Tena hiyo ndio nzuri hasa, maana mchanga huwa hauvimbi na kusinyaa kulingana na majira (mvua/kiangazi) kama ufanyavyo udongo wa mfinyanzi. Maan kuvimba na kusinyaa kwa udongo husababisha nyufa kwenye kuta, na ndio maana watu huweka 'blinding layer' ya mchanga kwenye msingi ili kuepukana na hali hii.
Ahsante mkuu sikiwahi kufahamu kwaniniwatu hujenga na kuweka 'hardcore' na 'blinding layer'
 
Back
Top Bottom