ukara
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 284
- 168
Utawala wa ukoo wa Gala Galauka chini ya Mtukufu ADUMBA umeinajisi ardhi ya Mbambadu na kwa jinsi hiyo yeye ndiye yeye, ana uwezo wa kufanya maamuzi ya kumpendelea yeye binafi hata kama kwa wengine maamuzi hayo yanageuka kuwa uchungu na si haki kwao
Mtukufu ADUMBA mtawala wa MBAMBADU kwa kushirikiana na maaskari wake watiifu wanashiriki kufanya dhuluma, utesaji, unyanyasaji na madhira ya kila namna kwa wananchi na raia wa ardhi ya MBAMBADU hasa wale wanaoonekana kwenda kinyume na mawazo na matakwa ya Mtukufu ADUMBA. Wengine wameamua kuwabatiza majina wale maaskari watiifu kwa Mtukufu ADUMBA kwa kuwaita vibaraka wa ADUMBA.
Wananchi wanaishi kwa hofu chini ya Mtukufu ADUMBA. Hiyo ndiyo nchi ya MBAMBADU inayoongozwa na ukoo wa Gala Galauka. Nchi yenye kila kitu, nchi yenye mito itiririshayo maji kwa mwaka, nchi yenye msitu mnene wa IGITA. Msitu uliojaa mizimu ya kila aina na wanyama wakali wa kila aina. Nchi ambayo wasichana hucheza ngoma ya NGOTENGOTE huku matumbo yao yakiwa wazi
Naam!!! Hii ndio nchi ya MBAMBADU chini ya mtawala ADUMBA wa ukoo wa Gala Galauka