ARDHI YA ZANZIBAR (2)
Ikiwa umuhimu wa kulinda ardhi ya Zanzibar utazingatiwa,basi cha kwanza ni kwamba ieleweke kwamba ardhi yake ipo LIMITED.
Maana yake hatuwezi kuongeza ukubwa Wa eneo kwa upande mmoja na huenda hata tukihitaji Hilo bado tutahitaji kujipanga katika πtechnology na knowledge ya kufanya reclamation ya bahari wenyewe.
Ni kweli kabisa kwamba Zanzibar iliwahi kufanya jambo hilo katika eneo la Darajani miaka ya nyuma sana kutoka company ya Netherlands/Holland.
Lakini je ni jambo rahisi sana? Kwamba halina gharama zake na fedha zitatoka wapi?
Suala jingine la kuzingatia kwenye utoaji wa ardhi Zanzibar ni suala la . Population growth ya Zanzibar.
kwamba idadi inaongezeka kila uchao na kuifanya Zanzibar kua high density population to compare with land.
Yaani βοΈ ile idadi ya watu inazidi ukubwa wa eneo! ndio maana ikiwa tutajikita kwenye kuangalia ardhi yake ni lazima kugusa pia kwenye uwekezaji. Kwamba ardhi wapewe wawekezaji ambao wako SIRIASIπ£
3. Zanzibar kuna Mipango miji mizuri lkn tatizo kubwa ni enforcement/implementation.
kuna zaid ya Mipango miji 4 je tumewahi kujiuliza utekelezwaji wake?kwamba umefanyika kikamilifu? Kuna ripoti?
Haya yote kwa ujumla wake ndio yanapaswa kuzingatiwa ndani ya visiwa na ikiwa kuna kasoro zozote zile zikiachwa madhara yake ni makubwa sana kama ifuatavyo:-
1. Wazawa kutokana na ugumu Wa maisha na hali ya umasikini walionao watabakia kua hawana ardhi kwa ajili ya π
1. makaazi.
2. β shughuli za kiuchumi na uzalishaji km vile kilimo, viwanda n.k
3. Maeneo ya kuzikia na kufanyia ibada.
4. Ukosefu Wa maeno ya wazi na michezo pamoja na mikusanyiko ya mikutano ya kisiasa, maafa na maombi ya jumla.
5. Kupoteza sifa za umiliki na matumizi ya ardhi hizo na kubakia kua ombaomba na kushindwa kuifanya kazi.
Unaweza kuona mifano halisi katika Vijiji ambavyo vipo nje ya manispaa ya mji wa Unguja. Kwamba wazawa hawana maeneo na hata maisha yao hayalingani na shughuli za uwekezaji uliopo pale.
Sikatai wamewauzia wenyewe wageni baadhi yao maeneo yao,lakini kwanini hakuna usimamizi kama ule wa Kamisheni ya utalii?
Kamisheni ya utalii mgeni ambaye anataka kupata hati ya umiliki wa eneo ni lazima awe na mzawa! Mzawa atamiliki 70% na mgeni 30%.
Ikiwa mgeni anaona hilo sio sawa kwake,kuna ZIPA ambayo ipo kwa ajili yao.kwamba hapo hahitaji kuwa patina na mzawa.
Sasa hata kwenye uuzaji wa maeneo wenyeji wajengewe Mazingira mazuri pia.
Shukran
Nitaendelea.